Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

kacheze chandimu hapa si mahala pako

Ullikuwa unamjuwa Suleiman Masudi Mnonji na Mohamed Waziri kabla ya kumsoma Mohamed Said? unataka ufaidi huu uhondo wa hili darsa peke yako? tulia upate darsa kidogo, japo hulipendi lakini linakuingia.
 
Kama nilivyokuambia hawa ndiyo wajanja wa JF anakejeli madrasa halafu anamtaja Ritz. Wazoee kaka.

Anakejeli madrasa halafu yeye mwenyewe yuko hapa anapata darsa kutoka kwa Mohamed Said.

Yericko muanzisha nyuzi, mwenyewe katulia tuli anapata darsa na anaanza kuuliza maswali, eti anamuuliza Mohamed Said kama anamjuwa Mkwawa?
 
MM,

Nime nimekusoma.
Lazima sisi kama binadamu tutakhitilafiana.

Wewe unakhitilafiana na mimi kama mimi nilivyokhitilafiana na kitabu
cha Historia ya TANU kilichoandikwa na Chuo Cha Kivukoni.

Sawa...

Kitabu hiki hakikuwataja wazee wangu waliopigania uhuru wa Tanganyika.
Sikufurahi.

kauli sahihi ni "walioshiriki" kwa sababu ukisema "waliopigania" ni kana kwamba walikuwa peke yao! Kwa hakika unayo haki ya kuweka rekodi sawa.
Nikanyanyua kalamu nikwarejesha katika historia kupitia kitabu changu.

Tatizo ni kuwa hujawarejesha kwa haki; umejaribu kuwapachika katika historia ilimradi na wao wawemo. Ili ufanikiwe katika hilo ikabidi uwaache wengine, au kuwadunisha wengine. Hili halikuwa sawa. Ungeweza kabisa kuwarejesha katika mahali sahihi pa historia bila kuwaondoa wengine!
Na wewe hujaridhika na kitabu changu kwa kuwaandika wazee wangu una
haki ya kuandika kitabu chako.

La hasha; sina tatizo kabisa la wewe kuandika habari za wazee wako au habari za yeyote mwingine. Tatizo langu ni la kuita kazi yako ni kazi ya kihistoria. Hujafuata kanuni za uandishi wa kihistoria, sehemu nyingi umeandika kwa hisia bila ushahidi wowote, na umefanya hivyo kwa kusudio moja tu "kuwarejesha katika historia". Hukuzingatia ukweli wa historia wala ushahidi wake na umetumia muda mwingine kulazimisha hisia zako zitafsiri tukio la historia.

Hivyo, kisicho niridhisha mimi ni kuita kazi yako ni 'historia'. Ungeita 'SIMULIZI LA WAZEE WANGU" watu tungejua tunachukua 'ukweli kidogo' na utamu kolea!

Hivi ndivyo usomi unavyokwenda.
Kila siku ni kutafuta kile ambacho hakikiwa kinafahamika na kukiweka hadharani.

Kama nilivyosema hapo juu wewe hukutafuta kisichofahamika; ulitafuta kinachokubaliana na hisia zako. Kusema kweli kitabu chako nimekipenda kwa kitu kimoja tu ni hadithi nzuri na unajua kuisimulia. Lakini, likija suala la substance, kitabu chako kinakosa substance ambayo inaweza kusimama kwenye historical scrutiny. Binafsi kwa kutumia kitabu chako na ulivyoandika tu bila kuangalia kwingine naweza kabisa kuweka tafsiri tofauti ya matukio yale yale uliyoyaweka wewe na bado watu wakadhani nimeandika historia kumbe ni mimi hisia zangu tu.

Kitu pekee ambacho hukuwatendea haki wasomaji wako na laiti ungefanya jitihada kubadilisha ni kuwa umewafanya waamini wanasoma an academic book based on historical facts with verifiable proofs. Bahati mbaya tofauti yangu nawe iko kwenye substance ya kitabu chako na zaidi katika madai ambayo unayatoa na umeshindwa kuyatetea hata kwenye maandishi yako mwenyewe.

