Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Kitu nilichogundua ni kwamba kuna watu humu hawawezi kujisimamia.
Lazima wajishikize kwenye nguzo.
Yafaa kujisimamia.

Nashukuru ndugu yangu kwakugundugu hilo,

Hawa vijana tunao hapa tangu 12/01/2013, mara ya kwanza nilikwazika kwa aina ya michango yao isiyo na mashiko, lakini sasa nimewazoea na ninawaona kama waburudishaji wa uzi huu tu!

Wavumilie tusonge mbele ndugu!
 

yericko sasa tushakuwa waburudishaji tena??
Eti kwa michango yetu isiyo na mashiko,inashangaza sana kuskia kauli hizo kutoka kinywani mwako.
Terminology ya chandimu nadhan imewakaa sana akilini mwenu,jaribu kuwaambia hao ya kwamba ni wewe uliekawa wa kwanza kutututoa nje ya mjadala kwa maneno yako ya kejeli na tulipokukumbusha ukasema kejeli ni sehemu ya mnakasha au hayo hayakuwa maneno yako??
Waambie wajifunze tuh uvumilivu tusonge mbele.
 
Sasa wakati tunasubiri audio na video naona bora tujikumbushe TAA ilikuwaje mwaka 1950. Ilikuwa imelala au ilikuwa macho?
Sawa ngoja tuangalie unavyoelezea na uone unapinga nini na unathibitisha nini
..
Hebu tuangalie hapa chini ''The Life and Times of Abdulwahid Sykes...'' anasemaje:

Ikumbukwe ni wewe unasema haya siyo Abdul Sykes...so unajinukuu unachosema wewe...

[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD] Having established the political committee, Abdulwahid settled down to write to all TAA branches in the territory in order to revitalise them.


Revitalise manake ni nini? = kamuni inasema:

verb (used with object), re·vi·tal·ized, re·vi·tal·iz·ing. 1. to give new life to.

2. to give new vitality or vigor to.


Hapa unaendelea na kusema:







Unasema kuhusu 'slumber' je 'slumber ni nini'?

Slumber -

verb (used without object) 1. to sleep, especially lightly; doze; drowse.

2. to be in a state of inactivity, negligence, quiescence, or calm


Na hapa chini unasema tena:

What was now required were serious issues to stimulate the minds of the young intellectuals.

The TAA leadership did not have to look far.

Stimulate ni nini:

verb (used with object) 1. to rouse to action or effort, as by encouragement or pressure; spur on; incite:




[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Sasa katika maneno yote uliyotumia kuelezea utaona kuwa yanahusiana na hali kuwa ya kulala; slumber, stimulate, revitalise n.k Sasa Nyerere anaposema alipoingia alikuta chama kina hali ya kulala alikuwa anasema uongo? La hasha... inawezekana kulikuwa na juhudi za kuamsha lakini kwa kweli bado mwamko ulikuwa haupo na yeye alishiriki vilivyo kuiamsha vinginevyo utaelezea vipi safari zake za kuzunguka Tanganyika nzima?

Kwenye kitabu chako umetoa takwimu za idadi ya wanachama wa TAA kabla ya Nyerere kuingia na miaka michache baadaye wanachama walikuwa wangapi. Unaweza kuwaambia wasomaji wetu humu ongezeko la wanachama chini ya uongozi wa Nyerere na idadi ya wanachama wakati wa uongozi wa Kyaruzi na Sykes?
 
mkuu ulishaambiwa nenda ukacheze chandimu na wenzio hapa si saizi yako. Hebu soma mara mbili ulicho'comment then pima na uzito wa thread hii inayotazamwa na watu zaidi ya 20000. Uangalie kama hupaswi kuwa kwenye chandimu

kwa jns hilo neno chandimu lilivotumika kwenye mnakasha huu nadhan hata kulielewa hulielewi ndio maana unalitumia hata sehemu isipostahili kutumiwa..!!
Unafaham hasa mafuhum yake??
 
