Uchimbaji Wa mchanga ndani ya mto Msimbazi Ulongoni B

Uchimbaji Wa mchanga ndani ya mto Msimbazi Ulongoni B

passion_amo1

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2023
Posts
1,828
Reaction score
3,922
Wakuu Habari za uzima?
poleni na harakati za kuendelea kulijenga Taifa letu.

Kuna jambo nahitaji kuliandika hapa ili wenye mamlaka watusaidie kutupa ufafanuzi. Kwa muda sasa wakazi wa Ulongoni B Karibu na darajani mtakubaliana na mimi kumekuwa na gari aina ya kijiko kikichimba mchanga ndani ya mto.

Gari hili la kijiko la kuchimba mchanga limekuwepo kwa muda sasa, kutokana na kwamba muda mwingi tunashinda kazini, tunakosa hata muda wa kufatilia Mambo yanayoendelea ninapoishi. Kijiko hiki nilikuwa nakiona kwa mda kidogo, sasa nikajaribu kuuliza kwa mjumbe Kwa kweli sikupata majibu yanayoeleweka.

Hichi kijiko kinachimba mchanga ndani ya mto Msimbazi ambao kimsingi umepanuka sana, yanaingia malori makubwa zaidi ya 8 yanajaza mchanga na kuondoka nao sehemu ambayo sisi wananchi hatufahamu. Mpaka usiku saa 2 unakuta wapo wanachimba mchanga!

Mwenyekiti anapita anaona, Mtendaji wa kata anapita anaona lakini wapo kimya, tunaomba mamlaka husika watufafanulie mchanga huu unaochimbwa mpaka usiku na malori zaidi ya nane yakiwa yamejaa unapelekwa wapi? Na kwa mamlaka ya Nani wanafanya hayo?

Mheshimiwa mkuu wa wilaya Edward mpogolo na mbunge wa jimbo la ukonga na Waziri wa ardhi Mhe. Jerry slaa. serikali ije kutazama kinachoendelea au viongozi watupe majibu ya nini kinachoendelea.

Ahsanteni.
 
Huo mchanga unapelekwa zanzibar; ni kwa maelekezo kutoka juu
 
Back
Top Bottom