Uchawi ulivyotamalaki milima ya Same Upareni

Uchawi ulivyotamalaki milima ya Same Upareni

Neno kushana maana yake Ni ku unda au ku mould au kutengeneza. Ukoo wa washana ndio walikua wanatengeneza au kufua vyuma na kutengeneza zana Kama panga, jembe n.k.
Utaalamu huu ulihusishwa na uchawi na ilikua Siri yao tu, yaani hawakuruhusu ukoo mwingine ujue kuunda zana ili ku protect hiyo trade yao.
Ndio maana ukoo unaoogopwa kwa uchawi upareni Ni washana. Zamani watu wa Koo nyingine waliepuka kuoa washana kwa sababu za kishirikina. Hata Sasa wanaojielewa hawaoi washana.
Mshana Jr correct me kabla sijaanza kutaja Mambo ya milango
Ni kama Sisi Kwetu kuna Koo moshi kibosho inaitwa Kiria na wakiendelea wanajiita Moria walikuwa wafua chuma na nikoo iliyokuwa ikifharaulika sana
 
Nimezaliwa Makanya
Nimekulia na Kusomea Makanya kuanzia chekechea, shule ya msingi mpaka Kidato cha nne,
Niliondoka Makanya nilipofaulu Kidato cha nne.

Makanya ndio kwetu, Makanya ndio watu wangu, nami ni mtoto wao.

Hayo unayosema yapo Kwa kiasi,

Makanya Ushirikina na Uchawi upo na unaathari labda Kwa wageni wasio wazawa.

Makanya inamchanganyiko wa Makabila kutokana na kilimo cha zao la Mkonge.

Wenyeji wengi ni Wapare,
Lakini pia kuna
Wamasai, wasambaa, Wachaga kidogo, Warundi, Wanyambo, Wasukuma, NK.

Pia wapo wanyiramba.

Uchawi Kwa kiasi kikubwa unapatikana Milimani ambapo ipo Mashariki mwa kamji Ka Makanya.

Wasambaa na watu wa Tanga wameongeza nafasi ya UCHAWI katika mji huo wenye ukame.

Makanya ndio Makao makuu ya Biashara ya Mirungi Afrika Mashariki.

Mirungi hiyo itokayo Milimani hasa Tae, Suji, Parane na Chime ina ladha inayopendwa na watumiaji ukilinganisha na Mirungi ya Kenya na Somalia.

Uchawi pia unaisaidia Biashara hiyo ya Mirungi kuendelea kuexist mbali na Rushwa.

Polisi Wanoko wasiotaka Rushwa hukipata cha mtema kuni wakifuatilia Wauza Mirungi huko Milimani.
Hivyo hujikuta wanapata madhara na kuamua kuacha au huamishwa kabisa kituo cha kazi.

Kipindi nakua, baadhi ya ajali za barabarani zilihusishwa na Uchawi na Ushirikina.

Makanya pia ni moja ya miji iliyojaliwa Madini ya Mawe ya Nasi(Gypsum stone) ambapo hutumika kutengeneza Saruji(Cement).
Ipo dhana katika mji huo kuwa Migodi ya Jasi inaathiri unyeshaji wa Mvua.
Watu wa Makanya kipindi nakua waliamini kuwa Mvua inahamishwa na wenye Migodi ya Mawe Jasi.

Ni kawaida Makanya Wingu Jeusi kutanda lakini upepo ukatokea na kupeperusha mawingu hayo na mvua kugoma kunyesha.

Hata hivyo, kitaaluma Tabia nchi ya Makanya na tambarare ya magharibi ya wilaya ya SAME ni SEMI-ARID DESERT.
Hivyo sifikiri uhaba wa Mvua Makanya unaotokana na uchawi na Ushirikina Bali ni tabia ya nchi ya eneo hilo

AINA ZA UCHAWI ULIOPO MAKANYA KULINGANA NA ASILI;

1. Uchawi wa Wapare wenye asili ya Milimani sio Tambarare
2. Uchawi wa kisambaa
3. Uchawi wa kizigua na Kibondei
4. uchawi wa Kimasai unaotokea magharibi ya Mji wa Makanya ambapo kuna Mji wa Ruvu.
5. Uchawi wa Kirundi kutokana na Wakazi wa Makanya wenye Asili ya Burundi ambao wengi walikuja kufanya vibarua kwenye mashanba ya Mkonge

6. Uchawi wa Wanyambo na Wasukuma. Hawa pia walikuja Kama vibarua vya Mkonge.

7. Uchawi chotara
Ambao kutokana na mchanganyiko wa Makabila Makanya kuna uchawi chotara.
Wachimba Jasi wanaotaka Maeneo mengine ya Tanzania wamechangia kiasi katika uchawi huu.

Msamiati Kama Zongo ni moja ya maneno ya kawaida Makanya.

