Uchambuzi wangu Simba vs Yanga

monta

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2014
Posts
1,271
Reaction score
1,803
#NgaoYaJamii

FT: Simba 0-1 Yanga
Mayele 11'[emoji460]

-Nimekitizama kikosi cha Yanga Wanamabadiliko makubwa sana kulinganisha na Mchezo wao wa mwisho walio ucheza dhidi ya Simba wamefanya usajili mzuri sana naamini wakicheza Kwa pamoja kwa muda mrefu watakua tishio

-Simba wanaonekana kuna Quality flani imepungua katikati ya uwanja mahali alikokuwa akicheza mwamba wa Lusaka (Chama) sasa anacheza Lary Bwalya ,Bwalya muda mungi anaonekana hayuko kwenye eneo sahihi la Namba 10! Muda mwingi anashuka sana chini na kumwacha Mugalu pasina na usaidizi nyuma yake

-Konate kacheza vizuri mno kwenye Jukumu la Box to Box Midifilder ila Naamini Bwalya ni mzuri zaidi katika position ile

-Mugalu a Complete striker japo kapata nafasi nyingi zakufunga ila hakufunga Kacheza vizuri mno alikua msumbufu kwenye backLine ya Yanga ila hakuwa na usaidizi hasa kipindi cha kwanza,hana bahati na nyavu

-Nimependa Goli ya Yanga Movement + Passing vyote kwa pamoja Muloko +Farid + Mayale [emoji91][emoji91]

- Khalid Aucho vs Yannick .Bangala wamenivutia sana leo usajili mzuri Vita yao na Thadeo Lwanga +Konate imenivutia japo kulikuwa na matumizi makubwa ya nguvu baina ya viungo hao jambo lililo pelekea wote kupata kadi za njano na Lwanga Redcard

NB:
-Huyu Dikson Job ni bongemoja la Center Back jinsi anavyo Paform kwenye mechi kubwa kama vile alikuwepo Yanga miaka 6 nyuma,...Ningumu sana Mchezaji hasa wa umri wake kuonyesha kiwango bora Kila mechi anayo cheza tena dhidi ya timu kubwa Credity kwake [emoji91]

-Dijgui Diarra kuonyesha uwezo mkubwa sana hasa kuanzisha mashambulizi,anajua nini anafanya(aliwahi kuwa kiungo kabla ya kuwa goalkeeper)

-Kennedy Juma kafanya kazi yake vema sana eneo la ulinzi

-Peter Banda ni Nchimbi mfupi

MWISHO wa Uchambuzi Kwenu Studio [emoji847]
 
Mpira umeanza kuuchambua tangu liniπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Hiyo ya pili kutoka mwisho subiri kiama chako kutoka kwa Makolo[emoji16][emoji1787][emoji16]...kimya ni vile tu kwa usiku huu hawatofungua data,maneno mengi hawana shughuli[emoji16][emoji16][emoji16]
 
Nilijua tu Simba tutasingizia Chama na Miquison. Ila ukweli Yanga walitufunga tukiwa na Chama na Miquison kabla ya mechi ya Kigoma.

Watani walikamia hii mechi. Ila bado Simba tupo imara kila idara.

Yanga ni bora asichukue kombe au afungwe na Lipuli ila sio Simba.
 
Huyo Banda unamuonea bure aisee
 
Comment Mujarabu Kama Alkasus
 
Kwa sababu zilizo nje ya uwezo wangu... Leo hatuwezi kuongelea habari za mpira
 
Simba watakuwa Mabingwa kwa sababu watashinda 90% ya mechi zao ili hali Yanga watapoteza kwa timu ndogo kama Polisi, Prison, Ruvu JKTn.k.
 
Kufungwa ni jambo moja na kucheza mpira ni jambo lingine.

Simba ya sasa wasahau biriani....baada ya kumkosa Miquison Chama angebaki walau msimu mmoja ndio aondoke.

Hata kama Simba ilikuwa inapoteza lakini kipute kilipigwa kisawasawa...Wapinzani walikuwa wanapumulia mashine muda wote.
 
Mechi za Darby huzijui wewe ngoja ligi ianze mechi za mwanzo tu utaona vitu tofauti kabisa na vya kwenye Darby ya hizi timu mbili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…