Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


sawa mkuu,ngoja nimekuelewa sana,
na kwa vile yeye mwenyewe kakiri ya kwamba hatajibu tena ni bora tukaendelea na mnakasha huu.
Ila tumkanye tuh aache uongo na upotoshaji,unless otherwise aache kejeli zake kwa ndugu moh said ili darsa huru liendelee.
ndugu moh said tafadhali endele tu na darsa kwani huyo kijana anaejitambulisha kwa jina la yericko nyerere hana credibility ya aina yoyote ile ya kumuia yeye ni mchochez,mdini,mfitini and whatsoever..!

Tumekuja kujiridhisha ya kwamba ni mtu tuh aliyekurupuka na kukosa staha ya kuhoji mambo kisomi,japo tunamshukuru kwa uzi huu na pia tunakushukuru wewe ndugu moh said kwa kutufungua macho wengi.

Insha allah ulipwe yaliyo ya kheri hapa dunian na kesho akhera ndug yetu
moh said.

sisi tunauthamin na daima tutauenzi sana mchango wako huu.
 
Unaonesha hujamsoma kabisa Mohamed Said, ungepata jibu, hebu tulizana umsome ujuwe harakati zilianza lini na kina nani. Unaingia kutaka kubisha kitu ambacho huelewi. Kilichopindishwa ni nini?
Mmmmhhh kumbe Mdini zomba upo huku ?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Sooth, watakuja hapa na kelele nyingine kwamba unamkoso raisi kwa sababu ya uislam wake! subiri kidogo tu.

"nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe
 
Wildcard! Unakiri kuwa nyerere si muasisi wa AA wala TAA!...tatizo lako ni TANU.
 
Jee, uliwahi kumsikia Tosiri kabla ya kumsoma Mohamed Said?
Ingekuwa busara sana kama ungeuliza hivi "Jee, uliwahi kumsikia shujaa Tosiri kabla ya upotoshaji wa mzee muovu Mohamed Said?" Hakika ningekuwa na raha ya kujibu.
 

Naona wewe unachanganya mambo hujui hata kinachojadiliwa unaleta mambo ya Chadema na CCM hujui hata hawa wazee baada ya TANU waliachana na siasa wala CCM haiwahusu CCM ni ya Nyerere. Hawa wazee hawausiki tena nyie Chadema ndiyo mpambane kuing'oa CCM. Historia itaandikwa Chadema ambayo imejaa Wakiristu wamekitoa madarakani chama cha Nyerere. Umenipata nadhani.
 

Mnakasha wa ''kuasisi'' TANU ilikuwa kitendawili hata cha waasisi wa TANU zaidi ya miaka 50 sasa.

Nilipokuwa nafanya mahojiano na Mzee Germano Pacha Tabora kuhusu historia ya TANU Mzee Pacha
alisema maneno haya: ''Kama isingekuwa kwa ile picha tuliopiga leo hii kungekuwa na waasisi wengi
sana wa TANU.''

Maneno aliyasema mbele ya Sheikh Ilunga Kapungu aliyekuwa mwenyeji wangu Tabora na ndiye
aliyefanikisha kunikutanisha na wazee wa Tabora.

Nilikutana na Mzee Pacha ndani ya ofisi ya Mzee Rashid Mussa katika ofisi ya duka la wazee wa
pale Tabora.

Nakuwekea hapa chini ili uone uzito wa Mzee Rashid Mussa katika historia ya African Associatio na
TANU.

Katika maelezo haya vilevile utaona jinsi African Association ilivyokuwa inaanzishwa na utaona historia
ya uasisi.

Huenda historia hii ikatoa mwanga katika kujua nani muasisi na nani si muasisi.

I am also grateful to Omar Suleiman, Haruna Taratibu and Hassan Suleiman,[1] the brilliant political organiser of the period between the two World Wars, and to Germano Pacha, the last TAA provincial secretary and a TANU founder member, for his information on the formation of the Party; and to Rashid Mussa who, not knowing that the person he was referring to was my grandfather, informed me about my grandfather's early political career and his role in the first General Strike in colonial Tanganyika in 1947.

