'Uchawi' wa biashara ni 'location' tuu kwisha!

The Eric

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2019
Posts
6,446
Reaction score
10,976
Kwema!

Sitemi cheche nyingi wala, ukiachilia mbali vigezo vingine vya kufanya biashara kama bidhaa nzuri, customer care etc, ila uchawi nambari one ni LOCATION Pekee. (Physics inasema Location matters provided other variable factors remain constant) πŸ‘ˆπŸ‘ˆπŸ‘ˆ Hiyo ndiyo Business Law.

Huwa nashangaa watu wanafungua duka la nguo huko porini yaani mbalii ambapo daah.

Hata hapa Dar es Salaam unakuta dukani mtu akikaa mpaka analala, hii ni kwa baadhi ya vichochoro. tunasemaga duka lipo kushoto.

Cc CONTROLA nisiingilie kazi yake.
 
Kuna ofisi ziko Mahala pabaya ila zinaacha kumbukumbu kwa mteja kulingana na kile mteja anapokea toka kwa huduma zao.
Je unaacha Hisia gani kwa mteja ? Kuanzia price elasticity
Reaction, Response na Reward hapa ndipo ulipo uchawi.
 
Biashara ni (mipango) strategy

Watu wanafungua chaka ni chaka, wengine hawana hata fremu lakini wanauza.
 
Naunga mkono hoja lakini Bei ya bidhaa yako ina nguvu kubwa sana katika biashara

Tunasema upate faida ya elfu moja ya pamoja halafu mteja asirudi au upate faida ya shilingi mia moja lakini iwe ya kudumu muda mrefu? Kampuni hiyo hutumiwa na wahindi, wachina na kwa Tanzania mabingwa wa faida kidogo mzunguko mkubwa ni wakinga, waha, na wafanyabiashara wa Katoro geita,
 
Location ina nguvu nakuunga mkono kwani ndio huamua hatma ya biashara yako, kipindi cha mvua ifakara utauza gunboot zenye rangi za jeshi jeshi, miavuli, naloni, madawa ya kilimo lakini ukienda ifakara kwenye mavuno utauza magunia, kamba, turubai, sindano za kushonea magunia maana yake eneo moja limeamua biashara mbili tofauti ndani ya mwaka mmoja,
 
Acha ujinga wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…