Maswali muhimu kujiuliza na utakayoyatumia kama msingi wa majadiliano katika mada hii:
Mkuu Ansbert Ngulumo
Ulichokisema ni kweli tupu, mkuu wa mkoa kuagiza jeshi kufanya usafi mahali pote jijini Dar Es Salaam ina maana huwa hawana kazi za msingi za kufanya kuhusu jamii? Je usafi ni janga kiasi ambacho inahitaji ushiriki wa jeshi la wananchi?
MAJUKUMU YA MSINGI YA JWTZ
- Kulinda Katiba na Uhuru wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
- Ulinzi wa mipaka ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
- Kufanya mafunzo na mazoezi, ili kujiweka tayari kivita wakati wote;
- Kufundisha Umma shughuli za ulinzi wa Taifa;
- Kushirikiana na Mamlaka za Kiraia katika kutoa misaada ya kibinadamu na uokoaji wakati wa maafa;
- Kukuza elimu ya kujitegemea na uzalishaji kupitia Jeshi la Kujenga Tiafa (JKT); na
- Kushiriki katika shughuli za Ulinzi wa Amani Kimataifa.
Aidha wakati wa Amani, Kamandi ya Jeshi la Nchi Kavu ina wajibu mkubwa wa kuzisaidia mamlaka za kiraia katika kukabiliana na maafa pindi yanapotokea bila kusahau kutoa elimu kwa umma juu ya umuhimu wa Ulinzi na Usalama wa nchi na mipaka yetu dhidi ya adui yeyote awe kutoka ndani au nje ya mipaka ya Tanzania.
<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<<
9.5.2 Mapendekezo ya Watazamaji
Kimsingi, baadhi ya mapendekezo yaliyotolewa na watazamaji wa uchaguzi ni kamaifuatavyo: -(i) elimu ya mpiga kura iendelee kutolewa kwa vyama vya siasa, mawakala nawatendaji wa vituo;(ii) ushirikishwaji wa watu wenye mahitaji maalum katika uchaguzi uboreshwe;(iii) juhudi zifanyike kuboresha mazingira ya kufanya siasa;(iv) utaratibu wa kuwatambulisha mawakala wa vyama vya siasa upitiwe upya; na(v) sheria za uchaguzi zifanyiwe marekebisho katika maeneo yafuatayo: -(a) matokeo ya uchaguzi wa Rais yaruhusiwe kupingwa mahakamani;(b) wagombea wa Ubunge na Udiwani wanaopita bila kupingwa wapigiwe kura kama ilivyo kwa mgombea wa nafasi ya kiti cha Rais;(c) utaratibu unaotumika kuwateua Wajumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi ufanyiwe marekebisho; na(d) mawakala wa vyama vya siasa wapewe vitambulisho mapema kabla ya siku ya uchaguzi.
10.4.8.2 Mapendekezo ya Kuboresha Mwitikio wa Wapiga Kura
Washiriki wa zoezi la tathmini kutoka katika makundi ya wazee, vijana, watu wenyeulemavu na wanawake walipendekeza mambo yafuatayo ili kuboresha mwitikio wa104wapiga kura katika chaguzi zijazo. Baadhi ya mambo yaliyopendekezwa ni yafuatayo: -(i) elimu ya mpiga kura iwe endelevu na itolewe kwa muda mrefu zaidi kwa maeneoyote nchini hasa vijijini;(ii) asasi za kiraia na taasisi nyingine zinazohusika na utoaji wa elimu ya mpiga kuraziruhusiwe kutoa elimu endelevu;(iii) uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura uwe endelevu;(iv) watendaji wa Tume waendelee kusimamia uchaguzi kwa kuzingatia sheria, kanunina maadili ya kazi zao bila upendeleo; na(v) Tume ianzishe utaratibu wa kupiga kura kwa njia ya mtandao (electronic voting).
SURA YA KUMI NA MBILI
HITIMISHO NA MAPENDEKEZO
12.1 Hitimisho
Tume ya Taifa ya Uchaguzi iliendesha zoezi la Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 kwamafanikio. Mafanikio hayo yalitokana na hali ya amani na utulivu iliyokuwepo nchini nautekelezaji wa mipango iliyojiwekea. Mipango hiyo ilitekelezwa kwa kuzingatia Katiba,sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa.Katika maandalizi ya uchaguzi mkuu, Tume ilihakiki vituo vya kuandikisha wapiga kurana kuboresha Daftari la Kudumu la Wapiga Kura. Baada ya kukamilisha zoezi la uboreshajiwa Daftari, Tume iliandaa vituo vya kupigia kura. Vilevile, Tume ilifanya ununuzi nausambazaji wa vifaa vya uchaguzi, uteuzi wa watendaji wa uchaguzi na mafunzo, uteuziwa wagombea, kushughulikia rufaa za wagombea, uratibu wa kampeni za uchaguzi,utoaji wa elimu ya mpiga kura, kusimamia zoezi la kupiga na kuhesabu kura, kujumlishana hatimae kutangaza matokeo ya uchaguzi.Kwa ujumla, zoezi la Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020 liliendeshwa na kuratibiwa kwamafanikio. Aidha, maoni na mapendekezo mbalimbali ya watazamaji waliowasilishataarifa zao yanabainisha kuwa uchaguzi huo ulikuwa huru, wa haki na wa kuaminika.
12.2 Mapendekezo
Ili kuboresha uendeshaji wa uchaguzi, Tume inapendekeza yafuatayo: -(i) itungwe sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi ambayo itaiwezesha Tumekutekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi;(ii) kuwe na watendaji wa Tume hadi ngazi ya halmashauri;(iii) mamlaka husika ziangalie uwezekano wa kuunganisha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi,Sura ya 343 na Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292 ili kurahisishautekelezaji wa sheria hizo;(iv) sheria za uchaguzi zitafsiriwe kwa lugha ya Kiswahili; na(v) Serikali iangalie uwezekano wa kuziwezesha kifedha asasi na taasisi zinazotoaelimu ya mpiga kura katika hatua mbalimbali za mchakato wa uchaguzi.