Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

MM

Kwani mimi nimekuuliza wewe maswali?
Mimi nimeandika kutoa darsa.

Hebu na wewe toa darsa nasi tusome.

darsa gani unalotoa ambalo unataka watu wapokee kama makinda ya kasuku? darasa ambalo mwalimu haulizwi maswali siyo darasa hilo. Ili darasa lako lieleweke wewe kama ni mwalimu - au unajiona hivyo - ni lazima uwe tayari kusikiliza maswali, na kuyajibu ili kusitokee kutoelewa au watu wakaondoka na kutokuelewa. Au unataka watu wasikie simulizi lako na waitikie "naam" na wasiulize swali? Miye sina tatizo kuulizwa maswali ninapotoa darasa langu na najaibu maswali yote ninayoweza kujibu nisiyoweza nasema siwezi au nitatafuta majibu.

Sasa mwenzetu na weye unataka watu wakusome tu wakubali na wasithubutu kujiuliza maswali au wao kukuuliza maswali. Kweli hiyo unaita elimu? Hata wajumbe wa Mwenyezi Mungu hawakukwepa maswali; ukisoma vitabu vya kidini utaona jinsi gani maswali ni sehemu ya kufahamu na kupata ujuzi zaidi. Inashangaza sana ndugu yetu kukwepa maswali kwenye somo ambalo wewe mwenyewe unatoa.

Mzee kubali maswali na uyajibu unayoweza ndio usomi wenyewe huo.
 
MM
Kwani hujasoma kitabu?


Nimesoma cha kwako; hicho cha Kivukoni sijakisoma ndio maana nimekuuliza kwani kwenye kitabu chako hujatawekea hicho cha Kivukoni kimesema nini zaidi ya kusema kimewaacha wazee wako. Nimejibu swali lako; jibu ya kwangu.
 
Mkuu sheria ya kupambana na ugsidi imeasisiwa marekani na mataifa mengine yameshurutishwa kuiridhia, sidhani kama nisehemu ya manyanyaso kwa uislamu duniani
 

MM

Kitabu cha miaka 15 iliyopita...

Kitabu cha rejea vyuo vikuu...
Nijibu maswali ya Mwanakijiji...

Mie nikikufanyia ikhisani
...
Si zaidi si pungufu.

Nakuageni rasmi Insha Allah
tutakutana pindi mwaka.
 
Ronn M,

Kwani Kivukoni walipoandika historia rasmi na kuwatoa Waislam
na kumbakisha Nyerere peke yake hofu ilikuwa dini?

1.Ndugu, ukiniuliza malengo ya kivukoni kuandika na kuwatoa waislamu(kama kweli waliwatoa) ni mada mpya inayohitaji utafiti. Mathalani tunapaswa kujua nani walikuwa mandated kuandika hiyo historia, walitumia data gani, je historia hiyo ilihaririwa? Hakukuwa na waislamu hapo chuoni, kwenye timu ya waandishi au hata serikalini walioona upungufu huo?

2.Nimegusia udini mana ndio mwelekeo niliouana hapa. Na kama ingekuwa ingekuwa mhadhara wa kidini wala usingeona mchango wangu hapa maana tayari upo ndani ya uhuru wako. Ila kama tunataka kuandika historia ya nchi lazima tuwe na objective test! Otherwise tutakuwa na historia ya tanzania ya Kikristo.. Kiislamu nk! Itakuwa tunatengeneza misahafu mipya!
 
Sasa kama mjadala ni kuhusu mapungufu ya utawala wa awamu ya kwanza, yapo mengi tu na tunaweza anzisha uzi mwingine juu ya suala hilo;

Mimi sijaongelea mapungufu ya awamu ya kwanza wala ya pili wala ya tatu wala ya nne.

Unakumbuka post zako?

Jee, Nyerere aliwekwa kwa kina Sykes au hakuwekwa? pale mtaa wa Stanley?

Jee, unakumbuka uliongea kuhusu "recruitment"?
 
Yericko,

Wewe usijihesabu kuwa uko kwenye mjadala.
Wewe hapa uko katika darsa unasomeshwa.

Hujafikia makamu ya kufanya mjadala.

Wewe wasema, watazamaji ndio waamuzi wa mwisho, lakini mimi naamini kama ni shule basi nimekupa ambayo hatauwe ahera hautaipata kamwe, na umeipata bureeeee kabisa kutoka kwangu na kwa waungwana wengine hapa.
Mohamed historia huihui, wewe wazijua ngano zile za wazee wa kariakoo na historia ya kidini pekee,

Nazo ngano za kariakoo ni ile ya kuanzia 1950 tu kuja mbele.
 
