KERO Ucheleweshwaji wa ujenzi na maboresho ya masoko ya Majengo, Kizota na Stendi Ndogo ya Mnada Mpya

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Wana bodi, kumekucha, tunamshukuru Mungu kwa kutujaalia uzima.

Naomba kuwasilisha kero kuhusu ucheleweshwaji wa ujenzi na maboresho ya masoko ya Majengo, Kizota na Stendi Ndogo ya Mnada Mpya. Tunaomba kufahamu miradi hii itakamilika lini.

Tunaiomba Serikali, pamoja na viongozi na wasimamizi wa miradi hii, hususan Waziri wa Biashara, watukumbuke sisi wafanyabiashara wa maeneo haya. Imepita zaidi ya mwaka mmoja na miezi mitatu huku baadhi ya miradi ikiwa imesimama bila maendeleo ya kuridhisha.

Hali hii imeathiri shughuli zetu za biashara na maisha yetu kwa ujumla, ilhali tuna familia zinazotutegemea na majukumu ya kila siku ya kuyatekeleza.

Tunaiomba Serikali kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi hii ili ikamilike haraka, turejee kwenye biashara zetu na kuendelea kujipatia kipato. Tunaomba sana mzingatie kilio chetu kama wananchi na wapiga kura wenu.

Asanteni.
 
Hapo Hakuna Lolote Miaka Inakwenda Viongozi Wapo Hawajitambui
Aibu Utaona Wewe.......
 
WE mgogo nini?
Hbari inaninginia, majengo ipo nchi nzima, kizota na mndani kila mkoa zipo, wewe unazungumzia mkoa gani?
 
Back
Top Bottom