special_one
New Member
- Jun 3, 2023
- 1
- 0
UCHECHEMUZI WA SERA KWA MAENDELEO ENDELEVU NA UTHABITI WA UTAWALA BORA
Tanzania tangu uhuru na muungano kuna maeneo mengi hatujayafikia ili kufikia Maendeleo endelevu kwenye viwango vya kiuchumi hata Kama tulipo tangazwa katika awamu ya tano na Bank ya Afrika kuwa tumeingia uchumi wa Kati. Na hii kimsingi inatokana na ukweli uliopo wa kiutawala na mfumo wa maamuzi kwa maslahi mapana ya Taifa.
Kwa Mtazamo wangu kama Kijana nimeona na kupekua majarida kadhaa utawala bora Ndio ufunguo wa Maendeleo Taifa lolote lile ulimwenguni, na hii ni kiwa na maana gani ndugu zetu baadhi wanao pata nafasi ya kututumikia wengi wanashindwa kuzitafsiri sera zetu za Maendeleo kama Taifa zaidi wanasukumwa na mihemko ya kiutendaji na kimaamuzi kwa dhumuni la kumridhisha aliyepo juu kimamlaka na aliyepo juu pia asipokuwa na busara ndio mwanzo wa uozo wa rushwa chafu na unyonyaji kwa mali ya umma.
Na hili suala kwa jinsi lilivyo Tanzania tunahitaji uelewa wa kutosha kuhusu sera zetu za Taifa tulizo nazo. Na uelewa ufanyike kwa makundi yote kuanzia vijana, wanawake na viongozi kwa ngazi zote.
Hii ikiwa ina maana kuwa kila mtu atakuwa na uelewa wa dhana ya uwajibikaji na kutambua majukumu yake kwa nafasi aliyepo kuliko Kama ilivo sasa mtu anaamini kuwa nafasi aliyepo yeyote anamsaidia raisi na sio watanzania na hii inatokana na ukweli watu wanashindwa tafsiri sera za Maendeleo za Taifa. Na hata Taifa halijaweka mkazo wa uelewa wa sera kwa mfano wakati huu kuna mchakato wa utoaji maoni ya Dira ya Maendeleo ya Taifa ambapo miongozo ya na vipaumbele vya kimaendeleo vitatafsiriwa kwenye dira hiyo kwa miaka 25 ijayo lakini hakuna msukumo au hamasa hata nguvu inayotumika wa ukusanyaji maoni kwa watanzania nchini Kama tunavopigiwa kelele na suala la uchaguzi ambalo muda wake bado haujawadia na pesa zimetengwa kabisa. Ila hao wanaopigia chapuo uchaguzi wanasahau kuwa dira ndio egemeo la kuombea kura kwa watanzania na kubaki kama kielelezo cha malengo kufikiwa.
Maoni yangu hili daftari la wapiga kura linapoenda kuhuisha takwimu zao mawakala wapeleke na ujumbe wa Dira ya Maendeleo ya Taifa maana wanaenda kukutana na 75% ya makundi ya Watanzania wenye umri kuanzia miaka 18.
Na pindi watanzania watakapo pata uelewa wa nguvu ya sera kwa Taifa ni rahisi kuleta uwajibikaji kwa kila raia na viongozi wetu. Hasa kwa sisi vijana inauma unakuta mtu hajui kitu kiletacho chachu ya Maendeleo katika maeneo yake anayoishi na hashiriki kwenye eneo lolote la kimaamuzi hata kwenye vikao vya serikali ya Mitaa na kijiji hana mpango akiamini siyo jukumu lake na wala wajibu wake ivo ni ngumu mtu wa ivo kuleta uwajibikaji labda tupeke umuhimu wa sera na Maendeleo pamoja na utawala bora kwa wa Tanzania.
Ninayo maumivu ya kizalendo kwa viongozi kwenye dhana ya utawala bora hasa kwenye sekta za wizara, kwa wadhifa wa Katibu Mkuu wa wizara husika kuletwa kisiasa na Tena kufanya utendaji kisiasa na sio kwa msingi wa kutafsiri sera ya wizara na kusimamia miiko ya na desturi ya wizara husika na kumpa miongozo Waziri aliyepo Kama yeye ndio Mtendaji mkuu na kukataa kabisa mihemko ya siasa ili kuleta muunganiko wa serikali kuu na wananchi.

Upvote
0