Hehee heehee acha uchokozi mkuu!

Uchokozi? au huo u nyerere wako ni wakujipachika? nasikia hata Leticia nae ni nyerere, au anti yako yule ndiyo ukapatia huko hilo jina?

Kuna mmoja namjuwa yeye kauvuka u nyerere anaitwa manyerere.
 
MM

Kitabu cha miaka 15 iliyopita...

Kitabu cha rejea vyuo vikuu...
Nijibu maswali ya Mwanakijiji...

Mie nikikufanyia ikhisani
...
Si zaidi si pungufu.

Nakuageni rasmi Insha Allah
tutakutana pindi mwaka.

Kwa heshima yote na taadhima mzee Said tunashukuru sana kwa uungwana wa kujumuika nasi. Kuna msemo kuwa "penye wazee haliharibiki neno" na wewe umekuwa miongoni mwa wazee wachache ambao wamethubutu kukaa na kuzungumza na vijana na wazee na kushindanisha fikra na nina uhakika bado halijaharibika neno. Pamoja na kutofautiana tunapoanglaia jambo lile lile heshima yangu kwako imezidi mno na kwa kweli naamini wewe ni hazina ya taifa na sisi kama taifa kutokukutumia katika kukusanya historia yetu ni makosa makubwa.

Mchango wako katika bahari ya ujuzi hata kama ni kama punje ya mchanga bado ni mchango muhimu na ni jukumu la kila Mtanzania na hasa kizazi cha sasa kufanya utafiti wa kuzidi kuijua historia yetu. Kwa kukusoma wewe nimepata changamoto ya kuandika kazi moja ya kihistoria ili nami nitoe mchango wa kusahihisha ulipokwama wewe na kuongezea ulipojazia.

Nakutakia maisha marefu, ya baraka tele wewe na familia yako yote na Mwenyezi Mungu akupe kila jema ulitamanilo na uje kuona matunda ya jasho lako.

Katika Ujenzi wa Taifa


Nduguyo,
MMM
 
Asalaam Alekum, Shalom, Peace be apon you guyz!..
damn hivi bado nyie wadanganyika mnazungumzia maswala ya Nyerere, Uislaam na Ukristu?... ama kweli mzungu alituweza sana kutupachika wingu hili ktk bongo zetu.... Dah! ama kweli adui yetu mkubwa ni kutawaliwa kifikra haswaaaa!

Kwako Muhammed Said, Hakuna mtu apaswaye kuitwa Muislaam ikiwa hajajisalimisha kwa Mwenyezi Mungu (Total submission to God), hizi habari za watu kuzaliwa ktk Uislaam wa majina na ukoo na nasaba, kuvaa kanzu na kubaraghashia hauwezi kutumiwa kama ushahidi hata mbele ya Mwenyezi Mungu isipokuwa wale walojinafsisha mioyo yao na wakafuata waloamrishwa na vitabu bya Mwenyezi Mungu..Na ndio maana wapo wale waliofuata vitabu enzi za Nabii Issa (Yesu) na kabla ya Muhammad waliitwa Masara na kwa sababu moja tu kwamba walifuata kitabu na wakawasamilisha kwa Mwenyezi Mungu...Hii inarudi nyuma hadi wakati wa Ibrahim walikuwepo walojisalimishakwa Mwenyezi Mungu na wakatofautiana na baba, mama au kaka zao wa tumbo moja..

Kwa hiyo mkuu wangu, ni dhambi kubwa sana kujaribu kuutafsiri Uislaam kama Wakristu maana hawa ni kundi la watu waliomfuata Yesu ama Wayahudi (Jews) ambao ni kundi la watu waliokubali kumfuata Judea, Uislaam ni dini ambayo humfuati mtu isipokuwa unajisalimisha kwa Mwenyezi Mungu na kufuata yale uloamrishwa. Infact Muslims are not followers of Muhammad bali Muhammad ni mjumbe tu (messanger)...Hizi habari za kuleta jamii ya waislaam kwa kuzaliwa ama kwa sababu anaitwa Abdul, Ally, Omar na kutuweka sote kundi moja ni ujinga mwingine kufuata utamaduni wa watu wengine ilihali ukweli sivyo!

Binafsi yangu nachukia sana mtu anapotaka kutumia dini kuhalalisha ujinga ambao ndio sababu kubwa ya hao unaowaita waislaam kuwa nyuma. Na nimeshakwambia sana tu ya kwamba ikiwa enzi ya Nyerere ni asilimia 5 tu waliweza kupata nafasi ya kuendelea ma na masomo shule za juu, ulitegemea Waislaam wangapi wachaguliwe na kwa kigezo gani? yaani unataka kunambia asilimia 95 ya watoto waloshindwa kuendelea na masomo wote waliokuwa Waislaam!!..

