KERO Ucheleweshwaji wa utoaji wa majibu ya rufaa za Utumishi Ikulu

KERO Ucheleweshwaji wa utoaji wa majibu ya rufaa za Utumishi Ikulu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Habari za kazi?

Sisi ni wahanga wa manyanyaso katika utumishi wa umma, na tumekata rufaa katika Ofisi ya Rais, Ikulu, tukitafuta haki zetu za ajira. Hata hivyo, mchakato wa kushughulikia rufaa zetu unaendelea kwa kasi ndogo, huku muda ukizidi kwenda bila kupata majibu.

Hadi sasa, hatujapokea majibu wala taarifa yoyote kutoka Ikulu kuhusu hatima ya rufaa zetu. Hali hii inazidi kutuweka katika mazingira magumu, kwani sisi pia tuna familia na majukumu ya kutekeleza kama watu wengine.

Tunaomba utusaidie kufikisha kilio chetu kwa mamlaka husika ili mchakato huu uharakishwe na haki yetu ipatikane. Tunatamani kurejea kazini ili tuweze kuendesha maisha yetu, kuwasaidia wazazi wetu na kutunza familia zetu.

Tunaomba sauti zetu zisikike na haki itendeke. Asante kwa kutupa nafasi ya kufikisha kilio chetu.
 
Back
Top Bottom