[SUP][SUP][1][/SUP][/SUP]A biography of Hassan Suleiman appears in Iliffe (ed) ‘The Politicians Ali Ponda and Hassan Suleiman,' in Modern Tanzanians, pp.227-253.

Hapo juu nimekuwekea kuonesha kuwa ni mzee wangu. Sasa endelea hapa chini:

[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD] Western Province, 1955[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD] Tabora began to participate in active politics in 1945 when the African Association was introduced to the township from Dodoma through the efforts of Edward Mwangosi.

The initiative in Tabora itself in forming the association of Africans came mainly from the Combine Dancing Club, a club formed by a group of young men of the township which had as one of its main activity the organisation of social affairs.

Strong members of the club were two Manyema brothers-Maulid Kivuruga and Abdallah Kivuruga; Chamnganda Usingizi, Ramadhani Nasibu, Rashid Mussa, Issa Kibira, Hamis Wabeba, Mwinyi Khatib Hemed, Swedi Juma, Issa Hamisi Pama and Rajab Kanyama.



[TABLE="class: MsoNormalTable"]
[TR]
[TD] On 3 rd March, 1945 the African Association was formed in Tabora with the following office bearers: Hamisi Simbe (President), Ramadhani Nasibu Vice-President, M.K. Hemed (Secretary), Chamng'anda Usingizi (Chairman), Fimbo Mtwana (Treasurer) and Rashid Mussa (Auditor). The African Association, like the club it had originated from, was dominated by Manyemas. It was in this way that the Muslim Manyema became the trailblazers of political development in Tanganyika.

Julius Nyerere witnessed the inauguration ceremony of the Association.[1]


Hemed wrote to the African Association headquarters in Dar es Salaam informing the leadership of its intention to open a branch in Tabora.[1]

[1] M.K. Hemed to the Secretary, African Association, Dar es Salaam, 11 th January 1945, TAA Tabora Party Archives File 741. For more information on African Association, Tabora, see Iliffe, A Modern History of Tanganyika op. cit. pp. 430-431.

[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 601"] In 1946, Makerere intellectuals started to show interest in the association when Hamza Mwapachu and Julius Nyerere, both graduates of Makerere College, were elected Secretary and Assistant Secretary respectively, with the other posts remaining in the hands of the Manyemas.

After the transfer of Mwapachu from Tabora, Nyerere became secretary of the Association. In the same year Nyerere travelled to Dar es Salaam as the Tabora delegate to the annual conference of the Association. This was the first time that Dossa Aziz came to know Nyerere.

But the friendship between Dossa and Nyerere did not flourish until 1952 when the latter came to Dar es Salaam and teamed up with other young nationalists like Abdulwahid, who was the president of the Association, and his young brother, Ally.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]


[1] E. A. M. Mang'enya, Discipline and Tears, Dar es Salaam University Press, 1984, p. 173.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

Muhimu ni kuwa hao wote niliowataja hapo juu walikuja kuwa waasisi wa TANU inategemea
msomaji amesimama vipi na wapi katika hiyo filosofi ya kuasisi. Hao wote waliingia TANU kwa
wakati mmoja ilipoasisiwa Tabora.

Katika tatizo la Nyerere na Abdulwahid Sykes tatizo lilikuwa hili.

Nyerere hakutaka la kwanza historia ya TANU ihusishwe na akina Sykes. Yeye akisimama kuwa
kuja kwake yeye ndiyo TANU ikazaliwa.

Lakini ni kweli yeye ndiye aliyeifanya TANU izaliwe?

Ukitaka jibu la swali hili inabidi urudi nyuma kwa baba yake Abdu, Kleist Sykes aliyeasisi African
Association na chama kikaendeshwa na wanawe hadi TANU ilipoasisiwa.

Baadhi ya watu wakawa wanasema lau kwa pembeni mmojawapo baba yangu Said Salum, rafiki wa
Abdu Sykes Ahmed Rashad Ali na watu wengine wa Dar es Salaam kuwa ''Nyerere hana asili na TANU.
Chama hiki mwenyewe Abdu Sykes mimi nikimshuhudia akifanya mambo yale siku nyingi.''

