Uchawi na ushirikana tanzania: Kwanini???

Uchawi na ushirikana tanzania: Kwanini???

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Ndege alieleta barua,[/TD]
[TD="class: tr-caption"][/TD]
[TD="class: tr-caption"][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Akiwa ametulia baada ya kufikisha ujumbe.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]



Tanzania ni nchi iliyoko Africa Mashariki. Ni nchi pekee yenye makabila mengi na idadi kubwa ya watu kuliko nchi nyingine ktk Africa Mashariki. Kwa miaka mingi wakazi wengi wa nchi za Afrika mashariki wanaamini ktk uchawi na ushirikina. Hata hivyo tafiti zinaonesha kuwa watanzania wengi wanaamini ktk uchawi na tiba za jadi kuliko wenzawo ktk afrika mashariki.

Katika maeneo mengi uchawi umekuwa ukitumika kutoa tafsiri kwa mambo ambayo hayaelezeki mfano mtoto mgonjwa sana au gojwa geni.

Mauaji ya albino miaka michache iliyopita ni ushahidi tosha kuwa imani za kishirikina zimeshamiri tanzania. Mauaji ya vikongwe ktk miji iliyoko kanda ya ziwa hasa mikoa ya Shinyanga ambapo inakadiriwa kuwa zaidi ya watu 600mwaka 2011 waliuwawa kwa hisia kuwa ni wachawi ni ushahidi mwingine.


Ukitembelea miji mikubwa ya Dar es Salaam, Arusha na Mwanza utashangazwa na wingi wa mabango ya waganga. Ni jambo la kusikitisha sana, wakati wenzetu wakitia juhudi ktk technolojia sisi tunashamiri ktk uchawi.

Tafiti zinaonesha kuwa 60% ya watanzia hutolea sadaka mababu ili kupata mafanikio ktk maisha, lakini pia ktk idadi hiyo wakiwemo wakristu na waislamu. Magonjwa mengi yanayotibika watu wengi huamini ktk kurogwa. Magonjwa kama malaria, UKIMWI, magonjwa ya akili kwa watanzania wengi ni kurogwa. Tumeshuhudia wagonjwa wengi wakiacha dawa zao na kwenda kwa waganga au kwenye maombi.
Hata baadhi yetu tumekuwa tukikatazwa kwenda kuwatembelea baadhi ya ndugu kwa kuamini kuwa ni wachawi wanaweza kuturoga.

Uchawi tanzania umetumika kuelezea mafanikio ktk mpira, sanaa,na biashara.

Kwanini uchawi umeshamiri tanzania?
Kuna nadharia nyingi kujibu swali hili. Mojawapo ni kuwa tanzania haikutawaliwa kwa muda mrefu na wakoloni kuliko nchi nyingine za Afrika.

Lakini pia elimu. Bila watu kupata elimu ni rahisi kufuata ushirikina na kurithisha imani hizo kwa vizazo vinvyofuata.


Sababu nyingine ni Umaskini. Watu wengi wanatafuta utajiri kwa njia za mkato. Hivyo hufanya waamini kuwa wakitumia viungo vya binadamu huweza kufanikiwa.

Ubora wa huduma za afya. Hii ni sababu mojawapo ambayo hufanya watu wengi waende kwa waganjwa wa jadi. Katika vituo vingi vya afya hakuna vifaa, wataalamu na madawa ya kutosha.


Madhara ya Imani za kishirikina.
Mojawapo ya madhara ni mauaji. Mauaji yanayolenga kundi au jamii ya watu fulani kama albino,vikongwe au watoto waliozaliwa pacha.Lakini pia ongezeko la vifo kutokana na magonjwa yanayotibika. Watu wengi wamepoteza maisha kwa kucheleweshwa kufikishwa ktk huduma za afya.Madhara mengine ni kuongezeka kwa makosa ya jinai.

Pia ongezeko la usugu wa dawa hasa za HIV na antibiotics nyingi ni kutokana wa watu kukatisha tiba baada ya kuanzishiwa dawa jadi.

Suluhisho kubwa ni serikali kuimarisha mfumo wa elimu. Kuhakikisha sayansi inatiliwa mkazo. Lakini pia serikali kuboresha miundombinu ktk vituo vya afya. Hakuna sababu ya wagonjwa zaidi ya mmoja kutumia kitanda kimoja au kukaa foleni masaa manne wakisubiri kumuona mtoa huduma ya afya.

 
Back
Top Bottom