Uchambuzi "Waite" Mrisho Mpoto

Uchambuzi "Waite" Mrisho Mpoto

Jamal naeem

Member
Joined
Jan 10, 2014
Posts
72
Reaction score
20
Nimejaribu kufatilia huu wimbo karibu miezi 5 ili kujuwa lengo la Mjomba maana huwezi kumsikiliza kwa mara moja ukapata majibu kwasababu hutumia sitiari na tafsida na aina nyingi tu za part of speech ila nimeyapata mawazo haya na kama kuna mtu anajuwa zaidi ya hapa basi si vibaya tukashare mawazo yetu.

Waite ukisikiliza kwa makini utunzi huu unakwenda na hali halisi ya nchi yetu kwa sasa. Ndio maana hata pale mwanzo inasikika beat ya wimbo wa taifa ikimaanisha "Mungu ibariki Tanzania na Wabariki viongozi wake hekima umoja na Amani."
Maudhui ya "Waite" yamegusa sehemu ya muungano wetu wa Zanzibar na Tanganyika ndani ya miaka 50 na Pamoja hatua za kuchukua ili muungano wetu udumu.
Mrisho Mpoto a.k.a Mjomba sio mwanasiasa lakini mashairi yake ya harakati dhidi ya jamii yake ambayo ni political consciousness.
Kitikio cha wimbo huu kimeanza kama ishara ya kuna watu wanapaswa kuitwa na watu fulani kama ifuatavyo.
"Waite wakalishe chini watoe hofu kwanza ,wambie wao hawamo japo nao walikula waite waite waite"
hii inaonesha wazi lazima tuwaite tuwatoe hofu maana wana woga kwa kitu ambacho walikula lakini itabidi tuwambie nyny hamumo ila tuweze kuishi kwa amani maana wana woga sana.

Mjomba anaanza kusema tabia ya binaadamu alivyo na hulka yake akifanyiwa mambo ambayo hayaendani na maisha yake.
"Mjomba chutama sisi ni waungwana na muungwana akivuliwa nguo mara nyingi huchutama." Pia mjomba anazidi kusema jinsi hali ilivyo kwa kusema haya.
"Kuna baadhi ya michezo ukishindana peke yako lazima uwe mshindi lakini kwa mchezo ule uliwahitaji kukuongezea mashabiki na washangiriaji wenye sauti zisizokauka".hii ina maana kwamba mchezo huu ni wa zanzibar na watanganyika wala si wa chama tawala peke yako CCM ndio maana ana mashabiki wengi na wenye sauti zisizokauka lakni mjomba kazidi kukumbusha kwamba "Mwiba wa kujichoma hauna pole" vilevile Mjomba anataka pia muungano wetu udumu kwa maneno haya"Tusitenganishwe na mto wakati kuna Ngarawa mjomba"
Pia mjomba anatufahamishe jinsi gani Zanzibar walivyoanza hadi hapa walipo kwa maneno haya.
"Walivyoanza hakuna aliyedhani kwanza walifika mapema mmoja wao akaandikisha jina lake kwa niaba ya wengine Japo wote wana majina yao na hayafanani, Jina lako nani? Mimi unatoka wapi kwetu unakwenda wapi?humu ndani kikazi binafsi nani? mimi aaaaaaaaaa wakaingia hujachelewa mjomba waite".kama tuvyojuwa Zanzibar ilipata uhuru wake 1963 kutoka kwa waingereza na walifanya mapinduzi yao 1964 hii ni mapema sana kama mjomba anavyosema maana hapo hata S.africa,zimbwabwe,Msumbuji wapo hawajapa uhuru wao ila znz ilipata mapema na Karume aliandikisha jina lake kwa niaba ya wazanzibar japo hakujuwa alikuwa kikazi au binafsi ndio maana mjomba anasema hawajachelewa lazima wawaite na wahoji.

Pia Mjomba anasema jinsi gani walivyoaminiwa Serikali ya Tanganyika na Zanzibar kwa kauli hii."Mjomba ukipewa kazi ya kuosha maiti siku zote wewe ni zaidi ya ndugu, wanaamini huwezi kuidhuru". Hii ni dhamana ya hali ya juu nadhani iko wazi.