Kusema kuwa watu wasiokubaliana na wewe waandike kitabu chako ni kukwepa jukumu lako kama mtu uliyetaka kuandika historia. Binafsi ungetutendea sote hisani kwa kukubali kuwa utajitahidi katika matoleo yajayo ya kitabu hicho kuweka more substance na kupunguza uandishi wa hisia zaidi. Utafanya vyema mno ukikubali kuwa katika toleo lako la sasa kitabu chako kimeweka madai mengi yasiyo na ushahidi na utajihidi kuweka ushahidi mle ndani.

Kitabu cha Prof. Hamza Nyonzi (ambaye nilifanya mahojiano naye ya kina 2006) kuhusu Mwembechai ni kitabu ambacho kinamvuta wa historia kwani amejitahidi kwa kadiri ya uwezo wake kuweka ushahidi kwa kadiri alivyokuwa navyo. Ninakipenda kile zaidi kwa sababu kimeandikwa kisomi na alipokubali kufanya mahojiano nami nilimuuliza baadhi ya maswali ambayo yalikuwa yananitatiza na alidiriki kuyajibu. Ukitaka Watanzania wenzako wachukulie kazi yako kama kweli ni ya kisomi usiishie kutoa madai tu; weka na ushahidi wa madai yako. Kutuambia tukasome wapi au twende kwa nani kutafuta ushahidi wa madai yako wewe ni kutufanya tufanye goose chase.

MMM
 
Kwa Mohamed Said na Echo chambers zake,

Article ambayo Mohamed Said aliiandika na Mwaikakagile kuitumia bila kumtambulisha kuwa yeye ndiye author hii hapa:http://allafrica.com/stories/200402170852.html

Mimi sikujua kuwa Mohamed Said ndiye Ally Sykes. Au ni Ally Sykes ndie ali-mplagiarise Mohamed Said?

Amandla.......

FM,

Umefanya haraka hebu tulia na nisome tena katika hiyo post.

Hiyo uloweka ni taazia niliyoandika mimi na inatokana na kitabu ''Under the Shadow of British
Colonialism...''

Niliweka jina la Bwana Ally kwa makusudi ya maombolezo.
Peter Colmore alikuwa mzee wangu kama alivyokuwa rafiki yake Bwana Ally.

Hapana makala hiyo siyo waliyonitaarifu rafiki zangu kuwa nimenakiliwa na mimi niliposoma kitabu
nimeona ufananaji katika uandishi na staili.

Sasa tafadhali talii kitabu hicho ''Life in Tanganyika...'' kisha rejea katika mnakasha endapo utaona
ipo haja.

Mnaandika na ghadhabu katika nafsi zenu ndiyo maana mnakosa utulivu wa fikra.
Mjadala hautaki hivyo.

Mjadala unataka utulivu wa hali ya juu kabisa.

Lakini kama nilivyokwishasema.
Katika Uislam hilo si kosa ni usambazaji wa elimu.

Waandishi wa namna hii hawabughudhiwi.
 
Muhammad b.Khalfan al Barwani alikuwa mfanyabiashara mkubwa wa watumwa. Ni kweli alipigana na wajerumani lakini haikuwa katika kutetea uafrika au waafrika bali biashara yake. Mwaka 1890, shujaa huyu alikuwa tayari kuungana na wajerumani ili mradi wamwachie eneo la kutawala kama mdhalimu mwenzake Tippu Tip. Mwaka 1908 aliandika kitabu kinachoitwa " ndoto za Sheykh Ahmad" ambacho kilitafsiriwa na baadhi ya watu kama wito kwa muangano wa waislamu. Huyu, bila shaka, alikuwa muislamu kwanza na sidhani kama alijiona hata siku moja kama mwafrika. Kwa mtazamo wangu, kama alikuwa rafiki wa "Abdalah" Mkwawa basi ilikuwa marriage of convenience ya "adui wa adui yangu ni rafiki yangu". Unless tuambiwe kuwa "Abdalah" Mkwawa alipokuwa akipigana na wajerumani alikuwa anatetea uislamu wake na sio wahehe wake! Rumaliza akama alivyokuwa Tippu Tip hakuwa shujaa wa Afrika. Kwangu mimi, hakuwa na tofauti na wajerumani aliokuwa akipigana nao.