Kuvunja Jungu, n.k
Makanya na Hedaru ni moja ya miji Maarufu wilayani Same na pia inaongoza Kwa ujanja ujanja.

Sisi Wana Makanya tunapendana mno,
Kumbe wewe ni shemeji yangu. Jiko nimeopoa Makanya kwa mzee Z (RIP)
 
Huwa nacheka sana baadhi ya watu wakipinga kwa nguvu zote kuwa hakuna uchawi. Hawa hawajatembea wakajionea kwa macho yao na kushuhudia live kabisa, SIO KUSIMULIWA.

Last week kuna picha ilitrend mitandaoni ikionesha gari la Landcruiser pickup likiwa limekita pua juu ya paa la nyumba ya udongo na kudumbukia ndani. Achana na ubora na uimara wa nyumba ambayo pamoja na kuathirika kwenye paa lake lakini kuta zimebaki salama licha ya kuangukiwa na gari lenye uzito wa tani hivi.

Baada ya picha ile kuzagaa mitandaoni kuna wanahabari walichukua muda kwenda kupata ukweli na uhalisia wa tukio zima na wakatuletea na video! Katika video husika mashuhuda wakalihusisha tukio zima na imani za kishirikina! Mwenye gari kampuni ya minara ya Arusha kaingia mitini na kulitelekeza gari lake ambalo liliserereka lenyewe likapata support ya waya za umeme na kwenda kuishia kujikita kwenye nyumba husika. Hakukuwa na vifo wala majeruhi licha ya kwamba wakati wa tukio kuna mtoto alikuwa kalala ndani.

Mimi nilikuwa mitaa ya huko mwanzoni mwa mwaka huu. Nilienda kwenye mishe zangu personal. Nilienda Milima ya kati ya Hedaru na Same eneo linaitwa makanya Kijiji cha TAE. Kwa hakika kule niliukuta ushirikina katika uhalisia wake.

Kule mahakama ya haki ni ushirikina hakuna dhuluma, hakuna wizi, hakuna kugeukana hakuna kusalitiana. Ukizingua kwenye hayo moto utakuwakia. Kule ni heshima, adabu, ukweli na uaminifu.

Wizi wa bodabida ni tatizo kubwa Tanzania lakini sio Makanya wala Tae. Wakati naelekea Tae tukapita mahali porini kuna bodaboda imeegeshwa kwenye mti nikaambiwa ina wiki mbili hapo na mwenyewe alitoa tu taarifa kwa ndugu zake kuwa ilimuishia mafuta. Akaiacha hapo akauchapa mpaka Makanya akaenda zake aendako.

Safari yangu ya Tae ilinikutanisha na mambo ya ajabu lakini mengine ya kutisha. Kwa kifupi Tae kunaogopeka kati ya vijiji vyote vya kule. Tae mpaka leo hakuna usafiri wa Jumuiya kwenda na kurudi Makanya licha ya kwamba kuna umbali wa kama Kilometers 20 hivi huko ni boda au kuuchapa na ni kupanda ama kushuka milima na vilima.

Magari yaendayo Tae ni kwa ajili ya waendao kwa waganga wa kienyeji, misiba, shughuli za kiserikali na miradi.

Tae kuna vilinge maarufu vya kuua, kuharibu, kutengenezwa mambo yako. Na wakuu wake hawaingiliani bali wanashirikiana. Nikiwa kule nilishuhudia nyumba zilizoachwa na wahanga wa usaliti kwenye siasa.

Wahanga wa usaliti kwenye biashara (mirungi, bhangi na gongo)
Wahanga wa wizi mbalimbali
Wajuaji nknk
Nilikaa Tae siku tatu tuu lakini niliyoyaona kule yanafaa kuandikiwa kitabu kizima!

Tukirudi kwenye ajali husika tujihoji haya. Kwanini mmiliki kaamua kuitelekeza gari yake ya mamilioni pale?
Je, dereva wake kakimbilia wapi?
Je, wafanyakazi wa kampuni kuna mahali waliharibu?

Bado natafuta wasaa nifike eneo la tukio. Na nikienda huko nitawaletea mrejesho.

View attachment 1828122
nimeipenda hii,ukipata muda tembelea pia sehemu inaitwa ndivamhundu ipo huko upareni ,ni eneo ambalo lina history ya pekee sana na huwa kuna miujiza mingi sana kwenye hilo eneo.
 
nimeipenda hii,ukipata muda tembelea pia sehemu inaitwa ndivamhundu ipo huko upareni ,ni eneo ambalo lina history ya pekee sana na huwa kuna miujiza mingi sana kwenye hilo eneo.
[emoji1545][emoji1752]
 
Tena Mwambie Kina Mshana wapo Wengi sana Lushoto
Wapare wapo sana Lukozi, Mtae mpaka Shume uko pia Kwekifinyu.. Pale Lukozi ziko koo hasa za kina Mbwambo, Mndeme, Mjema. Wambugu wengi ni Kwemakame, Magamba, Malibwi mpaka Mshangai
 
Wapare wachawi sana na wanaendekeza ushirikina na kurogana ptyuuuu!!
 
