Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Niliwahi kusoma makala fulani kwamba MKWAWA alikuwa anajua kusoma na kuandika kiarabu, kama ni kweli lugha hiyo alijifunzia wapi?

Ndio alijua kusoma na kuandika kijerumani na kiarabu,

Ni chifu wakwanza afrika kujuakusoma nakuandika
 
hii mada ilikuwa nzuri naona sasa inaharibika na kupoteza mwelekeo, watu wanaelimika lakini vinaanza kuingia vitu visivyo stahili au visivyohusiana, kama mnakasha umefika mwisho basi ufungwe na kuanzisha mnakasha mpya kwa mambo mapya
Inaharibikaje mkuu?
 

Yericko Nyerere,

Pole sana mdogo wangu.

Kila siku jaribu ''to go an extra mile'' ahsante kwa hilo bandiko kwa maana halisi ya neno ''bandiko.''
Najua ulipotoa hiyo historia.

Sasa hebu sikiza maneno haya.

Mkwawa jina lake ni Abdallah Mkwawa, Mtwa-Mkwavinyika bin Mtwa Muyigumba Mwamuyinga.
Alikuwa na rafiki yake akiitwa Muhammad Khalfan Barwani maarufu kwa jina la Rumaliza.

Historia ya Mkwawa na hata ya Wajerumani weyewe katika Tanganyika haikamiliki bila ya
kumtaja Rumaliza.

Nimesoma bandiko lako taarifa hii muhimu sana haipo.

Sitaki kuendelea.
Nakupa home work hiyo hapo juu.

Rudi ulikopata hiyo historia uliotuwekea na fanya tena tafiti uje na majibu ya Mkwawa na Rumaliza
au ukipenda Muhammad Khalfan.

Nilibahatika kukutana na Muhammad Said Dubai hiki ni kitukuu cha Rumaliza.
Kanipa mengi kuhusu babu yake mkuu.

Mwisho Yericko nakukanya mdogo wangu kwa nia njema na mapenzi ya kaka kwa mdogo wake.
Hata siku moja usithubutu kunipa changamoto katika mambo haya.

Hapakuwa na sababu ya wewe kuanza na kitisho: ''Mohamed Said je wamjua mzalendo huyu aliye
ukataa ukoloni wa kijerumani?''

Mzee Abdallah Ross alikuwa rafiki ya baba yangu.
Mzee Ross ni mtoto wa dada yake Chief Mkwawa.

Watoto wa Mzee Ross ni rafiki zangu kwa hiyo naijua historia yao hata bila ya kusomeshwa.

Mzee Ross baba yale alikuwa Muingereza.
 


ni wazi kabisa ya kwamba hawakuwezi ndugu moh said,,

umewashika pande zote,wamebaki wana tapa tapa tuh.

Wape darsa.
 
hii mada ilikuwa nzuri naona sasa inaharibika na kupoteza mwelekeo, watu wanaelimika lakini vinaanza kuingia vitu visivyo stahili au visivyohusiana, kama mnakasha umefika mwisho basi ufungwe na kuanzisha mnakasha mpya kwa mambo mapya

Hilo nimeliona siku nyingi.
Uchovu umetuingia.

Bora tuipumzishe hii mada.
Labda kama Yericko itakuja clip ya Nyerere.
 
Vizuri sana Mohamed, kule Iringa huwa wanamuita Lumalisa na si Rumaliza

Ninachojua uswahiba wa Mkwawa na Lumalisailikuwa ni uwezo mkubwa wa Lumalisa kujua dawa za kuua watu, nitajitahidi kuwaona wanzagila akina Lumato walishikilia leo hii mizimu ya Mkwawa na baba yake Mnyigumba
 

Huna haja ya kwenda Iringa kote.

Tafuta kitabu ''Jihadi Kuu ya Majimaji 1905-1907'' cha Hussein Bashir Abdallah.

Huyu mwandishi ni ndugu yako kabisa.
Mwalimu Hussein ni mjukuu wa Sheikh Mohamed Ramia.

Yeye ni mwalimu wa historia.
 
Huna haja ya kwenda Iringa kote.

Tafuta kitabu ''Jihadi Kuu ya Majimaji 1905-1907'' cha Hussein Bashir Abdallah.

