GE2025 Uchambuzi wangu: Yatokanayo na maandamano ya Oktoba 29, 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Sehemu yoyote isiyo na haki usitegemee amani iwepo, hii nchi ilivyo sasa ndo matokeo ya walichokipanda, na bado kuna mengi tutayashuhudia, ogopa sana raia wakiwa hawana imani tena na Serikali yao, ni hatari
Huyo mpuuzi hakustahili reply yako!
 
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Boniface Mwabukusi, ametoa wito kwa vyombo vya kimataifa kuchukua hatua za haraka dhidi ya watu wote waliopanga, kufadhili na kutekeleza vitendo vya mauaji, utekaji na upotezaji wa Wananchi kabla, wakati na baada ya uchaguzi.

Kupitia kauli yake, Mwabukusi amesema kuwa mazungumzo yoyote ya kisiasa hayawezi kuanza bila uwajibikaji, akisisitiza kuwa wale wote waliotajwa katika matukio hayo wanapaswa kukamatwa na kufikishwa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) kwa makosa ya uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Aidha, ameitaka Serikali kuhakikisha kuwa watu wote waliotekwa na kupotezwa wanarejeshwa na kuunganishwa na familia zao, huku akisisitiza kuwa kesi zote za uonevu dhidi ya viongozi wa CHADEMA, akiwemo Tundu Lissu, ziondolewe mara moja.

“Kabla ya mazungumzo, lazima kila mmoja abebe msalaba wake. Hakuna kusafishana. Kila aliyehusika na mauaji haya ya raia wasio na hatia awajibishwe kwanza,” amesema Wakili Mwabukusi, akiongeza kuwa kutaka mazungumzo kabla ya uwajibikaji ni sawa na kuhalalisha udhalimu na kuwatukana waliouawa bila hatia.

#WananchiForum #UhuruWaHabari #ToThePeople #ForThePeople #ByThePeople #UhuruWaMaoni
 
Kuna chuki kubwa sana hapo inajengwa mioyoni mwa Watanganyika.. Na chuki Ina hulka ya kumea na kukomaa ama kutunga mimba na kuzaa
Kuna chuki kubwa sana hapo inajengwa mioyoni mwa Watanganyika.. Na chuki Ina hulka ya kumea na kukomaa ama kutunga mimba na kuzaa
Gang battle, sasahivi chuki iliyopo kati ya wananchi na vyombo vya ulinzi na usalama,,, haimuliki popote na hizi gang battle huwa haziishi kiufupi wajiandae kulipa gharama
 
Babaake ALITEKWA mapema mwaka huu na jeshi la Polisi, mamaake amekutwa amefariki BAFUNI kwa kupigwa na risasi.

Huyu dogo na mdogo wake wa kike kwasasa ni Yatima. Watasomaje, watakula nini basi ni wao watajua bila kujali umri wao.

Hii ndio hali halisi ya familia nyingi kwasasa Tanzania. Haya ndio maumivu ambayo vijana wa taifa la kesho wanabeba vifuani mwao.

Poleni sana wa dogo zangu Mungu awe nanyie Katika kipindi hicho kigumu
 
Kakaka tatizo letu tupo so reactive.
 
Hakuna Maridhiano na shetani, awamu ya pili ya kuikomboa Tanganyika I mean a upyaaa. Sasa siyo makaratasi tena liundwe Jeshi kabisa.
 
Hii ni nchi yetu sote ... kuna dhana ovu imejengwa na mtawala kujiona nchi ni ya kwake na anauwezo wa kufanya alitakalo ... Kwa mauwaji yale ? Leo unasema malidhiano ?? Mbona wale waliokuwa wanaimba NO REFORM NO ELECTION mbona hawakusikilizwa mapema ?? Au mtawala alijidanganya ni wimbo wa CDM pekee ?? Mtawala kumbuka mtanzania huyu wa leo sio wa enzi za mwalimu . Damu ya watu sio nzuri na huwa inarudisha majibu mabaya sana ....SIO KWAMBA WATU HAWAKUKUSHAURI KABLA ILA ULIWAPUUZA .. sana hivi hayo maridhiano utafanya na nn ?
 
Unaharibu, unaua, unanyanyasa, unateka na kubagaza mali za umma kwamakusudi alafu unatangaza maridhiano kwamba sisi niwajinga kiasi gani mpaka tukubaliane nahayo maridhiano
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…