Mkuu Mohamed Said, kule nyuma ulisema Mwalimu Nyerere aliingia/alijiunga na mambo ya SIASA mwaka 1953 baada ya kuacha ualimu na kufika Dar huku ukikazia kuwa ni Abdul Sykes ndie alikuwa mlezi wake kisiasa,

Lakini katika hotuba ya Mwalimu Nyerere anasema wazi kuwa alianza siasa wakati akiwa Makerere hata kabla ya kwenda UK, na tayari alishakuwa Katibu wa TAA kanda ya Tabora,

Nukuu,

"Pale, mimi na wanafunzi wenzangu tulikuwa tumeanzisha chama kinachoitwa Tanganyika African Welfare Association (TAWA) cha wanafunzi wa Tanganyika; mimi nikiwa katibu wao".

Haya ndugu yangu unaizungumziaje kaul yako kwenye kitabu chako?
 
Si kwa maana unayoichukulia.
Usihamaki.

Kwa Kiswahili nikisema usilete vitisho ni kuwa
kama lipo jambo na wewe unashadidia badala
ya kusubiri mtu huweza kukuambia acha vitisho.
 
Nyerere hebu jipumzishe kidogo.

Kama Nyerere alikuwa anafanya siasa Uganda
hilo ni jambo zuri.

Tuangalie siasa za Tanganyika mwaka 1950.

Nasema hivi ili tuone alipofika New Street 1953
alikikuta chama kina hali gani.

Kiko macho au kimesinzia?
 
Hapo si mimi nasema.

Nimesoma nyaraka za Abdulwahid Sykes 1950.
Baada ya kusoma ndipo nikaandika hayo.

Ila shikilia kitu kimoja.
1950 Nyerere bado hajakutana na Abdu Sykes.

(Nyerere hajaja Dar es Salaam hadi 1952 na akaingia
katika uongozi April 1953)

Chama kimetoka kwa Mwalimu Thomas Plantan
na Mzee Clement Mohamed Mtamila 1949 kiko
mikononi mwa Dr Vedasto Kyaruzi na Abdulwahid Sykes.

Kuhusu wanachama wa na hapa nadhani unakusudia
wanachama wa TANU.

Wanachama wa mwanzo kundi kubwa walitoka Rufiji kenda
waandikisha Said Chamwenyewe.

Kisha kundi lingine likapatikana Lindi kwa msaada wa Yusuf
Chembera, Salum Mpunga na Masoud Mnonji.

Peke yake Nyerere asingefanikiwa katika sehemu hizi.

Na ilikuwa rahisi kupata wanachama kwa kuwa hawa wote
watu wa Kusini kuanzia Rufiji, Kilwa, Lindi, Mikindani ni wafuasi
wa Tariqa Quadiriyya na Khalifa wao alikuwa Sheikh Hassan bin Amir.

Huyu Sheikh Hassan bin Amir alikuwa ndiye Mufti wa Tanganyika na
mjumbe katika TAA Political Sub Committe 1950.

Hayo mengine ulouliza wala yasikushughulishe.
Una haki ya kuona upendavyo.

Si ajabu historia hii iliwatia unyonge baadhi ya viongozi wetu na hadi
leo imekuwa haipendezi kama tunavyoshuhudia hapa jamvini.
 
Tuanrudi kule kule, Mohamed, ushahidi wa kanisa kushinikiza unatoka wapi?

Halafu ulishaulizwa EAMWS ilianzia wapi na kwanini huko ilikoanzia haipo kwa sasa?

Unapozungumzia umoja wa waislam, ni upi huo kati ya Sunni, Shia, Bohora, Ismailia n.k.?
Nini kinashindikana kurudisha umoja huo?

Na hapo nyuma kuna post umesema wamishenari walijenga shule na kuwapendelea wakristo! Mohamed unajua maana ya missionary? Malengo yao na itikadi yao? Hivi ulitegemea EAMWS iwe na chuo kikuu kischobagua au kupendelea kule malengo yake yalipo?

Umeulizwa, mlezi wa iliyokuwa EAMWS alikuwa Agakhan, vipi mbona yeye anarudi na kujenga chuo kikuu kingine katika serikali ile ile iliyoua EAMWS 1968?
 
Naihurumia jamii ambayo imelishwa hizi ngano za Mohamed Said kwa muda wa miaka 15 na yenyewe ikapokea hizo ngano kama zilivyo. Huyu mtu hana nukuu yoyote iwe ya John Sivalon, Andulwahid Sykes wala hiyo listi ndeeefu ya anaowaita wazee wake. Anayotetea yeye ni mawazo yake aliyokaa akayatunga kwa malengo maalum hasa pale alipowasoma aliowakusudia na kutambua mapema kuwa watayapokea mazima mazima bila hata kujiuliza.