Huyu mwandishi ni ndugu yako kabisa.
Mwalimu Hussein ni mjukuu wa Sheikh Mohamed Ramia.

Yeye ni mwalimu wa historia.
Ninaukaribu na chifu wa huko sasa hivyo bora nipate habari zaidi za Lumalisa toka kwa wahusika kamili
 

Yericko,

Mimi sipendi kufanya kebehi kwa kuwa mimi sipendi
mtu anikebehi.

Mimi hupokea kebehi na masingi kutoka kwa wanangu
siku timu yangu Liverpool, Merseyside ikipata kichapo.

Nazomewa nyumba nzima maana nimezungukwa na
Man U.

Mke wangu hajui mpira lakini ananiunga mkono anasema
hawezi kustahamili kuona mumewe nafanywa kinyago
kwa hiyo na yeye anawaambia watoto kama mnamzomea
baba yenu na mimi nizomeeni.

Inasaidia kidogo kuwapunguza Man U kelele.

Rumaliza ati alikuwa na ujuzi wa madawa sijui nini...
Nimecheka peke yangu.

Yericko hebu tulia usome kwanza ndipo uingie dimbani.
Namna hii ni hatari.

Rumaliza sifa yake kubwa ni ''marksman.''
Kasome hiyo sitokupa tafasiri.
 
Kama mpakamda huu bado hujaelewa na kukibaini nilichokieleza kwenye uzi huu muhimu basi wewe unamatatizo

Nimepitia utumbo wa habari yako kwa kina na mapana na marefu, sijaona huo uchochezi wa Mohamed Said uliouweka kwenye kichwa chako cha habari.

Jee, unaweza kutumia kichwa chako ukanukuu huo uchochezi wa Mohamed Said? Naona tu umeteleza mpaka Iringa kwa Mkwawa.
 
Ndio alijua kusoma na kuandika kijerumani na kiarabu,

Ni chifu wakwanza afrika kujuakusoma nakuandika

Anajuwa kuandika Kijerumani? Halafu anawaandikia Wajerumani Barua kwa Kiarabu? Inakuingia akilini?

Jitihada zako za kujikwamua zinaelekea kuzuri.
 
kunachochote unachokijua katika historia ya nchi hii nje ya yaliyoandikwa na mohamed said?


vingi sana,,

kimoja wapo ni hiki>>yericko "x" si mwanafamilia wa julius kambarage nyerere,bali ni ulimbukeni wake tuh na kujipendekeza pendekeza ndiko kumemfanya aonekane chakubimbi kwa kung'ang'ania nasaba isiyo mhusu..!
Unakubali ama unakataa??
 
Mpaka sasa hakuna aliyethibitisha uchochezi wa Mohamed Said zaidi ya maneno matupu. Cha kufurahisha mnamkejeli mnamuita mpuuzi lakini mnasoma kwako historia ya Tanganyika.

Leo naangalia nyuma nakwenda mbali sana.
Toka utoto nikipenda sana kusoma na kusikiliza.

Wazee wakizungumza niko chini ya miguu yao mpaka
wakati mwingne inakuja, ''Mohamed haya kulala sasa.''

Nilipokujajua kusoma na kujua nini kimo katika vitabu
nikawa ''book worm.''

Nasoma vitabu vya Spaniards naingia nao melini
tunang'oa nanga tunaingia Atlantic.

Mawimbi yanapiga meli nami nimo tunaingia Amerika, nimo.
Nikinyanyua kichwa jua limezama.

Maghrib.

Library ilikuwa pale Mtaa wa Mkwepu.
Narudi nyumbani nimeazima kitabu naja kusoma nyumbani.
 
Kwamara nyingine ninakwambia kuwa wewe historia unaifahamu ya kuanzia 1950 tu,

Juu ya historia za machifu Tanganyika na afrika unahitaji msaada tena waharaka.

Wewe umesimuliwa na marafiki wa vituku wasiojua undani wa Mkwawa na wahehe.

Tafuta kitabu cha lugha ya kihehe kiitwacho "Ukoo wa Mkwawa na himaya zake"

Kimeandikwa na Wilium Malangalila mpwa wa Mkwawa.

Veve pe wimpefu yono, kong'omale ndikuwunge nyoko gunio ve.
 
