Uchifu sasa unatambulika rasmi kama sehemu ya uongozi Kiserikali?

Uchifu sasa unatambulika rasmi kama sehemu ya uongozi Kiserikali?

Tulimumu

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2013
Posts
14,409
Reaction score
13,262
Uongozi wa kikabila na kimila wa kichifu ulifutwa enzi za baba wa taifa mwl Nyerere.

Zimepita awamu nne hatujaona marais wakijangaika na machifu na uchifu. Lakini katika sehemu ya mwisho ya awamu ta tano ambayo inaendeshwa na Rais aliyerithi baada ya aliyechaguliwa kufariki naona kumeanza kampeni na juhudi kubwa za kuutambua na kuurasimisha uchifu kama sehemu ya uongozi wa nchi hii na ametamka kuwa Serikali yake itashirikiana na machifu kana kwamba ni viongozi wanaotambulika kikatiba katika nchi hii.

Kuna nini kwenye hii U turn?
 
Lakini katika sehemu ya mwisho ya awamu ta tano ambayo inaendeshwa na rais aliyerithi
Hii ni awamu ya 6, na siyo sehemu ya mwisho ya awamu ya tano.

Samia hajarithi kiti amechaguliwa na matakwa na nguvu ya kikatiba.

Kinachorithiwa ni mamlaka ya kifalme/kimalkia ama kichifu.
 
Hakika hii ni sehemu ya pili ya awamu ya tano!. Tutarukaruka lakini ukweli utabaki kuwa ukweli.

Ni kama ng'ombe alishaliwa, Samia kabakishiwa mkia amalizie. Sera na mambo yote ya kipande hiki cha awamu ya tano yalishakamilika na kuwekewa misingi. HAKUNA JIPYA, BALI KUPAKA RANGI KIDOGO HAPA NA PALE, LAKINI NI SURA ILEILE.

Usiangalie awamu kwa porojo za wanasiasa. Angalia yanayotendeka. Kama siyo ujenzi wa SGR, manunuzi ya ndege, kuhamia dodoma, na kuminya demokrasia ni lipi jipya?

Hii ni awamu ya 6, na siyo sehemu ya mwisho ya awamu ya tano.

Samia hajarithi kiti amechaguliwa na matakwa na nguvu ya kikatiba.

Kinachorithiwa ni mamlaka ya kifalme/kimalkia ama kichifu.
 
Bwa mdogo Bwashee
Uchifu ulifutwa na mtoto wa chifu Burito wa Uzanaki aitwaye Julius Nyerere na machifu wenye nguvu Kama Fundikira na Humbi Ziota wakapewa uwaziri
Acha kujifanya unajua kila kitu kumbe mweupeeee
Zile ni siasa tu, uchifu haujawahi kufutwa!

Labda kama wewe hujatokea ukoo wa kichifu.
 
Uchifu mbona upo ila sio wa ki madaraka kama unavo sema. Ni watu na mila zao. Hata ukiwa na hela wenzako bar wata kupa uchief
 
Naona wanaendelea kujikita kwenye ushirikina, hili taifa spiritually limekabidhiwa kimaagano kwa ibilisi........ndo maana wanamfanyia ibada kwa kukimbiza moto kila mwaka......
 
Wanalazimisha tu ni awamu ya tano. Awaamu hubadilika kwa uchaguzi yeye karirhi anaendeleza awamu ya tano siyo ya sita
Hii ni awamu ya 6, na siyo sehemu ya mwisho ya awamu ya tano.

Samia hajarithi kiti amechaguliwa na matakwa na nguvu ya kikatiba.

Kinachorithiwa ni mamlaka ya kifalme/kimalkia ama kichifu.
 
Wanalazimisha tu ni awamu ya tano. Awaamu hubadilika kwa uchaguzi yeye karirhi anaendeleza awamu ya tano siyo ya sita
Awamu ni mtu siyo mihula ya uchaguzi. Ndiyo maana Zanzibar wako awamu ya 8
 
Anaogopwa kupigwa kipapai na walozi.... Ndio maana anakimbilia sana huko...
Wenzake walifanya ila ilikuwa siri sana.... Yeye anafanya waziwazi.....

Tumuache tu aendelee labda yatakuwa na faida siku za usoni.
 
Back
Top Bottom