Amandla.....
tippu.tip_.jpg

Kwi kwi kwi teh teh teh!
 
Naona jina la ''Abdallah'' liko katika ''quotation marks.''
Najua uko katika shida kubwa kukubali ''new information.''

''Denial'' ni kitu cha kawaida katika mambo kama haya.
Siwezi kukulaumu katika hili.

Mkwawa alikuwa na kamanda wake mmoja huyu vilevile
alikuwa ni ndugu yake jina lake akiitwa Yusuf.

Fika katika Makumbusho ya Mkwawa, Kalenga uone hata
mswala aliokuwa akiswalia Mkwawa.

Kuhusu utumwa naomba nikugusie kitu kidogo.

Ile biashara ya Across Atlantic Slave trade kulikuwa na meli
ya kubeba watumwa iliyopewa jina ''Jesus.''
 
Sawa...

kauli sahihi ni "walioshiriki" kwa sababu ukisema "waliopigania" ni kana kwamba walikuwa peke yao! Kwa hakika unayo haki ya kuweka rekodi sawa.

Tatizo ni kuwa hujawarejesha kwa haki; umejaribu kuwapachika katika historia ilimradi na wao wawemo. Ili ufanikiwe katika hilo ikabidi uwaache wengine, au kuwadunisha wengine. Hili halikuwa sawa. Ungeweza kabisa kuwarejesha katika mahali sahihi pa historia bila kuwaondoa wengine!

La hasha; sina tatizo kabisa la wewe kuandika habari za wazee wako au habari za yeyote mwingine. Tatizo langu ni la kuita kazi yako ni kazi ya kihistoria. Hujafuata kanuni za uandishi wa kihistoria, sehemu nyingi umeandika kwa hisia bila ushahidi wowote, na umefanya hivyo kwa kusudio moja tu "kuwarejesha katika historia". Hukuzingatia ukweli wa historia wala ushahidi wake na umetumia muda mwingine kulazimisha hisia zako zitafsiri tukio la historia.

Hivyo, kisicho niridhisha mimi ni kuita kazi yako ni 'historia'. Ungeita 'SIMULIZI LA WAZEE WANGU" watu tungejua tunachukua 'ukweli kidogo' na utamu kolea!

Kama nilivyosema hapo juu wewe hukutafuta kisichofahamika; ulitafuta kinachokubaliana na hisia zako. Kusema kweli kitabu chako nimekipenda kwa kitu kimoja tu ni hadithi nzuri na unajua kuisimulia. Lakini, likija suala la substance, kitabu chako kinakosa substance ambayo inaweza kusimama kwenye historical scrutiny. Binafsi kwa kutumia kitabu chako na ulivyoandika tu bila kuangalia kwingine naweza kabisa kuweka tafsiri tofauti ya matukio yale yale uliyoyaweka wewe na bado watu wakadhani nimeandika historia kumbe ni mimi hisia zangu tu.

Kitu pekee ambacho hukuwatendea haki wasomaji wako na laiti ungefanya jitihada kubadilisha ni kuwa umewafanya waamini wanasoma an academic book based on historical facts with verifiable proofs. Bahati mbaya tofauti yangu nawe iko kwenye substance ya kitabu chako na zaidi katika madai ambayo unayatoa na umeshindwa kuyatetea hata kwenye maandishi yako mwenyewe.

