Heri,
Wote tulizaliwa tukijua tumegawanyika sehem tatu yaani roho,nafsi na mwili kwa mujibu wa kitabu.Ila kusudi la Muumba lilikuwa wote tuwe MOYO (moyo safi) kwa mujibu wa mathayo 5:8 (Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu.) na mithali 4:23 (Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.)
Muumba alituumba tuweze kumiliki na kutawala vinavyoonekana na visivyoonekana kwa mujibu wa
Zaburi 8:4-6
4 Mtu ni kitu gani hata umkumbuke, Na binadamu hata umwangalie?
5 Umemfanya mdogo punde kuliko Mungu; Umemvika taji ya utukufu na heshima;
6 Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; Umevitia vitu vyote chini ya miguu yake.
Badala yake baada ya dhambi visivyoonekana ndio vikawa na nguvu na ndo vikawa vinatutawala na kuendesha uumbaji.
Warumi 7:17
Basi sasa si mimi nafsi yangu ninayetenda hilo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu.
Isaya 26:13-14
13 (Ee Bwana, Mungu wetu, mabwana wengine zaidi ya wewe wametumiliki; lakini kwa msaada wako peke yako tutalitaja jina lako.
14 Wao wamekufa, hawataishi; wamekwisha kufariki, hawatafufuka; kwa sababu hiyo umewajilia, na kuwaangamiza, na kuupoteza ukumbusho wao.)
Je ni nini kilisababisha hayo yatokee?
Wote tulizaliwa tukijua tumegawanyika mara tatu yaani Roho,nafsi na mwili, maana yake nini?
Ukiwa roho ilikuwa ni kuugua tu
Warumi 8:23
Wala si hivyo tu; ila na sisi wenyewe tulio na malimbuko ya Roho, sisi pia tunaugua katika nafsi zetu, tukikutazamia kufanywa wana, yaani, ukombozi wa mwili wetu.
Ukiwa nafsi ilikuwa ni kubeba uchafu tu
Marko 7:21-22
21 Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati,
22 wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu.
23 Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi.
Ukiwa mwili ilikuwa kuwa na uadui na Muumba wako.
Warumi 8:7
7 Kwa kuwa ile nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, kwa maana haitii sheria ya Mungu, wala haiwezi kuitii.
Utendaji wa roho, nafsi, mwili na asili ilikuwa ni kuibiana vipawa na viwekezo hasa wale wenye maarifa,kuishi maisha ya mwengine huku yeye akiteseka,unafunga nyumba yako lakini mtu anajigeuza mjusi au panya au kutoonekana anaingia na kufanya yake.
Ilikuwa haiwezekana kuwa msafi wa moyo kama ukiwa ni roho,nafsi na mwili maana ulikuwa huwezi kutenda kile unapenda.Ni Muumba peke yake ndiye anayeweza kutufikisha kwenye usafi wa moyo ili aishi yeye ndani yetu.
Isaya 57:15
Maana yeye aliye juu, aliyetukuka, akaaye umilele; ambaye jina lake ni Mtakatifu; asema hivi; Nakaa mimi mahali palipoinuka, palipo patakatifu; tena pamoja na yeye aliye na moyo uliotubu na kunyenyekea, ili kuifufua mioyo ya wanyenyekevu, na kuifufua mioyo yao waliotubu.
Ukiwa roho,nafsi,mwili na asili ulikuwa huwezi tenda vile unapenda sababu kulikuwa na wanaokumiliki na kukufanya wewe kiti chao kwa kujua ama kutokujua.
Warumi 7:15
15 Maana sijui nifanyalo, kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; bali lile nilichukialo ndilo ninalolitenda.
18 Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati.
19 Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati.
Hupendi uzinzi ila unajikuta umezini,hupendi kutoka nje ya ndoa yako unajikuta umeshachepuka,hupendi uongo ila unajikuta unadanganya,hupendi ulevi ila unajikuta unakunywa pombe,hupendi wizi ila unajikuta unaiba,hupendi umalaya ila unajikuta unajiuza
Je haya yote yamekujaje?
Ni kutokana na uumbaji wote kuwa kwenye uteka ndo maana watakatifu wote walishindwa kufikia kwenye usafi wa moyo (MOYO SAFI).
Warumi 8:20
20 Kwa maana viumbe vyote pia vilitiishwa chini ya ubatili; si kwa hiari yake, ila kwa sababu yake yeye atiyevitiisha katika tumaini;
Je KUSUDI ni nini?
Muumba alitukusudia tuwe MOYO yaani wasafi wa Moyo( Clean heart) hapo mabaya hayakai.Bila ya kukaliwa na mzimu wowote au jini lolote au maruhani yeyote,uwe wewe kama wewe ulivyoumbwa bila kuning’iniwa na uchafu wowote au mtu yeyote.
Mithali 4:23
Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo; Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.
Mathayo 5:8
Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Muumba.
Je Moyo maana yake nini?
Nikisema Moyo sio huu unaopelekwa India kupasuliwa lahasha bali ni muonekano wako wote ndio ulikusudiwa uwe MOYO na yale mema na mazuri uyapendayo.