Mfumo wa usikilizaji wa kesi na kutoa hukumu mahakamani una walakini kwani kesi ambazo upelelezi umekamilika na kusikilizwa bado hazitolewi hukumu katika muda mwafaka. Nina mfano mmoja wa jamaa aliyetapeliwa kwa kutoa pesa ya kununulia kontena mwaka 2006. Mshtakiwa alimpeleka kwa mwenye kontena wakalikagua wakakubaliana bei. Wakaenda serikali ya mtaa kulipa. Mshtakiwa akatia saini upande wa shahidi wa jamaa hela ikalipwa wakakubaliana mzigo uchukuliwe ndani ya siku tatu. Baada ya siku tatu jamaa kaenda na lori na mshtakiwa wakakuta kontena halipo na mwenye nalo amehama (hayupo ktk maeneo yale). Kwenda serikali za mtaa nao wakashangaa! Mnunuaji akabaki kumbana aliyempeleka.
Jamaa kaenda kumshtaki yule agent akatoa na vielelezo. Agent akakamatwa akasomewa shtaka upelezi ukaanza. Kesi ikasikilzwa ikabakia kutolewa hukumu. Kila jamaa akienda mahakamani kesi inaahirishwa. 2006,2007,2008, 2009, 2010 hadi 2011. Hakimu aliyesikiliza kesi kahamishwa kaja wa pli kaja wa tatu kaja wa nne. Cha ajabu hakimu wa mwisho katoa hukumu kwa kusema kwamba mshtakiwa hana hatia kwani kwenye faili hakuna vielelezo vinavyoonesha kuhusika kwake katika biashara ile.
Kinachokera hapa wala sio hiyo hukumu ila ni ule muda wa nenda kesi inaahirishwa nenda kesi inaahirishwa. Hivi ingekuwa ni daktari anayetibu mgonjwa au injinia anayejenga daraja hali ingekuwaje? Mahakimu pamoja na mazingira magumu ya kazi lakini nawaombeni mjitahidi hasa kwa kesi ambazo hazina utata ktk upelelezi hukumu zitolewe mapema.