Kusema kuwa watu wasiokubaliana na wewe waandike kitabu chako ni kukwepa jukumu lako kama mtu uliyetaka kuandika historia. Binafsi ungetutendea sote hisani kwa kukubali kuwa utajitahidi katika matoleo yajayo ya kitabu hicho kuweka more substance na kupunguza uandishi wa hisia zaidi. Utafanya vyema mno ukikubali kuwa katika toleo lako la sasa kitabu chako kimeweka madai mengi yasiyo na ushahidi na utajihidi kuweka ushahidi mle ndani.

Kitabu cha Prof. Hamza Nyonzi (ambaye nilifanya mahojiano naye ya kina 2006) kuhusu Mwembechai ni kitabu ambacho kinamvuta wa historia kwani amejitahidi kwa kadiri ya uwezo wake kuweka ushahidi kwa kadiri alivyokuwa navyo. Ninakipenda kile zaidi kwa sababu kimeandikwa kisomi na alipokubali kufanya mahojiano nami nilimuuliza baadhi ya maswali ambayo yalikuwa yananitatiza na alidiriki kuyajibu. Ukitaka Watanzania wenzako wachukulie kazi yako kama kweli ni ya kisomi usiishie kutoa madai tu; weka na ushahidi wa madai yako. Kutuambia tukasome wapi au twende kwa nani kutafuta ushahidi wa madai yako wewe ni kutufanya tufanye goose chase.

MMM

MM,

Tusinase kwenye kitabu kina umri wa miaka 15.

Nina maandishi mapya mengi.
Itakuwa bora kama tungesonga mbele.
 
Lakini madai yako hayazeeka kwani bado ni ale yale. Kwenye maandisha mapya mengine umejaribu kuandika kihistoria zaidi au ni mwendelezo wa maandishi haya haya ya zamani?
 
Mkuu Moh, nilipo ona anazungumzia historia ya Mkwawa kwa kirefu bila ya kuzungumzia jina lake la ubatizo na alikuwa madhebu gani - ndio nikamwanzia mbali kwamba "nasikia Mkwawa alikuwa anajuwa kuandika na kusoma kiarabu" - amejibu ndio! Hii ina maana alikuwa anaelewa kila kitu, sasa kwa nini akulisema hilo, au ndio yanarudi yale yale ya kupidisha historia kwa kuondoa mambo muhimu ambayo yanaonekana yatawapa umaarufu watu/kudi fulani!!

Hata ili la kuanzisha historia ya Mkwawa kabla atujamaliza tuliyo anza nayo kwanza inashangaza kidogo, kuna jamaa walitaka alete vitu fulani fulani humu lakini naona hilo hakulitekeleza!

Wengi wetu humu tuna kiu ya kutaka kujua kiundani historia ya kweli kuhusu mababa/mababu zetu wanzilishi wa harakati za kupingana na ukoloni wa Kingereza, kuanzia kwenye miaka ya 1920s mpaka late 1950s, watajwe kwa majina yao, mchango wao na madhehebu yao - kama kuna baadhi ya wanaharakati walio shindwa kuelewana na Nyerere kwa sababu mbali mbali baada ya kukaribishwa kwenye kikundi chao, basi zielezwe sababu na ni nani alihusika kuwafuta kwenye historia ya nchi yetu na zitolewe sababu za msingi za kufanya mambo ya kiimla yanayo litia dosari historia ya Taifa letu, niliona juzi juzi hapa ndio JK alitumia uwanadamu kwa kuwakumbuka baadhi ya wanaharakati hawa kwa kuwatunuku nishani walio hai na wengine ambao wamekwisha tangulia mbele ya haki, sina shaka raia wema wataedelea kumpatia JK majina ya wale wote walio sahulika kuhusu harakati hizo.

