miamiatz
JF-Expert Member
- Dec 4, 2017
- 505
- 941
Changamoto nambari moja inayotajwa kurudisha nyuma vijana wengi ni ukosefu wa mtaji. Ni kweli hii ni changamoto kubwa sana ila kuna kubwa zaidi ya hii. Twende pamoja katika makala hii na tuongeze mchango wetu kwenye comments.
Mimi changamoto ambayo naona ni kubwa zaidi kuliko ile ya ukosefu wa mitaji kwa vijana wa Tanzania ni uwezo wa kupembua soko, kuandaa upembuzi huo na kuuwasilisha vyema.
Kwanini nasema hii ni changamoto kubwa zaidi? Hebu fikiria unaposema huna mtaji halafu awepo mwenye pesa anataka kutoa pesa unadhani atakuuliza swali gani la kwanza?
Bila shaka swali la kwanza ni je soko lipo? Jibu la kijana hapa linatakiwa kushusha nondo za uchambuzi wa soko alioufanya na kuwasilisha makaratasi yenye maelezo ya uchambuzi huo.
Kama uchambuzi wako unaonesha wazi wazi kuwa bidhaa unayotaka kuizalisha ni dili hapa mjini bila shaka utapata mbia kwa haraka sana. Shida inakuja tu unapotafuta mbia mkajaribu biashara kama itafanikiwa ama haitofanikia.
Hii ni sawa na kumwambia mdada mzuuri, anaejiheshimu na aliejituliza kusubiri mume kuwa unataka kuwa nae ila huna hakika kama utamuoa ama la. Unataka mjaribu mahusiano kama yata work out. Unategemea jibu gani?
Hivyo basi kama kweli una nia na biashara flani na una uhakika wa soko andaa uchambuzi wake. Kama hujui unaanzaje kuchambua soko basi hatua ya kwanza unayotakiwa kuipitia ni kutafuta atakaeweza kukusaidia kuchambua soko na sio kukimbilia kutafuta mbia wa kutoa mtaji.
Nakaribisha comments za kuongezea mada hii.