Nina wasi wasi na hizo anazozitaja kama nyaraka za Abdulwahid Sykes kama zipo na anazinukuu kama zilivyo, watu wa aina yake ndivyo walivyo, wachochezi. Nikitoa mfano ameombwa alete nukuu ya kitabu cha Sivalon kama kilivyo kuthibitisha maneno anayodai kuyasoma humo lakini kashindwa...kama kawaida ya mbea amebakia kujiuma. Kama tusingepata hiyo hotuba ya Nyerere ambayo imemuumbua mchana kweupee, bado angekazania tu uongo wake kuwa Mwalimu hakuwataja wazee wake.

Kuhusu nyaraka za hao wazee wa Mohamed Said ambazo anadai anazo, hata siku moja hajawahi kuzitoa popote pale, ziko tu kichwani kwake na hakuna mtu amewahi kumdai sauti wala video kuzithibitisha. Uwezekano mkubwa upo kuwa aliziandika yeye mwenyewe na kwa njia aliyotaka. Yeye leo pamoja na kutolewa hotuba ya Mwalimu kwa Wazee wake bado anadai uthibitisho wa sauti na ikiwezekana video. Sasa na mimi leo namwomba na yeye atuletee hapa sauti za wazee wake wakisema na kutenda anayodai Mohamed Said.

Sasa maajabu ya hawa wazee wa Mohamed Said! Sisi tukiongelea wazee wetu Watanganyika wa sehemu zote kusini hadi kaskazini, magharibi hadi mashariki, yeye amekazania wazee wake wa Gerezani Dar es Salaam (ukanda), tukiwataja wazee wetu Watanganyika wa makabila yote makubwa kwa madogo, yeye amekazania wazee wake Manyema na Wazulu (ukabila) na tukiwaenzi wazee wetu Watanganyika wa dini zote pamoja na wasio na dini, yeye amekazania wazee wake wa Kiislaam (udini).

Mwisho nina ombi kwa jukwaa (hii ni JF)...imeonekana kitabu/vitabu alivyoandika Mohamed Said havina ukweli na kama upo ni asilimia kidogo sana, sasa tusiishie hapa...tuende next step...wapotoshaji kama yeye adhabu yao ipo. Their works have to be discredited as academic dishonesty...a deliberate attempt to falsify, fabricate data, records, or information. Taasisi, Waandishi na wachapishaji wote aliowawekea maneno mdomoni kwa nukuu zisizo sahihi, juhudi zifanyike wajulishwe hatua ziweze kuchukuliwa. Nawapa changamoto wana JF.
 
Kitabu cha Bw. Said hakiwezi hata kidogo kuitwa kitabu cha historia; kwa yeyote ambaye amekisoma kwa makini atakuwa amegundua kuwa hakielezei historia kama ilivyotukia bali historia kama hisia za mwandishi zilivyomuongoza kuielewa. Nitatoa mfano wa swali moja ambalo Bw. Said hajalijibu hadi leo hii:

Nyerere alikuja Dar kwa mara ya kwanza mwaka gani?
 

Mag3,

Umekasirika sana.

Kuhusu kumweka Sivalon hivi lazima niweke mie. Hiki kitabu mbona maarufu tu si hata na wewe unaweza kukitafuta?
Basi unanishambulia kwa jambo dogo kama hili?
Msikiti wa Mtambani kimejaa tele bei shs: 2000 hadi shs: 1500.

Idara ya Historia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wapo wahadhir waliobobea katika historia si wafuatwe waambiwe wakichunguze
hiki kitabu changu kwani kuna tatizo gani?

JF si watu khasa wanaoweza kukufanyia kazi hiyo.
Hiyo changamoto umeipeleka sipo.

Kama hilo kubwa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam si wakifanyie hata pitio (review) mbona vyuo vya Ulaya na Marekani wamefanya?

Ingawa miaka 15 ishapita bado hujachelewa.
Fanya hayo na mimi Insha Allah utanikuta ni mwenye kusubiri.