Mimi nilikuwa nashauri historia kuhusu Mkwawa, Abushiri, Mangi Meli, Milambo, Rumanyika, Songea nk hayo tuachane nayo kwanza.

B,

Ahsante sana kwa fikra zako hizo.

Msiba mkubwa katika historia ya Tanganyika ni mkono wa Wamishionari
kujaribu kufuta athari za Uislam katika kila jambo linalowagusa Waislam.

Nenda Makumbusho ya Majimaji Mahenge Songea uone ufisadi unaofanyika
pale kubadili historia ya Waislam.
 
Lakini madai yako hayazeeka kwani bado ni ale yale. Kwenye maandisha mapya mengine umejaribu kuandika kihistoria zaidi au ni mwendelezo wa maandishi haya haya ya zamani?

Wewe unacho kitabu cha historia hata ujuwe namna ya kuandika historia?

Historia ya Mohamed Said imeandikwa kiufundi mkubwa hata wewe unalijuwa hilo na huwezi kuikosoa, amekwambia kama unaona kuna sehemu huiafiki si uandike yako? yeye hakuridhika na maandiko ya kivukoni akaamuwa kuandika na kukumbusha mashujaa waasisi wa kupigania Uhuru wa Tanganyika ambao hawakuandikwa kwa makusudi kabisa ya lengo la kuwa nyerere ndio kila kitu. Pili iko shamba inakuwashia nini? au ndio muujiza wa utakatifu umeyeyushwa?
 
Kama ni wewe uliyeiandika mbona iko katika first person narrative? Au wewe ndie ulianzisha kampuni ya Sykes Sales Promotion? Au wewe ndie uliyeajiriwa na Colmore katika kampuni yake ya real estate? Au haujaisoma ile appendix?

Mwaikakagile kwa kuiweka kwenye appendix na sio kwenye main body ya text kunaashiria wazi kuwa yeye sie author bali ni documents ambazo ameambatanisha kuongezea uzito yale aliyoandika mwenyewe.

Na mwisho amesema wazi kuwa ameitoa kwenye gazeti la The East African la 16 Februari 2004. Kwa hali hiyo hata kama ni wewe ndie uliyeiandika (kitu ninachotia wasiwasi) basi mtu yeyote ambae angetaka kujua nani mwandishi wa hiyo obituary, angekukuta.

Ndio maana nasema una pretensions of grandeur na sense of victimhood. Kila wakati unahisi umeonewa hata pale ambapo sio.

Mimi natumia neno mmisheni kama vile wewe unavyotumia uislamu. Kugawa, kuonyesha tofauti.Kuonyesha kuwa kwa mtazamo wako mkristu bado ni yule wa mishen kota, adui na mbaya wa waislamu. Tofauti yangu na wewe, mimi natumia neno hili kuonyesha upuuzi wa hoja hiyo. Mmisheni katika ujumla wake hajawahi kuwa adui wa muislamu na vice versa.

Amandla......

Huna haja ya kutumia neno ''upuuzi.''
Hapana haja ya kutukana.

Huu ni mjadala tu chukua kama uko nyumbani kwangu
nimekukaribisha chakula cha jioni tuko mezani tunakula.

Kwa kuwa sisi ni watu wa ''ideas'' lazima fikra itaingia
katika mazugumzo na gumzo litaanza.

Hapo kweli patakuwa na haja ya kutukanana?

Tulia kisha Insha Allah hamaki zikishuka tutaendelea na
mnakasha.

Nitakupa kwa nini ''orbituary'' ya Colmore iliandikwa kama
ilivyoandikwa na mengine mengi ya kukuburudisha wewe na
wanaukumbi.
 
FM,

Naona jina la ''Abdallah'' liko katika ''quotation marks.''
Najua uko katika shida kubwa kukubali ''new information.''

''Denial'' ni kitu cha kawaida katika mambo kama haya.
Siwezi kukulaumu katika hili.

