Ajenge mifumo, wizara isiende kwa upepo wa waziri tu, akija mwingine inayumba.
Hao mafundi mchundo wanaojenga shule, kuna mfumo upi wa kuangalia ubora wa kazi zao? Maana injinia wa Halmashauri ni mmoja, hawezi fuatiloa kila hatua ya jengo.
Simsikii akijenga ajenda kuhusu ukusanyaji mapato, fedha ndio injini ya nchi, ni kwa namna gani anadhibiti mapato ya halmashauri? Tunataka halmashauri iwe imara kwenye kukusanya mapato, na akiwa ziarani, akague vyanzo vya mapato, na aelezewe vyanzo vipya vilivyobuniwa.
Pia upande wa shule za serikali kuna malalamiko waalimu hawadhibiti nidhamu ya wanafunzi.
Asipojenga mifumo, ataonekana kaja kufanya zimamoto kwa ajili ya uchaguzi.