Huwa nacheka sana baadhi ya watu wakipinga kwa nguvu zote kuwa hakuna uchawi. Hawa hawajatembea wakajionea kwa macho yao na kushuhudia live kabisa, SIO KUSIMULIWA.

Last week kuna picha ilitrend mitandaoni ikionesha gari la Landcruiser pickup likiwa limekita pua juu ya paa la nyumba ya udongo na kudumbukia ndani. Achana na ubora na uimara wa nyumba ambayo pamoja na kuathirika kwenye paa lake lakini kuta zimebaki salama licha ya kuangukiwa na gari lenye uzito wa tani hivi.

Baada ya picha ile kuzagaa mitandaoni kuna wanahabari walichukua muda kwenda kupata ukweli na uhalisia wa tukio zima na wakatuletea na video! Katika video husika mashuhuda wakalihusisha tukio zima na imani za kishirikina! Mwenye gari kampuni ya minara ya Arusha kaingia mitini na kulitelekeza gari lake ambalo liliserereka lenyewe likapata support ya waya za umeme na kwenda kuishia kujikita kwenye nyumba husika. Hakukuwa na vifo wala majeruhi licha ya kwamba wakati wa tukio kuna mtoto alikuwa kalala ndani.

Mimi nilikuwa mitaa ya huko mwanzoni mwa mwaka huu. Nilienda kwenye mishe zangu personal. Nilienda Milima ya kati ya Hedaru na Same eneo linaitwa makanya Kijiji cha TAE. Kwa hakika kule niliukuta ushirikina katika uhalisia wake.

Kule mahakama ya haki ni ushirikina hakuna dhuluma, hakuna wizi, hakuna kugeukana hakuna kusalitiana. Ukizingua kwenye hayo moto utakuwakia. Kule ni heshima, adabu, ukweli na uaminifu.

Wizi wa bodabida ni tatizo kubwa Tanzania lakini sio Makanya wala Tae. Wakati naelekea Tae tukapita mahali porini kuna bodaboda imeegeshwa kwenye mti nikaambiwa ina wiki mbili hapo na mwenyewe alitoa tu taarifa kwa ndugu zake kuwa ilimuishia mafuta. Akaiacha hapo akauchapa mpaka Makanya akaenda zake aendako.

Safari yangu ya Tae ilinikutanisha na mambo ya ajabu lakini mengine ya kutisha. Kwa kifupi Tae kunaogopeka kati ya vijiji vyote vya kule. Tae mpaka leo hakuna usafiri wa Jumuiya kwenda na kurudi Makanya licha ya kwamba kuna umbali wa kama Kilometers 20 hivi huko ni boda au kuuchapa na ni kupanda ama kushuka milima na vilima.

Magari yaendayo Tae ni kwa ajili ya waendao kwa waganga wa kienyeji, misiba, shughuli za kiserikali na miradi.

Tae kuna vilinge maarufu vya kuua, kuharibu, kutengenezwa mambo yako. Na wakuu wake hawaingiliani bali wanashirikiana. Nikiwa kule nilishuhudia nyumba zilizoachwa na wahanga wa usaliti kwenye siasa.

Wahanga wa usaliti kwenye biashara (mirungi, bhangi na gongo)
Wahanga wa wizi mbalimbali
Wajuaji nknk
Nilikaa Tae siku tatu tuu lakini niliyoyaona kule yanafaa kuandikiwa kitabu kizima!

Tukirudi kwenye ajali husika tujihoji haya. Kwanini mmiliki kaamua kuitelekeza gari yake ya mamilioni pale?
Je, dereva wake kakimbilia wapi?
Je, wafanyakazi wa kampuni kuna mahali waliharibu?

Bado natafuta wasaa nifike eneo la tukio. Na nikienda huko nitawaletea mrejesho.

View attachment 1828122
🥺🥺🥺
 
Kiasili ni mchaga, ila nimezaliwa same, nkakulia kijiji cha MAHUU, karibu kabisa na Mlima Shengena, Primary nimesoma hapo hapo same, so nnapajua vizuri, Kuhusu Uchawi kiukweli panaogopeka sana,

Nakumbuka moments nyingi sana, sisi tulikua ni wafugaji, tulikua tunaenda kuchunga Mbuzi huko milimani, matukio ambayo sitoyasahu ni kukutana na nyoka wa kila aina, Wilaya ya same inaweza ikawa top 3 katika wilaya zenye nyoka wengi kwa hapa Tanzania
 
nimeipenda hii,ukipata muda tembelea pia sehemu inaitwa ndivamhundu ipo huko upareni ,ni eneo ambalo lina history ya pekee sana na huwa kuna miujiza mingi sana kwenye hilo eneo.
Hii ipo upareni sehemu gani?
 
Back
Top Bottom