Mkwawa alikuwa na kamanda wake mmoja huyu vilevile
alikuwa ni ndugu yake jina lake akiitwa Yusuf.

Fika katika Makumbusho ya Mkwawa, Kalenga uone hata
mswala aliokuwa akiswalia Mkwawa.

Kuhusu utumwa naomba nikugusie kitu kidogo.

Ile biashara ya Across Atlantic Slave trade kulikuwa na meli
ya kubeba watumwa iliyopewa jina ''Jesus.''

Kilemba?

chief.jpg

Naamini mpaka leo hii vazi lao la heshima wahehe ni kilemba na kanzu, hapo Chief Abdallah Mkwawa ndani ya Ihraam na Kilemba ananikumbusha Wasudan huyu.

KhartoumAP0312_468x596.jpg
 
Mkuu Moh, nilipo ona anazungumzia historia ya Mkwawa kwa kirefu bila ya kuzungumzia jina lake la ubatizo na alikuwa madhebu gani - ndio nikamwanzia mbali kwamba "nasikia Mkwawa alikuwa anajuwa kuandika na kusoma kiarabu" - amejibu ndio! Hii ina maana alikuwa anaelewa kila kitu, sasa kwa nini akulisema hilo, au ndio yanarudi yale yale ya kupidisha historia kwa kuondoa mambo muhimu ambayo yanaonekana yatawapa umaarufu watu/kudi fulani!!

Hata ili la kuanzisha historia ya Mkwawa kabla atujamaliza tuliyo anza nayo kwanza inashangaza kidogo, kuna jamaa walitaka alete vitu fulani fulani humu lakini naona hilo hakulitekeleza!

Wengi wetu humu tuna kiu ya kutaka kujua kiundani historia ya kweli kuhusu mababa/mababu zetu wanzilishi wa harakati za kupingana na ukoloni wa Kingereza, kuanzia kwenye miaka ya 1920s mpaka late 1950s, watajwe kwa majina yao, mchango wao na madhehebu yao - kama kuna baadhi ya wanaharakati walio shindwa kuelewana na Nyerere kwa sababu mbali mbali baada ya kukaribishwa kwenye kikundi chao, basi zielezwe sababu na ni nani alihusika kuwafuta kwenye historia ya nchi yetu na zitolewe sababu za msingi za kufanya mambo ya kiimla yanayo litia dosari historia ya Taifa letu, niliona juzi juzi hapa ndio JK alitumia uwanadamu kwa kuwakumbuka baadhi ya wanaharakati hawa kwa kuwatunuku nishani walio hai na wengine ambao wamekwisha tangulia mbele ya haki, sina shaka raia wema wataedelea kumpatia JK majina ya wale wote walio sahulika kuhusu harakati hizo.

Mimi nilikuwa nashauri historia kuhusu Mkwawa, Abushiri, Mangi Meli, Milambo, Rumanyika, Songea nk hayo tuachane nayo kwanza.

Yericko,

Mkwawa alikuwa Muislam.
Waislam hatubatizwi tunazaliwa tayari ni Waislam.
 
Mohamed hili ni kosa kubwa na nashangaa kwanini mtu wa uelewa wako anaweza kudhani ni jambo jema.

Kwa kadri nijuavyo uislam ni dini na ili uwe mwislam ni inakupasa kuisoma dini katika Korani, kusoma hadithi na kuzielewa sunna.Ndio maana katika Uislam wale waliobobea ni wasomaji wazuri sana hata kama wamezaliwa kutoka koo za mahalifa.

Notion ya kwamba baba anaitwa Mwinjuma na mama Mwanameka basi mtoto wao Mwanamtama atakuwa Mwislam ni upotofu mkubwa. Atakuwaje mwislam bila kusoma na kuielewa dini yake!

Matokeo ya haya ni kupata ''half baked'' scholars na kazi yao kubwa ni kupidisha mafunzo ili kukidhi haja zao.
Mfano ni Ilunga na wenzake wanaoamini kuwa ''kisasi'' ni neno linalosima lenyewe na hivyo kuropoka tu.
Matokeo ya haya ni kupata washabiki na si waumini.

