Marekani wakati wa utawala wa Bush hadi utawala wa Obama walikuwa wanataka kuweka makao makuu ya kamandi ya Afrika hapa Tanzania kwa sababu kadhaa; sasa hivi makao makuu ya kamandi ya Afrika nadhani bado yako Ujerumani. Sababu kubwa ya marais Bush na Obama kuja Tanzania na kusaka kiwanja cha kujenga makao makuu hayo, lakini maombi yao yalikataliwa, nadhani kwa msukumo fulani kutoka AU. Nakumbuka kipindi hicho watu wakisema nchi inatambulika sna hadi maraisi wa marekani wanashindana kuja Tanzania, lakini ukweli walikuwa wanakuja kutafuta maslahi yao.