Uchina itaiomba Tanzania (kama bado haijafanya hivyo) iwapatie kituo cha kijeshi (military base)

Nimesoma hiyo naval facility iliyokuwa inajengwa kwa siri na China imezuiwa baada ya Marekani kugundua faulo ile. US hawezi kubali UAE kutumika na China, ila sikutarajia kama hapo kabla UAE ingeweza kufikia hatua hiyo
 
Ukitaka kula, nawe ukubali kuliwa (Hii ni falsafa kubwa sana kwa anayejua dunia. Hakuna namna nyingine. Maisha yote ya binadamu yanazunguka kwenye falsafa hiyo!). Wajerumani walifanya hivyo, Wajapani, Wakorea....hata Wachina wenyewe, waliliwa kwanza!
 
Marekani iwaambie Tanzania kama ikifungamana na China, Marekani itaitambua rasmi Zanzibar kama nchi na itaisaidia kutambulika UN. Na vile vile Marekani iisadie Zanzibar kwa kuwapa silaha za kujilinda kama CCM wakitaka kuleta chokochoko Zanzibar. Kihistoria Zanzibar ilikuwa ni sehemu ya Oman na Oman wana uhusiano mzuri na Marekani. Zanzibar watumie mwanya huu kuchomoka na kupata maendeleo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…