Alfu Lela U lela
JF-Expert Member
- Dec 30, 2016
- 319
- 542
Yaani nipoteze muda wangu kuainisha vitu ambavyo vipo wazi?!!!, au ukiambiwa haki unaelewa nini?Unaweza kuziainisha kinagaubaga haki hizo zilizopotezwa?!!
Yaani nipoteze muda wangu kuainisha vitu ambavyo vipo wazi?!!!, au ukiambiwa haki unaelewa nini?Unaweza kuziainisha kinagaubaga haki hizo zilizopotezwa?!!
Ambazo 2015 Hadi March 2021 zilikuwepo, au sio?!!!! Mama tu huyu ndo kaja kuziondoa?!!Yaani nipoteze muda wangu kuainisha vitu ambavyo vipo wazi?!!!, au ukiambiwa haki unaelewa nini??
Huyo mpuuzi hakustahili reply yako!Sehemu yoyote isiyo na haki usitegemee amani iwepo, hii nchi ilivyo sasa ndo matokeo ya walichokipanda, na bado kuna mengi tutayashuhudia, ogopa sana raia wakiwa hawana imani tena na Serikali yao, ni hatari
Kaka mshana, kuna watu wanatia hasira mpaka kuna muda unajiuliza hawa kweli ni watanzania wenzetu au wametumwa!Huyo mpuuzi hakustahili reply yako!
Kuna chuki kubwa sana hapo inajengwa mioyoni mwa Watanganyika.. Na chuki Ina hulka ya kumea na kukomaa ama kutunga mimba na kuzaa
Gang battle, sasahivi chuki iliyopo kati ya wananchi na vyombo vya ulinzi na usalama,,, haimuliki popote na hizi gang battle huwa haziishi kiufupi wajiandae kulipa gharamaKuna chuki kubwa sana hapo inajengwa mioyoni mwa Watanganyika.. Na chuki Ina hulka ya kumea na kukomaa ama kutunga mimba na kuzaa
Kakaka tatizo letu tupo so reactive.Neno la utangulizi ( preamble)
BILA SERIKALI KUWAJIBIKA.. RECONCILIATION haina maana yoyote
.Kuwajibika kwenye uchafuzi wa kura uliowanyima mamilion ya Watanganyika haki yao ya kuchagua na kuchaguliwa
. Kuwajibika kwenye kupika matokeo ya uchufuzi wa kura.. Yenye kutia kinyaa na aibu kubwa
. Kuwajibika kwenye uharibifu mkubwa wa mali na miundombinu
.Kuwajibika kwa majeruhi waliokuwa wanatumia haki yao ya kikatiba kupaza sauti
.Kuwajibika kwa vifo vingi vilivyoyokana na wananchi waliotumia haki yao ya kikatiba kuandamana
. kuwajibika kwa kuwanyima majeruhi wote nafasi ya kupata matibabu
.Kuwajibika kwa marehemu wote waliokosa staha na heshima kwenye kuhifadhiwa
.Kuwajibika kwa kuwazuia ndugu na jamaa kupata taarifa za wafiwa na majeruhi
. Kuwajibika kwa kuzima mtandao kwa masaa yasiyopungua 80
Mtazamo wangu kwenye maandamano
Maandamano yalikuwa ya kimkakati na yaliyopangiliwa vema
1. Kupaza sauti kupitia kutoa futuko la hasira ya muda mrefu kwenye miundombinu ya mwendokasi... Simulizi za kunyanyasika na huu usafiri kwa muda mrefu wanazo wakazi wa Morogoro road.. Mbagala wameunganishwa humo humo
2. Kupaza sauti kupitia uwekezaji wa wasanii.. Hawa walionekana mas nitch wasaliti waliojivuna na kutoa lugha za kashfa kwa wananchi huku wakikumbatiwa na mamlaka
3. Wawekezaji na wafanyabiashara ambao mali zao zimejaa utata na harufu ya rushwa huku wakiwa bega kwa bega na utawala unaolalamikiwa sana
4. Viongozi wa kisiasa wa chama na serikali waliothibitisha kwa kauli na matendo kwamba wamedharau vilio cya wananchi kwa muda mrefu
5. Majengo ya serikali hasa TRA NA POLISI na MAHAKAMA. haya habari zake si ngeni kwenye unyanyasaji wa wananchi, kubambikiwa kodi, kesi na kuwanyima watu haki zao
Waandamaji wanaotajwa kutoka nje ya nchi hawakuwa wengine bali watanganyika wa
Dini zote
Imani zote
Vyama vyote
Makabila yote
Jinsia zote nknk
Tukumbuke hata wana ccm kwa wingi wao walishiriki haha maandamano kutokana na kutoridhishwa na yote yaliyotokea kwenye chama chao
Vyombo vyote vya ulinzi na usalama walau kwa kificho walikuwa sehemu ya maandamano huku wakiwatia wananchi hamasa moto na kuwapa mbinu mbalimbali za kuandamana!
Naendelea sehemu ya pili
Hakuna Maridhiano na shetani, awamu ya pili ya kuikomboa Tanganyika I mean a upyaaa. Sasa siyo makaratasi tena liundwe Jeshi kabisa.Sehemu ya pili
Serikali imepanga kufanya maridhiano. Lakini je imeshafanya tathmini ya kutosha juu ya hayo yalitokea?
Je inataka kufanya maridhiano na nani?
Na wana ccm?
Na CHADEMA?
Na wote waliopoteza ndugu zao kwenye utekaji au maandamano?
Na WATANGANYIKA? as special case?
Na waumini wa dini mbalimbali
Na vyombo vya usalama vyote?..
Yote hayo ni makundi lakini yenye msingi mmoja mkuu wa mwananchi Mtanganyika!
Mafunzo ya kuzingatia
1. Kwa wasanii simameni na wananchi katika nyakati ngumu.. Pesa za wanasiasa sio baba lakini sio nyingi kama za wananchi wanaowafanya muonekane kwa wanasiasa
2. Wanasiasa wa ccm. Msijione kwakuwa mmehodhi maradaka kwa nguvu basi mnaweza kuhodhi ngumu ya uma na hisia wa wananchi
3 . Kwa wafanyabiashara hakuna anayewapangia utashi wa kisiasa lakini mambo mengine fanyeni kwa siri kubwa kwakuwa wateja wetu ni wa vyama vyote
Tamati yangu!
Wasomi waliosimamia mchakato wa uchaguzi wametutia aibu kubwa kama taifa.. Sana wanastahili kuwajibika maramoja kabla ya maridhiano yoyote yale!
Wametanguliza maslahi binafsi na ya wachache kwa muono wa kisiasa na kipindi kifupi cha miaka mitano badala ya picha kubwa ya Tanganyika
Wafaidikaji wa mwisho waliokaa kimya lakini wanaochekelea! Wakandarasi watakaopata kandarasi za kukarabati miundo mbinu yote iliyoharibiwa.. Wanasema kufa kufaana. Ni msimu mwingine wa mavuno
Wenye maumivu makubwa
Kampuni za bima ambazo zitapaswa kuwalipa wote waliokuwa na bima kubwa zinazojumuisha majanga ya moto na ya kibinadamu
Wengine ni wafiwa wote waliopoteza ndugu zao ambao walikuwa tegemewa
Huu ni mwanzo mpya wa yatima na wajane! Ndoto nyingi zilizozimwa na wanasiasa waroho wa madaraka.. Baada ya muda kuna simulizi nyingi za kuumiza sana zitasimuliwa
Je mpaka hapo unaamini katika maridhiano?
wako tayari hata kula mavi ya abdulNi machawa wasiojitambua