nafikiri unahitaji elimu ya nini nini maana ya mkoa, wilaya, tarafa, jimbo, kata halafu ndio utaweza kuchangia hoja yako vyema. Kwani huwezi kuzungumzia ngazi ya kata katika mkoa kama ulivyofanya na ukaacha kutaja kata husika ipo katika wilaya ipi, jimbo lipi la uchaguzi n.k.
Nahisi habari zako ni za kusikia, kuhisi au kutunga. Kibaya zaidi umeshindwa kutupatia reference za mkoa upi unazungumzia, kata zipi zimechukuliwa na chadema na zipi ccm na idadi ya kura za kikwete na slaa kwa mujibu wa tume katika kata unayozungumzia.
Kabla ya uchaguzi wa 2010, wachangiaji hapa walikuwa wakija na data kamili lakini katika kipindi cha uchaguzi na baada kuna watu wanaonekana kuleta hoja bila uthibitisho. Hii ni hatari katika kipindi hiki cha kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi, kwani mnaweza kuleta uchochezi na kuhatarisha amani na tutlivu tulionao.
Tatizo la wengi wetu tulishiriki katika uchaguzi huu kishabiki tu, wakati naomba kura za wagombea wa chadema mtu kwa mtu wapo wengi waliniahidi kuwa watamchagua mnyika na diwani wake lakini kura watampa kikwete, wapo wengine waliniahidi kuwa watamchagua mnyika kama mbunge lakini uraisi watampa kikwete na udiwani walisema hajaamua kwa kuwa dmgombea udiwani wetiu alikuwa mgeni kidogo.
Hata katika kuhesabu kura matokeo yalionyesha mnyika alikuwa akizidi kura za dr slaa kuthibitisha kuwa hata waliomchagua kikwete katika ubunge walimchagua mnyika. Hapa sisemi kuwa kura za dr slaa hazikuibiwa, ndio maana ni vyema kusubiri kauli ya chadema kama alivyoahidi marando kuwa watataja ni katika vituo vipi, majimbo yapi kura za dr slaa zilizotangazwa na tume ya uchaguzi zintofautiana na zile zilizokwenye fomu za matokeo zilizosainiwa na wasimamizai wa vituo na mawakala.
This is home for great thinkers, leteni vitu vyenye uthibitisho.