Habari zenu wadau wa JF, siku zote nimekua najiuliza Sana hili suala la imani za ushirikina/ uchawi. Kiukweli nabaki njia panda pale ninaposikia wachawi wanauwezo wa kuingia ndani ya nyumba wakafanya wanachotaka na wakatoka bila kuonekana, hata wakitaka kusafiri wanasepa tu kiulaini kabisa. Ebu tujiulize kwanini/ iweje wanashindwa kufanya uchawi kwenye magereza wanapofungwa wanashindwa kutoka na kurudi makwao? Mwenye ufahamu na hili tudadavulie!! Naomba kuwasilisha......[emoji120]
Mkuu aya mambo yapo mpaka uko....
Around 2007 kipindi cha operation ya kufagia majambazi kuna Jambazi mmija mkubwa alikamatwa Tanga akatupwa Mahabusu Maweni.......
Kama wiki hivi siku jamaa akaamka na furaha zake akawaaga wadau mpaka na askari akawaambia leo Mama yake anakuja kumchukua, unaambiwa usiku ilipiga mvua moja ya hatari nasauti za paka kwa wingi, asubui jamaa akuwe na kuna nondo ya juu kwenye dirisha ilikutwa imepinda kidogo, jiulize amepitaje na ukizingatia gereza lilikua limezungukwa na katani......