Uchawi,Ulonzi na ndumba za Babu Tale,Salam na Fela umefanya muziki wa bongo kuwa ngumu sasa wananchi wamegoma kucheza Rhumba

Mkuuu kwani kituo kipi cha redio kinacho fanyiya promo wale wa wcb ??
 
Wenzenu wanapiga hela nyie mnakalia Uchawi Kwanini na nyie msiroge.Kuna aliyewakataza msiroge? Leo mnatafuta mchawi nani? Mkae mjue WCB wajanja wale,Subirini tu muda watakachokifanya na sembuse makiki yao yale!
 
Mkuuu kwani kituo kipi cha redio kinacho fanyiya promo wale wa wcb ??
Wasafi TV
Wasafi FM
Wasafi Media You Tube
Wasafi FM You Tube
Wasafi TV Facebook
Wasafi TV Twitter
Wasafi FM Facebook
Wasafi FM Twitter
Wasafi FM Instagram
Wasafi TV Instagram
Wasafi Fans all the worldwideweb.
 
Nikisikiliza NENDA KAMWAMBIE NA LALA SALAMA namuona diamond halisi wa mashairi Ila kiukweli huyu wa Sasa hapana nashindwa kuelewa sehemu kubwa ya maneno yake na kiuhalisia mengi hayana maana kabisa ukiacha yale matusi....
Ukiangalia nyimbo za karibuni za Wcb zimekua na maneno ya matusi Tena linganifu Rayvany na Diamond wakiongoza.

Hamonize kidogo anajitahidi Sana Ila kwa nyimbo alizoshirikishwa nje na akajaribu kingerezeza Zina ladha moja zote.....

Kwa Sasa ALIKIBA heshima inambeba Sana kuanzia maisha halisi, uimbaji na jukwaani. Namuheshimu kwa sababu mpaka Sasa anaishi muziki pamoja na mabadiliko makubwa Sana yaliyotokea ya kimuziki ambayo wengi wa umri wake hawapo Tena.

Siku psychology ya mziki ikibadilika ghafla Kuna wasanii WCB watapotea kabisaaa.
 
Hahaha kiba mnafiki Ana gubu mbahiri ...ndo mana hawezi ata aka mtoa yeyote out kwenye gemu kuna siku kaulizwa eti mbona hujapata tuzo akasema eti hazipendi na sasa hivi anaishiya ku copy kwa mondi vitu alivyotakiwa kuvianzisha mwenyew kiba anajaribu kuitembelea nyota ya daimond
 
Sasa mbaya zaidi WCB ndo huwa wanaamua muziki ubadilike au ubaki hivihivi,wanatumia njia nyingi kuwanyamazisha wasanii wengine ili wabaki wao tu wakiongelewa na wamefanikiwa kwa hilo,,ukimtoa SALLAM ambae hadeal sana hapa bongo,,WCB wakitoka tu wale wazee fitna BABUTALE NA FELA basi kazi itakuwa imeisha japo kuna vi fella vingne vinazidi kuzaliwa kama meneja momo,HIVI hakuna mtu anaweza akajitolea kupoteza wale wazee wa fitna jamani??.Maana ishakuwa shida mtaani,kila siku dabliyusibi tu..
 
Dah, hii "soft porn" kwa nini inashamiri sana siku hizi aisee maana sio hapa TZ tu bali hata international huko ni vile vile. Na kwa nini serikali inaliangalia tu badala ya kuliona kama distraction kwa watu?
 
Mtoa mada unafeli sana mambo ya zamani sana haya ebu angalia uwekezaji unaofanywa na wcb ni mkubwa kuliko wasanii wote mwaka tangu unaanza mpaka sasa msanii mmoja harmonise ana video nne tena ni za gharama
inamana wewe unachotaka mtu anayewekeza shiling laki moja apate faida sawa na alyeweka mil moja ata wewe unaweza ukasaga unga mzuri lakini hauwezi kushindan mauzo na bakhlesa
 
Umeongea mtazamo wangu.
 
Wenzenu wanapiga hela nyie mnakalia Uchawi Kwanini na nyie msiroge.Kuna aliyewakataza msiroge? Leo mnatafuta mchawi nani? Mkae mjue WCB wajanja wale,Subirini tu muda watakachokifanya na sembuse makiki yao yale!
Ao niwafa maji
 
Wasanii wengi pamoja na kutoa nyimbo nzuri lakini wengi wanakosa ubunifu kwenye kufanya promotion ya nyimbo zao kwani wanafikiri wakishatoa wimbo mzuri basi sisi mashabiki tutapokea tuu
Sasa hapo uchawi unaingiaje wakati umeshatoa jibu la kisayansi?
Kumbuka hata diamon alipambana sana
Kama uchawi unafanya kazi mshauri basi mavoko na yeye atumie
 
Ndumba znafanya Kaz hatar naona
 
Pongezi kwa Tale... kazi iliyotukuka imeonekana na kuzaa matunda.. mbuyu chali.
 
Kafara inatenda kama maagizo yanavotolewa. Mweeeeh
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…