Mkuu Moh, nilipo ona anazungumzia historia ya Mkwawa kwa kirefu bila ya kuzungumzia jina lake la ubatizo na alikuwa madhebu gani - ndio nikamwanzia mbali kwamba "nasikia Mkwawa alikuwa anajuwa kuandika na kusoma kiarabu" - amejibu ndio! Hii ina maana alikuwa anaelewa kila kitu, sasa kwa nini akulisema hilo, au ndio yanarudi yale yale ya kupidisha historia kwa kuondoa mambo muhimu ambayo yanaonekana yatawapa umaarufu watu/kudi fulani!!
Hata ili la kuanzisha historia ya Mkwawa kabla atujamaliza tuliyo anza nayo kwanza inashangaza kidogo, kuna jamaa walitaka alete vitu fulani fulani humu lakini naona hilo hakulitekeleza!
Wengi wetu humu tuna kiu ya kutaka kujua kiundani historia ya kweli kuhusu mababa/mababu zetu wanzilishi wa harakati za kupingana na ukoloni wa Kingereza, kuanzia kwenye miaka ya 1920s mpaka late 1950s, watajwe kwa majina yao, mchango wao na madhehebu yao - kama kuna baadhi ya wanaharakati walio shindwa kuelewana na Nyerere kwa sababu mbali mbali baada ya kukaribishwa kwenye kikundi chao, basi zielezwe sababu na ni nani alihusika kuwafuta kwenye historia ya nchi yetu na zitolewe sababu za msingi za kufanya mambo ya kiimla yanayo litia dosari historia ya Taifa letu, niliona juzi juzi hapa ndio JK alitumia uwanadamu kwa kuwakumbuka baadhi ya wanaharakati hawa kwa kuwatunuku nishani walio hai na wengine ambao wamekwisha tangulia mbele ya haki, sina shaka raia wema wataedelea kumpatia JK majina ya wale wote walio sahulika kuhusu harakati hizo.
Mimi nilikuwa nashauri historia kuhusu Mkwawa, Abushiri, Mangi Meli, Milambo, Rumanyika, Songea nk hayo tuachane nayo kwanza.