Nadhani sasa ni muda muafaka wa kufanya mathalani tathmini kidogo ya yaliyojiri na ikiwezekana kuwawezesha wengi wanaofuatillia huu mjadala kutafakari yaliyojitokeza na kujiuliza maswali kadhaa. Mengi ya haya maswali ni yale ambayo ninaamini majibu yake hayapatikani kirahisi ndani ya vitabu alivyoviandika Mohamed Said kuhusiana na harakati za kudai uhuru wa Tanganyika. Hata hivyo nina ombi moja tu kwamba kuanzia sasa kama kuna hoja ama ufafanuzi unatakiwa kutolewa, utolewe kwa njia inayokubalika kwa lengo la kuelimishana lakini kama mtu hana hoja au jibu sahihi ingefaa sana akibakia msomaji tu.

Wanajamvi naomba kwanza tujaribu kujizuia na majibu ya dhihaka na kejeli tuweze angalau kudumisha amani, upendo, undugu na utanzania ambao tumejivunia kwa miaka mingi bila kubaguana kwa misingi aliyotuwekea Baba wa Taifa. Na pili naomba mimi niwe wa kwanza kumuuliza Mohamed Said maswali mawili matatu ambayo yanaleta utata katika maandiko yake ambayo, kama anavyodai ameyafanyia utafiti wa muda mrefu, sidhani kama atashindwa kuyajibu kwa ufasaha.. Mohamed Said, maswali yangu kwako ni haya;

  1. Baada ya TANU kuasisiwa, viongozi wake wengine wa juu, pasi Mwalimu Nyerere aliyechaguliwa kwa kishindo kuwa Raisi wake wa Kwanza, walikuwa ni akina nani, walipatikanaje (kuteuliwa au kupigiwa kura?) na kwa sifa zipi? Hapa nina maana ya Makamu Raisi, Katibu na msaidizi wake, Katibu Mwenezi kama alikuwapo, Mweka Hazina n.k Hapo naongelea iliyokuwa kama kamati kuu ya TANU baada ya kuzinduliwa kama iliwahi kuwepo.
  2. Kama viongozi hawa waliteuliwa, ni nani aliyewateua na kwa kuzingatia nini. Je, katiba ya TANU ilikuwa inasemaje na je ilifuatwa katika kuwateua?
  3. Kama viongozi hawa walichaguliwa, walipendekezwa na nani waweze kupigiwa kura? Je hawa wajumbe waliowachagua walipatikanaje? Je majina yao yanaweza kuwekwa wazi kwa wanaofuatilia mjadala huu?
  4. Imedaiwa na Mohamed Said kuwa TANU ilivyozidi kupanuka na kuenea sehemu mbali mbali, idadi ya viongozi Wakristo iliongezeka kwa kasi na kuanza kuwatia shaka wenzao wa Kiislaam...je hawa viongozi walipatikanaje? Je waliteuliwa au walichaguliwa kwa kupigiwa kura?... vyovyote vile je katiba ya TANU ilifuatwa?
Wanajamvi naamini haya maswali ya mwanzo ni muhimu sana katika kuangalia, kutafakari na kujiridhisha na timeline kuhusu baadhi ya Watanganyika walioshiriki karika harakati za kudai uhuru kutokuwa na imani na uongozi wa Mwalimu kabla ya uhuru. Baadaye tutaingia kwenye awamu ya pili nayo ni baada ya uhuru...kitu gani kilileta kutokuaminiana?

cc. sweke 34, Ritz, Nguruvi3, zomba, Mwanakijiji, Boko haram, Saint Ivuga, Ngekewa, Sideeq, Barubaru, Mohamed Said, Abdulhalim, Ngongo, Tuko, Pasco, AshaDii, Kibunango, Tume ya Katiba, masopakyindi, Dingswayo, BAK, matumbo, jmushi1, Son of Alaska, mdizi, Joka Kuu, Campanero, Yericko Nyerere, Spike Lee, Jasusi, warioba E.W., Remote, Nanren, Do santos, Raia Fulani, Wimana, Birigita, THE BIG SHOW, WildCard, njiwa, Mwita Maranya, Rutashobolwa, Mchambuzi, kichwakigumu, adolay, Kituko, deadteja, Fundi Mchundo, Bukyanagandi, Mungi, Mingoi [/QUOTE]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…