Pia mjomba anazidi kutuambia jinsi gani viongozi wa Tanganyika wanavyofanya kazi kwa Zanzibar na pia mchango wa vyombo vyetu vya habari kama vile magazeti kwa kauli hii.
"Waliingia wakajipanga kwa sauti zao ya kwanza hadi ya nne wakaanzisha mapambio basi ikawa hivyo tu watu wakilia kazi yao wanatoa pole" mstari huu una maana kwamba awamu ya kwanza ya Nyerere hadi Ya nne Jakaya misiba ya zanzibar watu wakilia wao wanatoa pole tu kama ule wa mv spice, mv fatihi ndio maana wanajipanga kwa sauti zao ya kwanza hadi ya nne.

Ukija siku ya pili magazeti yetu husema hivi na mjomba anasema haya.
"Waandishi kwa utashi wao wakaandika msiba ulifana kweli hakuna aliyelia nje ya key" mjomba alicheka sana maana ujinga mtupu hapa inamaanisha kwamba msibani walifika viongozi wote wa kitaifa na hakuna hata mmoja alokosekana ndio maana hakuna aliyelia nje ya key.

Mjomba anazidi kutoa ushauri kwamba waite wakalishe chini watoe hofu kwanza kisha waambie muungwana hanuni kwa mashavu hununa moyoni. Tunajuwa wazi kwamba wazanzibar mfumo huu wa muungano wetu hawaupendi ila wengine wanashindwa kuonesha hisia zao mbele za watu kwa maslahi yao binafsi na kubakia kukaa kimya tu ila wanaumia ndani kwa ndani.
Ndio maana mjomba anazidi kusema haya.
"Waje tu kuwa mashahidi kwa kuwa na wao walikuwepo na walikula, japo kuwa hawakujua ulimtoa wapi mbuzi yule.
Mjomba anazidi kuwakumbusha Watanganyika kwamba.
"Ushahidi wao mjomba utakusaidia kwenye vitu viwili vya kwenye historia au kushinda kesi.
Pia Mrisho mpoto anatoa nasaha kwa viongozi wa Tanganyika kwamba.
"siku zote mjomba mimi huwa nakwambia anaekula kwa mikono miwili hawezi kushiba kamwe never. Hapa ndio ule msemo usemao Tanganyika imevaa koti la muungano kwa sababu anakula vitu viwili kwa wakati mmoja ndio maaana hawezi kushiba kamwe.
Mrisho mpoto lakini pia anasema na yeye anakumbuka aliiona Zanzibar kwa maneno haya.
"Mimi pia nakumbuka nilimuona alikuwa mbuzi(znz)tena mdogo. Na mwisho mjomba anasema kuna aina tatu tu za kujibu maswali.
 
nashukuru kwa uchambuzi wako ila mimi imenigusa tofauti na kademu kangu kalikonimwaga kwa tamaa ya fedha huo wimbo ni kama umemgusa
 
  • Thanks
Reactions: o_2
Nimekuelewa sana siku nyingine ukija njoo na 'salaamu kwako' ya huyo huyo jamaa
 
Kwa kuendelea kidogo Mjomba anaendelea ''kuna aina tatu za kujibu swali yani swali kwa swali (kama yesu) swali kwa mkato au swali kwa maelezo,''
elimu nyingine sio mpaka uiingie darasan, Big up kwa Mjomba na mchambuzi¡
 
Shukran mkuu..sasa nimepata mwanga wa nini Mpoto alimaanisha
 
acheni fix hakuna alicchochambua wimbo huu wala hauendani na muungano ni ishu nyingine tofaut kabisa. Mimi ni mtaalam kwenye fasihi i can read mesage behind the mesege so ngoja kuna novel namalizia then ntashusha uhakiki wa huu wimbo sio hiki mlichosoma sikilizeni wimbo vzur
 
dah! waite sio nyimbo ya siasa bali mjomba anakumbushwa matukio na marafiki zake.
 
acheni fix hakuna alicchochambua wimbo huu wala hauendani na muungano ni ishu nyingine tofaut kabisa. Mimi ni mtaalam kwenye fasihi i can read mesage behind the mesege so ngoja kuna novel namalizia then ntashusha uhakiki wa huu wimbo sio hiki mlichosoma sikilizeni wimbo vzur
Ndugu karibu utupe madini imekuwa kitambo sasa.
 
acheni fix hakuna alicchochambua wimbo huu wala hauendani na muungano ni ishu nyingine tofaut kabisa. Mimi ni mtaalam kwenye fasihi i can read mesage behind the mesege so ngoja kuna novel namalizia then ntashusha uhakiki wa huu wimbo sio hiki mlichosoma sikilizeni wimbo vzur
Ni kweli kabisa mkuu
 
Back
Top Bottom