Nimekuuliza mwanzo kabisa nitajie wanachama 20 wa mwanzo ndiyo ukaniwekea haya majina.
Haya majini nilikuandikia nimekuuliza hakuna hata mmoja alikuwa mwanachama wa mwanzo wa TANU.
Mchambuzi,
Ni kweli Bibi Titi Mohamed hakuwa mwanachama wa mwanzo wa TANU?
Hapa tunajifunza mengi kuhusu historia yetu.
hivyo ndivyo historia niliyosoma inanieleza, kama una ufahamu zaidi, hapa ndio sehemu yake ya kutuelimisha wengine;Nimekuuliza mwanzo kabisa nitajie wanachama 20 wa mwanzo ndiyo ukaniwekea haya majina.
kwanini hautoi ufafanuzi na kujadili hoja zako kwa kina kama nia yako ni kutuelimisha?Haya majini nilikuandikia nimekuuliza hakuna hata mmoja alikuwa mwanachama wa mwanzo wa TANU.
Mchambuzi
,
Ni kweli Bibi Titi Mohamed hakuwa mwanachama wa mwanzo wa TANU?
Hapa tunajifunza mengi kuhusu historia yetu.
Ni kweli, na binafsi sielewi kwanini ilitokea hivyo; Lakini kwa wale wenye upeo mdogo kama zomba, wanaweza kudai kwamba haya yalikuwa ni makosa ya Nyerere wakati TAA ilikuwa ni chombo ambacho Nyerere hakuwa na mahusiano nacho kabla ya 1954;
Kwa hiyo mimi nikawa katibu wa katawi ka TAA hapo Makerere. Niliporudi Tabora na kuanza kufundisha pale St. Marys (sasa inaitwa Sekondari ya Milambo), nikachaguliwa katibu wa TAA wa jimbo ambalo makao yake makuu yalikuwa Tabora. Ulipofanyika mkutano wa TAA mjini Dar es Salaam, nilihudhuria nikiwa mjumbe kutoka Tabora.
Kwa hiyo nilikuwa naijua Tanganyika African Association. Nilipokuwa ninaondoka kwenda Ulaya kusoma, nilikuwa nimeishaonja shughuli za TAA. Sasa niliporudi, baada ya kukaa Pugu siku chache, nikaja mjini Dar es Salaam. Nikauliza nani wanaongoza TAA? Nikaambiwa kuna jamaa mmoja anaitwa Abdul Sykes. Sasa ni marehemu. Abdul ndiye alikuwa katibu wakati huo.
MKuu Ritz, n
imekufatilia tangu mwanzo wa huu mnakasha na mara nyingi unakuwa ndani ya mstari na mara chache unaingia kwenye marumbano yasiyo na hoja, lakini naomba nikiri kuwa una vitu vingi ama niseme una info nyingi lakini unazitoa kwa kubanabana au kwa kutega watu, ningekuomba uiweke hapa List sahihi ya waasisi wote wa TANU bila kujali itikadi zao za Imani wala Kikabila, naliomba hilo kwa faida ya wote tunaofatilia manakasha huu
IKUMBUKWE PIA WAFATILIAJI WOTE WA MNAKASHA HUU WANAKUBALI KUWA KUNA MAPUNGUFU KWENYE HISTORIA YETU, KUNA KUSAHAULIWA KWA MATUKIO AMA WAASISI WA TAIFA LETU
kinachopingwa humu ni kile kitendo kuwagawa waasisi wa Uhuru wetu kwa minajili ya Kidini (Islam), Kikabila (Zulu and Manyema) na Kikanda (Gerezani-Mzizima)
Wazee tukae kwenye mada husika hayo mengine si mahala pake.
Ndugu yangu Kituko,
Hapa tunajifunza mengi sana mie najua machache kutokana na kuambiwa na Wazee wangu na kujisomea tu. Kuna watu humu wana vitu vingi sana tatizo mitazamo tuendelee kusoma humu ndugu yangu tutajua mengi.
Hivi nia yako ni kujaribu kubaini iwapo ninafahamu au hauna ufahamu na unataka kuelimika katika hili;
Mwasisi ni mwanzilishi, chama hakiwezi kuwa na waanzilisha elfu kumi, chama kinatokana na juhudi za watu wachache ambao wanakaa pamoja na kuamua kuunda organization husika, kisha baadae kuanza kufanya recruitment; Kwa mujibu wa historia ya nchi yetu, waasisi wa TANU ni hao kumi na saba na mengine nimeshajadili huko juu;
Kuhusu TANU kuasisiwa Burma, huu ni mwendelezo tu wa ujuaji - SO WHAT? Wewe unajua ANC ya Afrika ya kusini iliasisiwa wapi? Au what matters ni mafanikio yake...
Kaka nia yangu ni kujifunza wala sina nia ingine ili jukwaa letu sote hakuna ubaya kufahamishana historia.
WANAOONEKANA KWENYE WEBSITE YA CCM NI 17,SASA WA 18-20 SIJUI NINANI.
Achana na ANC hapa tunaongelea mambo ya nyumbani, usiwe kama mwenzako alipoona maji yanamzidi kimo akaanza Somalia, mara Nigeria.
Kwa hiyo, hao waasisi wa TANU Burma ambao wewe unasea ni muendelezo wa ujuaji, unawajuwa na kwenye historia yako ya kivukoni wamo? Na ulilijuwa hilo kabla hujamsoma Mohamed Said?
Mwasisi ni mwanzilishi, chama hakiwezi kuwa na waanzilisha elfu kumi, chama kinatokana na juhudi za watu wachache ambao wanakaa pamoja na kuamua kuunda organization husika, kisha baadae kuanza kufanya recruitment; Kwa mujibu wa historia ya nchi yetu, waasisi wa TANU ni hao kumi na saba na mengine nimeshajadili huko juu;
Kuhusu TANU kuasisiwa Burma, huu ni mwendelezo tu wa ujuaji - SO WHAT? Wewe unajua ANC ya Afrika ya kusini iliasisiwa wapi? Au what matters ni mafanikio yake...
Hoja ya msingi hapa ni kwamba mjadala kuhusu TANU iliasisiwa wapi hauna maana kwani hata hiyo Tanganyika yenyewe iliwekwa mipaka na watu ambao hawakuwa watanganyika;
Haina maana? hivi chama kilichodai Uhuru na waasisi wake waliofikiria kuiunda unasema haina maana? Unamjuwa Sheikh Takadiri, nilkubandikia post ya Mohamed Said inayomuelezea naona umeamuua kuuchuna.
Nakubaliana na wewe 100% kwenye nyekundu, kwenye buluu umechakachuwa, nnakuuuliza tena, umesahau au hujui kuwa TANU iliasisiwa Burma?
Ritz, Hapa ndio siku zote ninapoona kuwa tanganyika kuna historia mbili za Uhuru wake. Kwani watu maarufu kama Bibi TITI ambaye amepewaa mpaka mtaa mkubwa katikati ya Dar hayumo kabisa katika waasisi wa TANU, Achilia mbali akina KAwawa, Sheikh takadir, Jumbe tambaza na wengineo. Sijui Mchambuzi unaweza kutueleza nini kuhusu hawa. J e walipandika Train la TANU njiani na hawakuanzia mwanzo?