Uchawi umedunda kwa Ally Kiba

Uchawi umedunda kwa Ally Kiba

Wivu tu unawasumbua..wakimuona wema anavyopewa zawadi ya nisan murano wakati wao wanahongwa chips kavu wanachanganyikiwa kabisa

Mnataka watu wote wawe upande wenu eeeh??
Poleni aisee Kiba ndo keshakiamsha sasa, wale mashabiki wote waliokuwa wanalazimika kushabikia watu wengine sababu ya ukimya wa Kiba ndo washaamka hivooo tena kwa kasi mpyaaaa! Mtu kama anapendwa anapendwa tuuu na kama ndomo alikuwa anamchukulia poa basi habari ndo hiyo!!

Emmm mind you....ndomo mkali wa shooting tu lakini mapini ya ukweli hanaaaa ukatae ukubali ....hiyo kitorondo yenu ukiilinganisha na SIKUONI ya Ally K haiingii hata robo....ushafahamu?? Na ndo nyimbo ya longiii Vocally ndo usiseme kabisaa
 
miss strong una mahaba hadi shetani anayaogopa! Binafsi sina husuda kwa Ali K wala Diamond lakini namkubali zaidi Diamond kutokana na anavyojituma as compared na Ali K! miss strong, tuache ushabiki pembeni... hivi nini cha maana alichofanya Ali K kwenye ile show hadi tushawishike kwamba alimkalisha Diamond? Pili, mie nimeshahudhuria show za Diamond lakini lazima nikiri jana hakufanya vizuri na wala haioneshi kwamba alikusudia kufanya vizuri yeye ni shost ake Davido! Pamoja na yote hayo, zungumza na nafsi yako hata usipotoa jibu hapa... hivi kweli unaamini kabisa ile show sub standard ya Diamond ilikuwa mbaya maradufu kulinganisha na show ya Kiba?

Mkuu wadau wanaleta ushabiki wa Simba na Yanga kwenye muziki.
 
Hii inadhihirisha Watz tulivyo na roho mbaya sana. Mtu au sijui kikundi au sijui taasisi wanakodi watu just wamzomee Diamond! Hawa watu waliofanya kitendo hichi hawana tofauti na kikundi cha al-shabab cha Somalia. Diamond, hasife moyo hata kidogo, wapenda maendeleo wako nyuma yako.
Acha siasa wewe Babu Tale mapovu yamemtoka eti watu wamekodiwa.Wale ndio mashabiki anazomewa Jay Z hasemi watu wamekodiwa ndio iwe Diamondi hebu tumia akili zako acha kutumia za kushikiwa wewe.
 
Kilele cha fiesta siku ya jana tarehe 18 octoba 2014 Tanzania na dunia nzima kwa ujumla imeshuhudia msanii Ally Kiba akioyesha kuwa uchawi hauna nafasi kabisa kwenye muziki baada ya kumkalisha Diamond ambaye siku chache zilizopita alijinadi kupitia Clouds fm kuwa yupo tayari kumsaidia Ally Kiba kufanya nae collabo na sasa kibao kimemgeukia yeye ndiye atakayesaidiwa kufanya collabo.

MASHABIKI: Mashabiki walikuwa hawataki kusikia lolote zaidi ya Ally Kiba. Mashabiki wengine walienda mbali zaidi na kusema bora wasimuone T.I wao wanamtaka Ally Kiba tu.

DIAMOND AZOMEWA KAMA MBWA: kila akiimba mashabiki kila kona ya uwanja walikuwa wakimzomea Diamond huku wakitaka Ally Kiba arudi stejini. Mashabiki wasikika wakisema ''kiba kiba kiba kiba kiba'' huku wakimzomea Diamod ''buuuh buuuh buuuh''

Diamond apata wakati mgumu, Davido na Ney wa Mitego watumika kumbeba Diamond lakini mashabiki hawakuacha kumzomea.

DIAMOND ATAFUTA MCHAWI WAKE: Diamond huku akitapa tapa anahisi amechezewa mchezo na Clouds fm au Ally Kiba eti kwa kile anachokiita mafanikio yake, mashabiki wamjibu ''nani akuchukie wewe? kwa mafanikio yapi? kubadilisha wanawake au kutokumaliza nyumba? kama tunachukia mtu mwenye mafanikio wa kwanza angekuwa Mengi na Bakhresa sio mtu ka wewe''
Alizomewa Kikwete mwaka 2012 pamoja na Yoweri Museven chuo kikuu cha dar es salaam, who is Diamond bwana?

Msanii huyo aliyekulia Tandale na kufanya biashara ya kuuza mitumba na voucher, siku kadhaa zilizopita alinukuliwa na vyombo vya habari kuwa Jiji la Mbeya halina hotel inayoendana na hadhi yake, baadhi ya mashabiki kutoka Mbeya pia waahidi kumzomea siku akienda Mbeya kwani kumuacha ni kumuendekeza ipo siku atasema hajaona hotel ya kulala Tanzania nzima/hajaona chakula cha kula Tanzania na hatimae atasema watanzania wote sio level yake.

Ukweli ni kwamba Diamond kwasasa hapendwi nchini Tanzania, si kwamba ni msanii mbaya ila sababu kubwa ni dharau zake na kiburi. Hivyo aashauriwa aache kusingizia watu. ''Waliomzomea ni watu waliotoka kwao na wakalipa pesa zao''
Mjadala upo wazi kwa wanaobisha na kujiita #TeamDomo
 
Hii post ilishawekwa humu we umeamua kucopy na kupaste ee?
 
Wangempigia vuvuzela puuuuuu ! Shuka stejiniiiiiiii
 
Back
Top Bottom