Rusumo one
JF-Expert Member
- Oct 4, 2018
- 3,458
- 4,283
Habari za usiku wakuu na wote humu. Nijikite kwenye mada juu.
Katika mihangaiko yangu nipo eneo la Kata ya Galigali Kijiji cha Matonya na pia Kuna mida nakuwa Kitongoji cha Idete hapa baridi kali Sana huku nikiendelea kusaka maharage kwaajili ya biashara. Nachosikitika ni kuona madini yakichimbwa Hadi kwenye vyanzo vya mito na kelele zilizopo ni kwamba hata EIA haijafanyika, wananchi waliletewa wachimbaji na kutambulishwa na afisa madini wakiwa na afisa mazingira Wilaya ya Mpwapwa.
Niseme tu hii haipo sawa uharibifu mkubwa unafanyika isitoshe hawa watu inasemekana hawana hata vibali vya uchimbaji ni uhuni tu. Hivi huku hakuna mbunge? Simbachawene anakula posho anasahau wananchi wake Ila ingekuwa mwakani kipindi Kama hichi angeshafika, WEO,VEO na vitongoji wamelala. Taarifa zilizopo ni kuwa hata vyombo vya uchunguzi TISS,PCCB na PT wana taarifa Ila wamekalia kimya.
Napaza sauti Serikali kupitia wizara ya Madini iingilie kati suala hili makamu waziri mkuu fika huku ujionee mambo na watu wa mazingira mkuje.Kila usiku land cruiser zinazama na kubeba madini pia malori yanabeba madini usiku kwa usiku wakati Vijiji haviingizi kitu. Karibuni Matonya,Idete,Kinusi,Mbuga,Ipera.Mng'ang'a,Kikuyu mjionee fahari ya wahehe.
Nawasilisha.
Kamweneee!!!