Uchimbaji wa maduka ya chini kwa ajili ya kuongeza sehemu ya maduka unatajwa kuwa chanzo cha kuporomoka kwa jengo kariakoo

Exactly, hio ndio namna sahihi ya kufanya. Mafundi walikuwa njaa na boss ambaye ndiye mmiliki nae akili kisoda. Utakuta alishauriwa na Engineer vizuri akam bypass na kutafta mafundi yeye.Hapo kuna tajiri mwenzie alifanya huo upumbavu uka work out so akamjaza ujinga ili nayeye afanye upuuzi wa aina hio sadly amefeli na ameumiza watu.
 
Shida ni kukosa utalaamu na ujanjaujanja mwingi wala sio kuchimba hizo underground
Shida sio kuchimba underground unasema? Wewe leo hii toa bati lako kisha mwaga zege juu then pandisha ukuta ili uwe na nyumba ya ghorofa halafu uone kama hilo jengo hamna siku litapasuka nyufa kama si kuwaua kabisa wanao.
 
Fundi njaa
 
Kiongozi kwa hiyo michezo itakuwa ni maafa makubwa kwa nchi pindi likitokea tetemeko dogo tu mijengo mingi itaporomoka, siombei hilo ila ndio hivyo CRB na wengineo wamelala wa pono.
 
Hakuna ukaguzi wa majengo?
 
Wata
alam ujenzi/wahandisi watueleze kitaalmu ni kwa % ngap hii inaweza sababisha jengo kuporomoka!?,na kama ni hatari je serikali haikulijua hilo na wametoboa majengo mangap mpaka sasa!?
Usisikilize Hizo porojo mkuu, Huwezi ukachimba chini ya ghorofa, Haiwezekani hata siku 1..
 
Hii ratio ndio kwanza naisikia kwako toka dunia imeumbwa! Na mbaya zaidi utakuta na wewe unajiita injinia tena unasimamia site kabisa! Mwisho wa siku unakuja kuua watu
Alafu nenda kaangalie kwenye Lile gorofa kwenye collum wametumia nondo za mm ngapi?.ukikuta mm18 au 20.rudi nikutumie elfu 50.
 
Hii ratio ndio kwanza naisikia kwako toka dunia imeumbwa! Na mbaya zaidi utakuta na wewe unajiita injinia tena unasimamia site kabisa! Mwisho wa siku unakuja kuua watu
Kina fundi maiko hao!!!
Sie tuliopitia Technical school tunajua kabisa standard concrete mix ni 1:2:3 na High strength concrete ratio ni 1:2:2
 
Huwa sipendi kwenda kariakoo maana usalama ni mdogo pale. Kwanza umeme ukikatika kila mtu ana kijenereta chake siku vikilipuka ni kilio kingine. Halafu hizo ghorofa zina mizigo juu ya kutosha hivyo kuongeza uzito wa jengo. Halafu kuna ujenzi mwingi unaendelea, mtu anajenga ghorofa lenye underground pembeni kabisa ya ghorofa jingine, yaani zero distance unategemea nini kama sio majanga baadae
 
Raha sana, mimi huwa sipendagi mambo ya shortcut hasa kwenye vitu critical.
Mabocc mkuu naona wanataka kuonekana nao wanamiliki magorofa kariako .ujenzi janja janja nyingi sehemu yakuweka nondo mm 20 ,anamwambia fundi ujenzi aweke nondo mm 12 😂😂😂
 
Na watu wakaacha kazi za uokoaji wakaanza kumsikiliza?Basi nchi hii tatizo ni kubwa zaidi ya tunavyolichulia aisee.
Sijui kwa nini wanapendaga kuhutubia kati kati ya majanga. Kwa wenzetu wanabaki waokoaji tu, watu wote mnatakiwa kuondoka hiyo sehemu. Hii nchi ni zaidi ya janga.
 
Badala ku plan business cente nyingine wao wanabanana na kariakoo tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…