Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Suala la walimu kudhibiti nidhamu kwa wanafunzi ningependa kukujibu kuwa wajibu wa kuwalea watoto ni jukumu la wote na linaanza kwanza na wewe mzazi.sasa wewe toto limekushinda,limezibuka hakina adabu wala heshima wala staha kwa watu na ubaliangalia tu kama sanamu pasipo kuchukua hatua zozote zile ndio unataka yeye mwalimu alidhibiti kwa njia zipi wakati wewe mzazi unayelala nalo nyumba moja na kula nalo ugali limekushinda? Unataka mwalimu akalipige kwa rungu kuzibua kichwa ? Malezi bora yanaanzia kwako mzazi na siyo kumtupia lawama mwalimu.Ajenge mifumo, wizara isiende kwa upepo wa waziri tu, akija mwingine inayumba.
Hao mafundi mchundo wanaojenga shule, kuna mfumo upi wa kuangalia ubora wa kazi zao? Maana injinia wa Halmashauri ni mmoja, hawezi fuatiloa kila hatua ya jengo.
Simsikii akijenga ajenda kuhusu ukusanyaji mapato, fedha ndio injini ya nchi, ni kwa namna gani anadhibiti mapato ya halmashauri? Tunataka halmashauri iwe imara kwenye kukusanya mapato, na akiwa ziarani, akague vyanzo vya mapato, na aelezewe vyanzo vipya vilivyobuniwa.
Pia upande wa shule za serikali kuna malalamiko waalimu hawadhibiti nidhamu ya wanafunzi.
Asipojenga mifumo, ataonekana kaja kufanya zimamoto kwa ajili ya uchaguzi.