Kama swala ni ELIMU leo hii basi lizungumzwe na tusitake sana kukwepa ukweli maana lipo wazi kabisa na Nyerere hayupo duniani. Tumeujenga mfumo huu mpya sisi wenyewe tena kwa matusi na rais akiwa Mwinyi sasa iweje Nyerere ndiye wa kulaumiwa?..Ama rais anapokuwa Muislaam jina basi hakuna makosa isipokuwa yule mwenye jina la kizungu?
 
Nichukue fursa hii kutoa shukrani za pekee kwa Mzee wangu Mohamed Said,
Mjadala wetu uliodumu siku 19 tangu ulipoanzishwa umedumu vyema huku ukiibua hisia kali na mafundisho yaliyomema kwa ustawi wa taifa leo.


Historia ya nchi hii haitabadilika, huo ndio ukweli na ukweli utatuweka huru, jambo jema ni kuwa tunaweza kuihuisha tu kwa maana ya kuboresha mapungufu yaliyomo lakini si kuibadili.
Niwashukuru tena wadau wenzangu tulioshirikiana kwa namna moja ama nyingine kuusongesha mbele mnakasha huu.

Lakini nitakuwa mchoyo wa fadhila kama sitawataja wafuatao kwa majina yao:

Ritz,zomba,The Big Show, na mzee wa kisu kikali BashaDido

Hawa licha ya mnakasha huukuwa na ghadhabu lakini walikuwa ni viungo muhimu na burudani ya pekee hapa jamvini.


Naaam natangaza rasmi kuufunga mnakasha huu.

Asanteni sana wadau wenzangu, Mungu atubariki na Mungu aibariki JF idumu daima.
 
Mohamed Said,

Tunashukuru sana kwa mchango wako nakuombea dua Allah akupe maisha marefu uzidi kusomesha...na mimi binafsi naondoka rasmi kwenye huu uzi.

JF Daima.

Mag3, Nguruvi3, Mzee Mwanakijiji,

Kama takuwa nimewakosea kwenye michango yangu naomba mniwie radhi.

Wanabodi wote members na wageni mliokuwa mnafuatilia huu mjadala nadhani mmepata vitu.

JF Daima.
 
Last edited by a moderator:
Mohamed Said,

Tunashukuru sana kwa mchango wako nakuombea dua Allah akupe maisha marefu uzidi kusomesha...na mimi binafsi naondoka rasmi kwenye huu uzi.

JF Daima.
msinikimbie leo nimepata wasaa wa kuwepo kijiweni tuyarudi yote yalowaganda mioyoni maana sasa naona watu mnataka kuidai hata dini ya Mwenyezi Mungu kuwa mali yenu...
 
Mohamed Said, unaondoka unatuacha wakiwa.
Hebu Spike Lee, naomba kama hajakuacha mkiwa, mkumbushe ajibu maswali yangu haya. Maanake naona anaanza kujikaanga mwenyewe kwa mafuta yake na hata internet etiquette inaanza kumpa taabu kuifuata...font hizo!... ni zaidi ya zile za THE BIG SHOW! Hiyo si dalili nzuri. Maswali yenyewe haya;
Asante, naendelea kusubiri (remember the vulture is a patient bird)...hii ni safari ya tatu namkumbushia.
 
Last edited by a moderator:
Jasusi,

Nani kakuambia Yitzhak Rabin?

Mie naongelea kipindi cha Menachem Begin 1979. Moshe Dayan kafariki 1981

Arafat alikutana Camp David wakati wa Bill Clinton ambaye aliingia mamlakani 1988. Hakukuwa na mkutano Camp David enzi za Menachem Begin.
 

Ndugu yangu; mzee wetu kiungwana ameshindwa kujibu haya maswali na kaomba tumruusu aende; kuendelea kumdai ayajibu ni kumpa mzigo asiouweza. Wasomaji wako humu watakuwa wameelewa kwanini hajayajibu maswali mengi na ndio maana tumruhusu tu aende apumzike kidogo. Labda next time hatokuja na madai yale yale tena.
 
msinikimbie leo nimepata wasaa wa kuwepo kijiweni tuyarudi yote yalowaganda mioyoni maana sasa naona watu mnataka kuidai hata dini ya Mwenyezi Mungu kuwa mali yenu...

Mkandara,
Ulikuwa wapi? Nilikuwa nikupigie simu leo maana sijakuona hapa kitambo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…