Lakini nakuambia hawataweza na nakuambia tena hawataweza.
Kuna mengi usiyoyajua kama ulivyokuwa hujui kuwa ipo historia ya uhuru wa Tanganyika ambayo kabla ya leo hukujua ipo.

Nakuongeza watu ambao wanaweza kufuatwa kwa ajili ya kutazama nyaraka za historia ya uhuru wa Tanganyika.
Naamini watu hawa watatoa ushirikiano kama walivyotoa kwangu.

Wangine wa hai wengine weshatangulia mbele ya haki.

Nakuwekea hapa shukurani kama nilivyoandika katika ''The Life and Times of Abdulwahid Sykes (1924 - 1968) The Untold Story of the Muslim Struggle Against Colonialism in Tanganyika,'' Minerva Press London 1989.


[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD] I am grateful to the pioneers of change in Southern Province, Said Alley Mwalimu and late Mohamed Ali Abdallah ‘Makarios' both of Mikindani; to Salum Mpunga and Yusuf Chembera of Lindi, both of them now deceased, for letting me draw from their colonial experiences in southern Tanganyika; to Tewa Said Tewa, Dossa Aziz, Zuberi Mtemvu and Sheikh Haidar Mwinyimvua of Dar es Salaam; to Yusuf Ulotu of Moshi, popularly known as Yusuf Ngozi,Mohamed Kajembe, Rashid Sembe and Mmaka Omari of Tanga for providing me with unique information on colonial politics as it related to the ‘educated' African Christians on the one hand and the ‘uneducated' Afro-Arabs and African Muslims on the other. This information has helped me understand and interprete the conflict between Muslims and Christians which surfaced soon after independence and the contradictions which I have tried to depict in this work.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] I am also grateful to Omar Suleiman, Haruna Taratibu and Hassan Suleiman,[1] the brilliant political organiser of the period between the two World Wars, and to Germano Pacha, the last TAA provincial secretary and a TANU founder member, for his information on the formation of the Party; and to Rashid Mussa who, not knowing that the person he was referring to was my grandfather, informed me about my grandfather's early political career and his role in the first General Strike in colonial Tanganyika in 1947. I wish to pay special gratitude to Bilali Rehani Waikela, a Manyema gentleman and a devout Muslim. At twenty-five years of age in 1955, Waikela was one of TANU founding members in Tabora. [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] Waikela educated me about how Muslims as a political force supported Nyerere and the struggle for independence. He also briefed me about his days in detention with my grandfather at Uyui Prison for ‘mixing religion and politics'. I am indebted to him for putting at my disposal photographs of the period and his personal papers on the Muslim ‘crisis'which emerged soon after independence. I am grateful to Waikela for encouraging me to write this book and to write on the plight of Muslims as a result of their marginalisation by Nyerere's regime. Unlike many of my informants, Waikela allowed me to quote him without any fear. He was pleased to see that the information he had was being put to good use in preserving the history of our country for the benefit of future generations. He also put me in touch with other patriots like Mohamed Mangiringiri, Ramadhani Singo and others, whom I interviewed at length. [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] This work would not have been possible if it were not for the moral and material assistance I received from Ally Sykes. Ally Sykes allowed me to interview him on many occasions in spite of his busy schedules managing his business from his city center office. He allowed me to consult his own private files, personal letters, diaries and other family records. These records were kept in a safe which I was informed remained untouched for over thirty years. Going through the files I was amazed by Ally Sykes' obsession with record keeping. Every piece of paper with information was kept, however trifling it may have seemed during the struggle -a 1954 pencil note from Zuberi Mtemvu to Ally Sykes, informing him of a discussion he had with Nyerere about him and TANU; a 1953 money order receipt from Ally Sykes to Japhet Kirilo during the Meru Land Case; an undated copy of the letter from TAA to Queen Elizabeth signed by the entire executive (the President, Julius Nyerere, Vice-President Abdulwahid Sykes, General Secretary Dome Okochi, Assistant Secretary Dossa Aziz, Treasurer John Rupia, Assistant Treasurer Ally Sykes) congratulating Her Majesty on her coronation; a 1952 letter from Rashid Mfaume Kawawa from Bukoba to Ally Sykes informing him of the political situation in the Lake Region; a 1963 letter from Lady Judith Listowel; letters from Kenneth Kaunda, Julius Nyerere, Kasella Bantu ... the list is endless. This habit was apparently inherited from his father who used to file each and every piece of paper which had any information worth noting. [/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] It is a pity that I could not get access to Abdulwahid's diaries, which I understand had many entries in shorthand and are untranscribed. I was also not able to obtain World War I memoir of Kleist Sykes. There is no doubt whatsoever that these documents are invaluable. It is my hope that one day these important documents on the history of the Party and of our nation will find their way to the Tanzania National Archives for the benefit of future generations.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] Over the years, I had many discussions with members of the family, and got very useful information out of our casual talks. The result of all this is what I believe to be an authenticated historical narration of the life and times of Abdulwahid Sykes and other forgotten patriots to whom the country, CCM and the Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, owe so much in one way or another.[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] I wish to thank all those who allowed me to interview them but have asked for anonymity. Even those who refused to talk to me about the subject, and to publishers who rejected my manuscript out of fear and those who preferred silence, I must admit, in their own peculiar way contributed to this work.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Msemaji mmoja kanambia ningekuwa na uwezo wa kutunga kitu kama hiki kitabu hiki kiwe ni ''fiction'' tungelikuweka katika hadhi sawa na waandishi maarufu wa Kimarekani kama Irving Wallace, Ernest Hemingway, Mark twain na wengineo.