Anyway hii ilikuwa off topic turudi kwenye mnakasha na hasa hoja za Mag3 na tathmini ya mnakasha.
 
Yericko Nyerere,

Ungepunguza mabandiko yako ya post ya mwanzo na kuyaweka posts tofauti, ingepunguza ukubwa wa page. Umesomeka na ukiyaweka hayo mabandiko kwenye posts tofauti yatasomeka vilevile. Kuwa mbunifu kidogo,
 
Last edited by a moderator:
Mohamed hili ni kosa kubwa na nashangaa kwanini mtu wa uelewa wako anaweza kudhani ni jambo jema.

Kwa kadri nijuavyo uislam ni dini na ili uwe mwislam ni inakupasa kuisoma dini katika Korani, kusoma hadithi na kuzielewa sunna.Ndio maana katika Uislam wale waliobobea ni wasomaji wazuri sana hata kama wamezaliwa kutoka koo za mahalifa.

Notion ya kwamba baba anaitwa Mwinjuma na mama Mwanameka basi mtoto wao Mwanamtama atakuwa Mwislam ni upotofu mkubwa. Atakuwaje mwislam bila kusoma na kuielewa dini yake!

Matokeo ya haya ni kupata ''half baked'' scholars na kazi yao kubwa ni kupidisha mafunzo ili kukidhi haja zao.
Mfano ni Ilunga na wenzake wanaoamini kuwa ''kisasi'' ni neno linalosima lenyewe na hivyo kuropoka tu.
Matokeo ya haya ni kupata washabiki na si waumini.

Anyway hii ilikuwa off topic turudi kwenye mnakasha na hasa hoja za Mag3 na tathmini ya mnakasha.

Kuwa Muislaam si kusoma Uislaam au kuusoma Uislaam. Kuwa Muislaam ni kujisalimisha kwa aliyekuumba. Unapozaliwa tu, wewe tayari uko katika kujisalimisha kwa muumba wako. Ukristo ndio hauwi mkiristo mpaka ubatizwe. Uislaam unaamini kila kiumbe anazaliwa Muislaam (kajisalimisha kwa mola wake, akipenda asipende).

Na unapokuwa na fahamu zako na ukausoma zaidi Uislaam ni vyema zaidi, lakini usitake kupotosha watu. Wewe umeambiwa Chief Abdallah Mkwawa ni Muislaam na mpaka msala aliokuwa akisalia uko makumbusho yake Iringa. Sasa kataa hilo lakini usijidai "Kwa kadri nijuavyo uislam ni dini na ili uwe mwislam ni inakupasa kuisoma dini katika Korani", ujuavyo wewe si sahihi na unazidi kupotosha.

Kumbuka inaitwa Qur'an na siyo "Korani" kama utakavyo wewe.

Kama unataka kujadiliana zaidi juu ya hili funguwa nyuzi yake tukupe darsa ya Uislaam ni nini na dini ina maana gani. Usitafute pakutokea.
 
Kitabu cha Prof. Hamza Nyonzi (ambaye nilifanya mahojiano naye ya kina 2006) kuhusu Mwembechai ni kitabu ambacho kinamvuta wa historia kwani amejitahidi kwa kadiri ya uwezo wake kuweka ushahidi kwa kadiri alivyokuwa navyo. Ninakipenda kile zaidi kwa sababu kimeandikwa kisomi na alipokubali kufanya mahojiano nami nilimuuliza baadhi ya maswali ambayo yalikuwa yananitatiza na alidiriki kuyajibu.

MMM

Mkuu Mzee Mwanakijiji fanya hisani tupate clip ya mahojiano yako na Ust. Njozi ili tupate ilim zaidi juu ya yale ya mwembe chai
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom