Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar


Zoomba acha kupotosha watu kwenye mambo yanayoonekana kabisa!
Hivi hapo kunamtu yupo chini ya ulinzi?

Polisi hao na Mzee Kasim Hanga wote wanasikiliza hotuba kwa umakini mkubwa lakini wewe unaanza kuwatutusa watu hapa eti mzee Hanga kawekwa chini ya ulinzi!
 

Una matatizo ya macho? tazama vizuri.
 

mohamed saidi, tunaomba majibu, ww ndo uliyeandika hy unayoita historia, haya jibu vigongo hivyo, vingnevyo unajishushia heshima ni bora ungepotea mojakwa moja humu ndani.
 
Rais wa TAA alikuwa Dr Kyaruzi,

Kisha nafasi hiyo ikakaimiwa na Katibu Abdul Sykes baada ya Dr Kyaruzi kuhamishwa De mpaka Mwalimu Nyerere alipokuja kumshinda katika uchaguzi wa pale Arnatouglo mnazi mmoja pale 1953

Yericko Nyerere,

Bado sana pinda mgongo zama uisome historia ya Tanganyika.

Nimekuuliza nani alikuwa rais wa TAA mwaka 1949 na Katibu Mkuu naona unajibu kwa kutumia akili yako.

Huo mwaka ulioandika sijui unamdanganya nani labda jamaa zako.
 
Last edited by a moderator:
Hivi mnashindwa kujiuliza ni kwanini zile nchi tajiri Duniani(G8) haina hata nchi moja toka Uarabuni?

Poleni sana wafia dini wa Gerezani kariakoo...mtatawaliwa na mfumo kristo mpaka mnaingia kaburini.
 
haaa? Kweli zomba wewe huu uwanja haukufai, hoja ya mchonga nayo ni hoja? Ndo maana mnamkamua marehemu eti kumsafisha mavi kwny utumbo huku mkiacha mikojo kwny kibofu, au siyo uchafu? None-sense.
 
Huwezi kusema kuwa unaijua historia ya TAA na TANU bila ya kuwataja vijana wasomi wa wakati ule.

Abdulwahid, Ally Sykes, Tewa Said Tewa, Stephen Mhando, Dossa Aziz, James Mkande, na madaktari wale watano, Joseph Mutahangarwa, Luciano Tsere, Mchael Lugazia, Vedasto Kyarunzi, Wilbard Mwanjisi.

Bahati mbaya hawa wote hawana maana tena wanaitwa wasaidizi tu wa Nyerere.

Familia zao hawa niliowataja zipo mpaka sasa hivi na wengine wanafuatilia huu munakasha kwa makini kwa wale wanataka kuchimba zaidi historia ya Tanganyika wanaweza kuzitafuta hizi familia.

Bahati mbaya hakuna kumbukumbu zao wakati wanapambana kuijenga Tanganyika.
 
Yericko Nyerere kwanini ulikataa hio offer ya pesa ili ununue hio audio?

Unajua wengine sio wavumilivu wa kitu walichoahidiwa?

Ahadi ni deni bwana, kutokuja kwahio audio kumenifanya niwe na wasiwasi wa post zako kwamba zina ukweli au hazina ukweli.
Once again sisi kama wafuatiliaji tunataka kujua upande wa pili wa shilingi.
Kama hutaleta audio basi kutanifanya nisiamini yooooote uliyoandika.
 
zubeda
hapo kwenye red
umenipeleka mbali sana
 
Last edited by a moderator:
Nilisema kwenye post zilizopita
kwamba 'huyu mume ni mkubwa'
Ulimtaka mwenyewe mvumilie,acha kupiga kelele
Povu linakutoka,ushatukana matusi yote
bado ya nguoni
 
Na Njelu Kasaka

Bunge lilitumia mamlaka yake kuchunguza na kulinda Katiba

· Wenye taswira ya kidekteta waliliandama Bunge

MWAKA 1992, Zanzibar ilijiunga kwa siri na Shirika la Kiislamu (OIC-
Organization of Islamic Conference) na taarifa hizo zilipovuja kwenye
vyombo vya habari, Bunge likaamua kuchunguza.

Uchunguzi ulilenga kubaini mambo matatu. Kwanza, kupata ukweli wa
jambo lenyewe kwa kuwa lilikuwa limejitokeza kwa njia ya vyombo vya
habari hususan magazeti. Pili, kubaini uhalali wa Zanzibar kujiunga na
Shirika hilo; na tatu, kujiridhisha kama kwa kufanya hivyo Zanzibar
haijakiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wakati Bunge lilipokuwa linaendelea na uchunguzi malalamiko
yalijitokeza kutoka Zanzibar na kwa baadhi ya viongozi wa dini ya
kiislamu upande wa Bara. Baadaye Zanzibar ilijitoa kwenye Shirika hilo
ambalo kwa sasa limebadili jina. Shirika hilo sasa linajulikana kama
OIC (Oragazation of Islamic Cooperation) na malengo yake pia
yamerekebishwa.

Tangu wakati huo, baadhi ya Waislamu na hata baadhi ya viongozi kutoka
Zanzibar wameendelea kunung'unika na kuitaka Serikali ya Jamhuri ya
Muungano ijiunge kwa madai kwamba kuna mambo ya kufaidika kimaendeleo
kwa Zanzibar na kwa Waislam wa Tanzania kwa ujumla.

Madai hayo yanasisitiza kwamba OIC ya sasa ni ya kimaendeleo zaidi
kuliko kidini. Kibaya zaidi kuna mwandishi mmoja, Said Mohammed katika
kitabu chake kiitwacho: Christian Hegemony and the Rise of Muslim
Militancy in Tanzania, sura ya nane, ameandika kwamba Bunge
lilichunguza Zanzibar kujiunga OIC kwa msukumo wa dini ya Kikristo na
kwamba wabunge Waislam hawakushiriki.

Huu ni upotoshaji wa hali halisi iliyokuwapo wakati huo. Na kama sisi
tuliokuwapo wakati huo tusipoweka mambo haya sawa upotoshaji huo
utachukuliwa kwamba ni ukweli.

Kwa kuwa mimi nilikuwepo bungeni na nilishiriki katika sakata hilo
kutoka mwanzo hadi mwisho nitatoa ufafanuzi wa jambo hili katika hatua
mbili.

Hatua ya kwanza nitachapisha taarifa ya ufafanuzi niliyoitoa mwaka
1993, bila kubadili neno, na katika hatua ya pili, nitajadili kwa
kifupi OIC ni nini na kugusia madai kwamba Serikali ya Tanzania
iliahidi kujiunga na OIC na kwamba ijiunge sasa.

Wengine wanakwenda mbali zaidi na kutaka suala la OIC liingizwe kwenye
katiba mpya. Kwa kuwa Tanzania ni mwanachama wa mashirika mengi tu ya
kimataifa sijui OIC itaingizwaje kwenye Katiba mpya! Ifuatayo ni
taarifa ya ufafanuzi kama ilivyochapishwa katika gazeti la Mwananchi
Aprili 19-25, 1993:

Bunge lina haki ya kuchunguza suala la OIC

KIKAO cha Bunge kilichofanyika Februari 1993, mjini Dodoma, kilijadili
pamoja na mambo mengine taarifa ya Marmo (Philip) iliyochunguza
uhalali wa Zanzibar kama sehemu ya Jamhuri ya Muungano, kujiunga na
Shirika la Nchi za Kiislamu (OIC).

Suala la Zanzibar kujiunga na OIC, shirika ambalo wanachama wake ni
mataifa kamili wakati Zanzibar ni sehemu tu ya Taifa la Tanzania
limezusha mgogoro wa kikatiba na kusababisha mjadala mkali bungeni.
Pia lilizusha hisia tofauti baina ya Wantanzania na hata wengine
wakadhani kuwa Bunge linahoji suala hili kwa vile Zanzibar imejiunga
na Shirika la Kiislam na si vinginevyo.

Ukweli ni kwamba Kamati ya Katiba na Sheria ilichunguza suala la
uanachama wa Zanzibar katika OIC kwa misingi ya kikatiba. Hapa pia
ningependa kuwaelewesha Watanzania kuwa Kamati ya Katiba na Sheria ni
moja ya kamati za kudumu za Bunge na wala haikuundwa na Naibu Spika,
Mheshimiwa Pius Msekwa kwa madhumuni ya kuchunguza uanachama wa
Zanzibar katika OIC kama vile ambavyo baadhi ya watu wangependa
ieleweke.

Mimi ni mmoja kati ya wabunge saba waliowasilisha waraka kwa Naibu
Spika kumwomba akabidhi kwa Kamati ya Katiba na Sheria suala la
uanachama wa Zanzibar ili lichunguzwe kuona kama kwa kufanya hivyo
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haikukiukwa.

Pia tuliomba kamati ichunguze tuhuma kuwa Tanzania ilikuwa mwanachama
wa siri wa Shirika la Kiislam la Afrika (Islam in Africa Organization-
IAO).

Wengi wameuliza kwa nini sisi wabunge saba tulifikia uamuzi wa kutaka
masuala haya mawili yachunguzwe na Kamati ya Bunge. Ikumbukwe kwamba
mwanzoni mwa mwezi Desemba 1992, Shirika la Utangazaji la Uingereza
(BBC) lilitangaza kwamba Zanzibar ilikuwa imejiunga na OIC.

Mbunge wa Kibondo, Bw. Arcado Ntagazwa alilizungumzia suala hilo
bungeni lakini serikali ilikaa kimya. Baadaye gazeti moja liliandika
kuwa ni kweli Zanzibar ni mwanachama wa OIC.

Baada ya gazeti hilo kuchapisha hivyo ndipo aliyekuwa Waziri wa Mambo
ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Ahmed Hassan Diria,
alipokanusha na kusema kwamba kama Zanzibar imefanya hivyo imekiuka
Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Kwa mara nyingine tena gazeti hilo katika toleo la kwanza la mwezi
Januari 1993 lilichapisha habari kuwa Tanzania ilikuwa mwanachama wa
siri wa Shirika la Kiislam la Afrika (IAO). Gazeti hilo pia
lilichapisha maazimio ambayo yalidaiwa yalipitishwa na kikao cha
mwanzo cha IAO mjini Abuja, Nigeria, maazimio ambayo kwa Watanzania
wengi yalionekana kuwa ya kutisha kwa usalama na utangamano wa jamii
ya Kitanzania.

Katika kipindi hicho hicho gazeti lingine lilichapisha makala ambayo
yalionyesha kwamba ni kweli Zanzibar ilikuwa imejiunga na OIC licha ya
Waziri Diria kukanusha. Mpaka wakati huo, mbali ya taarifa ya Waziri
Diria hakuna taarifa nyingine iliyotolewa na ama Serikali ya Zanzibar
au Serikali ya Muungano kukanusha au kuthibitisha madai ya magazeti
hayo mawili.

Lakini mnamo Januari 9, 1993 taarifa ilitolewa na Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar kuthibitisha uanachama wake katika OIC. Katika
taarifa hiyo ilionekana wazi kuwa Serikali ya Muungano ilikuwa na
habari na suala la Zanzibar na OIC.

Matukio haya yalizua mambo matatu. Kwanza ni kutaka kujua kama kweli
Zanzibar kujiunga na OIC ni kinyume na Katiba hasa kwa kuzingatia
maadili ya siasa za Tanzania tangu uhuru na Katiba ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania inayosema kuwa shughuli zote za dini zitafanywa
nje ya mamlaka ya nchi.

Pili madai kuwa Tanzania ilikuwa mwanachama wa siri wa IAO na
kuzingatia maazimio yaliyodaiwa kuwa ni ya IAO, wananchi wengi
waliingiwa na hofu na kuzusha minong'ono katika sehemu mbalimbali za
nchi yetu. Tatu, ilionekana kuwa kuhusika kwa nchi yetu katika
mashirika hayo mawili kulikuwa kwa siri na hivyo kuzusha hisia kwamba
huenda malengo na madhumuni yake hayakuwa mazuri.

Mimi nikiwa mbunge nilipoyapata haya yote sikujua lipi ni la kweli na
lipi si la kweli. Nilishindwa kujua kama taarifa ya Waziri Diria
ilikuwa sahihi au taarifa kutoka Zanzibar ndiyo iliyokuwa sahihi. Mimi
kama Watanzania wengi walivyokuwa wakati huo, sikujua kama IAO ipo au
haipo na kama maazimio yaliyotajwa ni ya kweli au si ya kweli.

Watanzania wengi walijikuta katika hali hiyo na kitu ambacho
kingeondoa tatizo hili katika mawazo yao ingekuwa ni taarifa ya
Serikali ya Muungano wa Tanzania. Nikiwa mbunge na kiongozi, nilikuwa
na njia mbili za kufuata. Moja ni kujiunga na vikundi
vinavyonung'unika na hivyo kuwa mmojawapo wa wapika majungu na kueneza
fikra potofu zisizo na msingi.

Pili, kufuata taratibu zilizopo ili kupata ukweli wa mambo ulivyo na
kuwaondoa wasiwasi wananchi.

Kama mbunge taratibu ninazoweza kufuata ni za kibunge, sina njia
nyingine. Mbunge akitaka kupata ukweli wa jambo lolote zito
lililotendwa na serikali hana budi kutumia Bunge lenyewe ambalo lina
uhalali wa kikatiba kupata majibu sahihi kutoka serikalini. Lazima
ikumbukwe kwamba kwa muundo wake serikali ni chombo kizito, chenye
maguvu na usiri mwingi katika utendaji wake wa kazi.

Serikali haina msimamizi isipokuwa watu wenyewe kupitia wawakilishi
wao bungeni. Bunge ndicho chombo pekee cha wananchi kilichopewa
madaraka na Katiba ya Nchi kuisimamia, kuihoji na inapobidi,
kuichunguza na hata kuiwajibisha serikali katika vitendo vyake.
Zanzibar kujiunga na OIC na tuhuma kwamba Serikali ya Tanzania ni
mwanachama wa IAO, vilidaiwa kutendwa na serikali na kwa hiyo chombo
halali cha kulichunguza na kuhoji suala hili ni Bunge.

Kwa misingi iliyoelezwa hapo juu mimi sikubaliani na wale wote
wanaodai kuwa Bunge la Tanzania halina haki ya kuchunguza suala la
uanachama wa Zanzibar katika OIC,wala tuhuma kwamba Tanzania ni
mwanachama wa siri wa IAO. Ninaamini hatua zilizochukuliwa na Bunge
zilikuwa halali na haki, sahihi na zenye manufaa kwa taifa hili hasa
ukitilia maanani jinsi masuala hayo mawili yalivyozusha hisia tofauti
baina ya Watanzania.

Hoja kwamba Bunge halina uwezo wa kuhoji wala kuchunguza masuala ya
kikatiba yanayohusu Muungano na yale yanayohusu uanachama wa Zanzibar
katika OIC ni potofu na haiwezi kukubaliwa. Wananchi lazima waikatae
hoja hiyo kwa sababu ina malengo ambayo si mazuri.

Katika nchi ya kidemokrasia serikali huwekwa madarakani na watu, na
watu ndio ambao huisimamia serikali hiyo kupitia Bunge. Madaraka ya
watu juu ya serikali hujitokeza katika sura mbili. Sura ya kwanza ni
wakati wa kupiga kura kumchagua Rais na wabunge, na sura ya pili ni
madaraka wanayokuwa nayo wabunge kwa niaba ya watu juu ya serikali
kati ya vipindi vya uchaguzi.

Bunge ndiyo kielelezo cha madaraka ya watu ndani ya nchi yao kwa
masuala yote yanayowahusu.

