Uchimbaji wa maduka ya chini kwa ajili ya kuongeza sehemu ya maduka unatajwa kuwa chanzo cha kuporomoka kwa jengo kariakoo

Yaan wanachimba maduka jengo ambalo liko tayari ama inakuaje?
Ndio uone akili za watanzania zilivyolala. Jengo limeshajengwa kwa viwango vya kuishi binadamu wao wanageuza vyumba vya gorofa maghala ya kutjnzia bidhaa, flows za gorofa zimejengwa kwa kufuata stability ya foundation wabongo wanabomoa foundation kuongeza flow nyingine😄
 
Wanataka maghorofa yaelee kama kwenye ndoto za Abuu Nuwas kujenga nyumba angani.
 
Imagine ni magorofa mangapi wameshafanya huo mchezo wa kuchimba chini bila utaalam kuhusika. Lazima jengine lishuke after 5 years. Inaonyesha huyo aliefanya hivo ameiga kutoka kwa wengine waliokwishafanya hivo kisiri! Ngoja tuone jengine lishuke sasa huku serikali ya ccm ikiangalia tu.
 
Yaan wanachimba maduka jengo ambalo liko tayari ama inakuaje?
Shortcut is always a wrong cut.
Ni upumbavu usiomithilika😂 yani mtu ana disturb msingi wa jengo tena chakavu. Approach iliotakiwa ni kuvunja na kujenga upya foundation yenye underground shops, yeye akaamua kutoboa baadhi ya maeneo ya msingi yenye kuta ili aache zile sehemu rigid zenye nguzo bila kujua hata ukuta umechangia support ya kubeba flow za juu.

Mmiliki wa jengo anatakiwa aende jela straight away na kuwajibika na hasara alizowatia wahanga.
 
Sasa hivi itabidi tuache kwenda chini kwenye zile basement
Ukiwa Trapped kule you are as good as dead maana huwa hewa hamna kabisa na una feel ile struggle ya kuvuta hewa nzito yenye joto kali na harufu za majasho.

Jiulize kifusi kikiziba kabisa zile exits hali itakuwaje kama sio kufa kwa mateso.
 
Exactly, mimi kama kiongozi lazma ningetafuta kumjua mmiliki na straight away angepandishwa kizimbani. Sadly kwa utawala huu he will get away with it ila kwa kile chuma JPM alikuwa anakula mvua za kutosha.

Tamaa za kipuuzie kabisa hizo.
 
Ukiwa Trapped kule you are as good as dead maana huwa hewa hamna kabisa na una feel ile struggle ya kuvuta hewa nzito yenye joto kali na harufu za majasho.

Jiulize kifusi kikiziba kabisa zile exits hali itakuwaje kama sio kufa kwa mateso.
Terrible. Inatakiwa kuwa na mamlake zenye akili.
Ilibidi hata kuomba vikosi vya uokoaji nje ya nchi.
 
Hii mbona Kali mzee?
Inamaana wanachokonoa foundation ya jengo wapate space ya kuweka fremu huko chini mbona hainiingii akilini asee.
Hao mafundi waliokuwa wanafanya hiyo kazi hawakuwa na Akili au?
Nijuavyo hizo underground floor zinawekwa baada ya jengo zima kubomolewa na kujengwa kwa site plan mpya.
 
Wanapenda mambo ya kufosi sema nashukuru hio kadhia ilimfika mwanae🤣 ili ausikie uchungu wake
 
UPIGAJI.
Ratio ya zege mfuko moja wa cement,ndio 4 za kokoto ,ndio 3 za mchanaa,.
Hii ratio ndio kwanza naisikia kwako toka dunia imeumbwa! Na mbaya zaidi utakuta na wewe unajiita injinia tena unasimamia site kabisa! Mwisho wa siku unakuja kuua watu
 
Inaonesha wananchi wana taarifa ila wenye nafasi ya kutumia taarifa hizo hawana taarifa au wanapuuzia tu taarifa.
Ila tamaa ya fedha kwa wamiliki wa majengo, wafanyabiashara, mainjinia na watoa vibali karma haitowaacha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…