Uchawi wa Yanga huu hapa mambo hadharani.!

Uchawi wa Yanga huu hapa mambo hadharani.!

Notorious thug

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2021
Posts
2,817
Reaction score
10,667

Naaam heri ya sikukuu za Krismasi na Maandalizi ya Mwaka Mpya 2023. Achana na mambo ya kulilia jezi nyeusi leo nakupa uchawi wa Yanga walioufanya kwa takribani mwaka mmoja Uchawi namba moja. AZIZ K -baada ya kuisumbua Simba walipokutana na Asec Mimosas Yanga wakavutiwa na Winga huyu mwenye Makeke mengi uwanjani haraka haraka akasinya mkataba na kuingia mzigoni Simba walitakiwa kumpata mchezaji huyu kutokana na mara zote mbili walizokutana nae uwanjani aliwalaza na viatu ila kutokana na kua watu hovyo wa kusajili wachezaji wakamsajili Nelson Okwa ambaye hajaonesha kiwango hadi kuelekea mechi na Kmc haonekani kwenye kikosi cha kwanza,benchi wala Jukwaani. Ubora wa kikosi-Achana na siasa zungumzia mpira tuchukulie kikosi cha Yanga Vs Simba pale Simba kuna wachezaji kama Chama(mchezaji bora kwenye ligi yetu) Moses Phiri na Henock Inonga pekee ndio wanaweza kukalisha wachezaji wa Yanga benchi Mohammed Hussein kiwango kimekua sio kizuri labda kutokana na kucheza michezo mingi. Kucheza kitimu- Hapa mtoe huyu jamaa wa Kongo anayependa kukimbia kama hana kichwa ndio mchoyo ila kwa wengine wanacheza kitimu na kusahau ubinafsi tofauti na timu kama Simba wachezaji kama Pape Osman Sakho na Okrah ni wabinafsi sana fikiria wangecheza kama Chama Simba ingekua wapi.

 
Hata kocha wa Simba Hana frist eleven Nadhani anapangiwa na viongozi.
FB_IMG_1672053762269.jpg
 
Back
Top Bottom