Kwa hiyo kiongozi yeyote anayelikataa Bunge maana yake anakataa
madaraka ya watu juu ya serikali yao. Kiongozi kama huyo anataka
kutawala bila kuwepo na chombo cha kumhoji anapopotoka. Kwa kifupi
kiongozi kama huyo anataka kuleta udikteta jambo ambalo Watanzania
lazima walikatae.

Kuhusu matamshi kutoka viongozi wa Zanzibar kwamba Bunge halina uwezo
wa kutamka kuwa Zanzibar imekosea katika jambo fulani na kwamba si
chombo chenye uwezo wa kutamka hivyo, usemi huu si kweli. Bunge lina
madaraka na uwezo juu ya Zanzibar katika masuala yote ambayo ni ya
Muungano, na ndio maana wabunge wake wanatoka pande zote mbili za
Muungano.

Kuwepo kwa wabunge wa Zanzibar katika Bunge la Muungano kunalipa
uhalali Bunge kushughulikia masuala yote ya Muungano popote Tanzania.

Zanzibar kujiunga na OIC ni suala la kikatiba na masuala ya Katiba ni
masuala ya Muungano. Kwa hiyo, Bunge kujishughulisha na suala la
uhalali wa Zanzibar kujiunga na OIC si nje ya madaraka yake. Unaposema
Bunge halina uwezo juu ya Zanzibar hata katika mambo ya Muungano ina
maana kuwa Muungano haupo, jambo ambalo si kweli – kisheria (dejure).

Mahakama ya Katiba inahusika pale inapotokea mgogoro wa tafsiri wa
vipengele vya Katiba baina ya pande mbili za Muungano. Kwa mfano,
Zanzibar walipoomba kutoka Serikali ya Muungano ruhusa ya kujiunga na
OIC, wangesubiri kupata jibu.

Kama Serikali ya Muungano ingewakataza kwa kutumia vipengele vya
Katiba ambavyo Zanzibar wanafikiri haviwazuii kufanya hivyo, basi
mgogoro wa kikatiba ungelikuwa umezuka na Mahakama ya Katiba ingeombwa
kutoa tafsiri sahihi ya vipengele hivyo. Na Katiba hiyo lazima iwe
Katiba ya Jamhuri ya Muungano, siyo ile ya Zanzibar.

Kuwepo kwa Mahakama ya Katiba kushughulikia tofauti za tafsiri ya
vipengele vya Katiba kati ya Bara na Zanzibar hakulizuii Bunge
kushughulikia ukiukwaji mwingine wowote wa Katiba unaoweza kufanywa na
Serikali ya Muungano au ya Zanzibar. Ni vizuri Bunge likashughulikia
suala la kulinda Katiba, vinginevyo tutakuwa na Katiba ambayo
inafuatwa tu pale inapokubaliana na matakwa ya viongozi na kukiukwa
pale inapowazuia kutekeleza matakwa yao.

Jambo jingine ambalo limeulizwa na baadhi ya wananchi na ambalo
ningependa kutoa maelezo ni lile linalouliza kwamba ilikuaje Naibu
Spika kuwapata haraka haraka wabunge saba kuja Dare es Salaam kutia
saini waraka uliofikishwa kwake wakati Bunge lilikuwa halikutani?

Ukweli ni kwamba hakuna mbunge aliyeitwa na Naibu Spika (Pius Msekwa)
kuja Dar es Salaam kushughulikia suala hili. Wabunge wote saba
walikuwepo Dar es Salaam kuhudhuria mikutano ya kamati mbalimbali za
Bunge. Na zaidi ya hayo Naibu Spika hakututaka tuandike bali
tuliandika kwa kujituma wenyewe.

Bado kuna baadhi ya wananchi ambao waliuliza kwa nini mara baada tu ya
kuwasilisha waraka wetu kwa Naibu Spika tukatangaza suala hili kwa
waandishi wa habari. Kuna sababu tatu za msingi ambazo zilitufanya
tutangaze hatua tulizochukua. Kwanza, mbunge ni mwakilishi wa watu na
hivyo yote anayoyafanya kwa wadhifa wake kama mbunge lazima yajulikane
kwa wananchi anao wawakilisha.