Leo nusu karne mjadala bado unafukuta na unaendelezwa na wajukuu...
 
zomba, siwezi kukubaliana na uzushi wa mpuuzi mwenzako mohamed saidi!

hii ndiyo kazi mnayotumana na ndugu zako kina yericko nyerere kuifanya sasa,

kumuita ndugu moh said mpuuzi na matusi mengine mengi tuh,yeye wapi kamwita mtu mpuuzi?

Ni kujiaibisha na kuharibu mantiki kuu ya mjadala huu,ingekuwa kama hajawatuma basi angewakemea kuacha matusi,si mara moja ama mara mbili ndugu moh said kaonekana kuwakemea wale wanaomuunga mkono yeye katika hoja zake kuacha kutumia lugha zisizofaa.
Mmeishiwa hoja
 


Mzee Mohamed Said, countless number of times alikua anasema kuwa kaandika historia ile ili wazee wake, ambao wamepigania uhuru, watambulike.

Sasa unavosema "Mbona Unamsemea" nakushangaa sana. Haupo makini inaonyesha.

Some tena thread hii upya alafu uje tena...

Nimemaliza
 
Last edited by a moderator:
Labda nipatie msamiati wa kumuita mtu anayefanya mambo ya kipuuzi huitwaje? mtu anayetumia taarifa zisizo na ukweli kupotosha watu anaitwaje?
 
Wala sihangaiki kukujua wewe ni nani kwakuwa haitaongeza wala kupunguza michango ya mimi na wewe hapa jukwaani!

Jambo jema ni kusonga mbele na mnakasha huu kwa elimu zaidi na ya mafaa kwa watanzania wote!

Sasa kaka, katika kusongesha mbele mjadala huu, nimekuuliza maswali yangu matano, umekataa kuyajibu. Mjadala utasonga vipi mbele na wewe kujibu maswali hutaki?

Pili, tutasonga vipi mbele hali yakua unamtusi mzee wa watu? maneno kama "umesimuliwa na wazee wako, ukajifungia ukaandika kitabu" kweli ndo tutaweza kusonga mbele kwa namna hii

Kama mjadala umekushinda, funga mjadala watu waendelee na shughuli zao za kawaida

Ninawasilisha
 
Sihitaji kuwa chadema kujua kwamba mambo hayaendi sawa nchini. Najaribu kufuatilia trend. Naelewa Mkurya wa Kitunda dar, anashabihiana na mkurya wa Mara. Mbona sioni wale 'wazee wa dar' waliopigania uhuru wakishabihiana, japo kwa mbali na 'wazee wa dar' wa sasa? Imekuwaje jamii ya wenye kuchukia dhuluma, leo hii inakula na kulala na wanaodhulumu? Kama kweli wazee wa dar walipigania uhuru kwa kiasi wanachotaka tuamini, basi ilikuwa kwa ajili ya maslahi binafsi.
 
Unakijuwa kisa cha Abushiri? au umepata kusikia kisa cha vita ya majimaji? hebu tumuombe Mohamed Said akupe historia fupi ya resistance ya pwani.

Abushiri wa Tanga? Majimaji ya Kusini (Ruvuma,Mtwara,Lindi na Iringa)? Nataka harakati za 'Mzizima' kupinga ujio wa wakoloni, dar-nyumbani kwa 'wazee wa dar'.
 
Mwenye kuandika kitabu anatangaza? unaona tu kimeandikwa kinachapishwa kinasambazwa. Huna ubavu huo.
Ubavu ninao, lakini sina agenda ovu kama ya mzee mwenzio MS! Maana unahitaji agenda ovu ili uandike kitabu cha kusadikisha yasiyo sadikika.
 

Hayo ni matusi? Ama wewe sio mswahili?
 
Kaishiwa hoja huyo Yericko hana mpya ye ndo udini umemkaa baada ya kuona mtu anayefanana nae jina hausiki na uanzishwaji wa TANU wala TAA bali alishirikishwa tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…