A
Anonymous
Guest
Kuna changamoto katika Nanyumbu District Council inayohusu ucheleweshaji wa malipo ya gharama za uhamisho kwa watumishi, hususan walimu wa sekondari. Hali hii imekuwa ikileta usumbufu mkubwa kwa wahusika kutokana na mazingira ya kazi na maisha wanayokutana nayo baada ya kuhamishwa.
Uhamisho ulifanyika tarehe 21 Desemba 2023 kwa baadhi ya walimu waliopangiwa shule za Rukumbi Secondary School na Mkapa Girls Secondary School, ambazo ni shule mpya zilizoanza mwaka 2024. Hata hivyo, hadi sasa mwaka 2026, walimu hao hawajalipwa kikamilifu stahiki zao, ikiwemo disturbance allowance, achilia mbali posho nyingine za uhamisho.
Pamoja na kwamba Halmashauri ina vyanzo vya mapato ya ndani vinavyoongezeka kila mwaka pamoja na fedha za uhamisho kutoka serikali kuu, bado sababu za kuchelewa kwa malipo hayo hazijawekwa wazi. Tunaomba mamlaka husika zifuatilie suala hili na kuhakikisha haki za watumishi hao zinatendeka kwa wakati.