Pili, suala la uanachama wa Zanzibar katika OIC na tuhuma kwamba
Tanzania ni mwanachama wa IAO yaliwagusa watu wengi na wote katika
kipindi hicho walisubiri kuona hatua gani inachukuliwa na nani. Kwa
hiyo tulipenda kuwajulisha wananchi kwamba Bunge lao lilikuwa
linachukua hatua za kupata ukweli wa mambo hayo.

Tatu, hatua ya kutaka uchunguzi ufanywe juu ya masuala hayo mawili
ilichukuliwa na wabunge saba na tukaomba matokeo ya uchunguzi huo
yafikishwe bungeni Dodoma katika kikao cha Februari, 1993. Kwa
kulitangaza jambo hili tulikusudia liwafikie wabunge wote popote
walipokuwepo ili wajiandae na hata kufanya mawasiliano na wananchi
wanaowawakilisha kabla ya kufika Dodoma.

Kabla ya kumaliza maelezo haya nataka nigusie kidogo hisia
zilizojitokeza kuonyesha kwamba uchunguzi wa masuala ya OIC na IAO
ulianzishwa kwa vile tu mambo hayo yana uhusiano na dini ya Kiislam.

Hapa ningependa kuwahahakishia waumini wa dini hiyo na Waanzania wote
kwa ujumla kwamba sisi wabunge saba katika kuomba uchunguzi ufanywe
katika masuala haya mawili hatukuwa na nia yoyote mbaya na dini ya
Kiislam. Hatukuwa na chuki wala uhasama wa aina yoyote ile.

Madhumuni yetu ilikuwa ni kupata ukweli wa mambo hayo na kuona kama
Katiba ya nchi haikuwa imekiukwa. Mimi (nina amini na wenzangu wana
msimamo kama huo), siwezi kutumia wadhifa wangu kukandamiza au
kupendelea dini moja dhidi ya dini nyingine.

Msimamo wangu ni kuyaacha masuala ya dini kwa wale wanaoamini na wala
serikali isijiingize katika kuendeleza imani ya dini moja dhidi ya
imani nyingine. Ingawa katika gazeti moja la Januari 21, 1993
nilitajwa kuwa mimi ni mchungaji wa kanisa, nataka kutumia nafasi hii
kukanusha kwamba mimi si mchungaji wala padre wa kanisa.

Katika maisha yangu mimi sijawahi kushika wadhifa wowote katika kanisa
wala katika dini nyingine yoyote. Aliyenitangaza kwamba mimi ni
mchungaji alifanya hivyo kwa madhumuni yake binafsi.
Endelea Kuhabarika

Zanzibar: Kwa kujitangaza nchi, imekiuka katiba ya Muungano?

Makala/Source: Gazeti la Raia Mwema
 
Hapo naona umeufyata, inabidi ujichekeshe tu, unalo?

Wewe lazima utakuwa na nyegemshindo ndiyo maana kila wakati kimkia chako kinarukaruka huku na kule wanaume wanapoongea. Kufyata kuhusu nini sasa? Mwalimu wako ameleta hapa copy ya ID as a member of Library of congress?? (Almost all the phones have cameras now) Au je kuwa member of library of congress au kitabu chako kuwa mle ni ushahidi wa kuwa uliyoaandika kwenye kitabu chako ni facts? Ndiyo maana nikasema haya mambo muendelee kudanganyana huko huko bongo!! tatizzo mwalimu wako akiishiwa hoja lazima aanze tambo na tatizo ya tambo hizo, nyingi hazina ukweli wowote ila hutumika kutishia hadhira anayoongea nayo kuonyesha eti ni jinsi gani yeye alivyo mahiri. Bahati mbaya hapa JF si hivyo, no stone will remain unturned.

 

Hivi wewe unajiona kuja humu kudai ID ndio umekuja na hoja ya maana? Hivyo ndio wewe unathibitisha Kichwa cha habari? Ndio ushahidi wako ulioleta kumsaidia mgala mwenzako? Afanaaleik!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…