Bahati mbaya kitabu changu ni kazi ya kweli si ''fiction.''
Nimekosa bahati ya kuwekwa sawa kwa sawa na mabingwa hawa watunzi.

[SUP][SUP][1][/SUP][/SUP]A biography of Hassan Suleiman appears in Iliffe (ed) ‘The Politicians Ali Ponda and Hassan Suleiman,' in Modern Tanzanians, pp.227-253.
 
Mzee Said utaona kuwa katika shukrani zako zote huna Mkristu hata mmoja; hukutafuta familia ya Rupia kutaka kujua na wenyewe wana resources gani; hukutafuta familia ya Kyaruzi kutaka kujua na wenyewe walikuwa na resources gani; na cha kushangaza zaidi hukutafuta kuzungumza na familia ya Nyerere (Mama Maria bado yu haid) kutaka kujua baadhi ya tuhuma unazomrushia mumewe. Kimsingi, katika kuandika histohisia yako hukutaka kupata taarifa zozote ambazo zingepingana na kile ambacho tayari ulikuwa umedhamiria kukiandika - "historia" yenye msingi wa chuki dhidi ya Ukristu kwa ujumla wake na dhidi ya Mwalimu Nyerere binafsi.

It is this that makes your work incredibly discreditable! It follows none of the known rules of historical writing.
 

MM,

Hivi unataka tubishane kwa hilo?

Iwe itakavyo kuwa kwani kuja Dar we umeona jambo kubwa sana.

Mbona mimi sijakuja kutoka popote nimezaliwa pale Sewa Haji karibu na
Traffic Police.

Kulikuwa na hospitali pale.
 

Sawa huko sikupita sasa na nyie si ndiyo vyema mkaangalie kuna kitu gani?
Mkipata nanyi muandike?

Huko kwengine si na wewe uende kwani nani kakutazeni?

Kazi za kisomi anaekuja baadae anapita kule mwenzake hakufika.
Kwa njia hii kila siku kunakuwa na jipya.
 
MM,

Hivi unataka tubishane kwa hilo?

Iwe itakavyo kuwa kwani kuja Dar we umeona jambo kubwa sana.

Mbona mimi sijakuja kutoka popote nimezaliwa pale Sewa Haji karibu na
Traffic Police.

Kulikuwa na hospitali pale.
mwandishi wa historia asiyejua nyerere amekuja Dar Mwaka gani!
 

Ndugu yangu huko nishapita.

Siko hapa kutaka ushindi.

Nia yangu ni dunia ielewe upande wetu Waislam tunasema nini kuhusu
kuhujumiwa tusipate elimu.

Hilo nimelieleza na wapo watafiti wa nje na wao wamepita nilikopita mimi.
 

Sijui Kyaruzi alifariki 2012 na Clement Mtamila anaangukia kundi gani! wazee au waziii wa Mohamed Said
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…