Nguruvi,
Hukumu umesema wewe mie siwezi wala sina uwezo wa kuwa hakimu wa Allah.
Kuhusu kuwasemea Waislam ni kwa kuwa wewe huwajui Waislam.
Ungetujua basi ungeijua nafasi yangu katika umma.
Ijumaa iliyopita nilialikwa kuzungumza katika moja ya misikiti mikubwa
Dar es Salaam.
Katika kila msikiti kila taasisi ya Kiislam ukiondoa BAKWATA ya utakuta
maandishi yangu au DVD.
Kila hafla ya Kiislam naalikwa na Waislam wananiweka kukaa kinarani.
Unataka ushahidi gani zaidi ya huu?
Waislam wanawajua wazushi, waongo nk. nk.
Ningekuwa katika hao nisingekuwa miongoni mwao na kila siku namuomba
Allah hatma njema.
Mfano wa waja wema ndiyo huu leo Sheikh Hassan bin Amir anakumbukwa
na kurehemewa kila msikiti na maadui zake wanalaniwa.
Sawa sawa kabisa! na wala kualikwa si kosa tena ni jambo jema kabisa lakini hilo halijawa idhni ya wewe kuongea maoni yako kwa niaba ya Waislam.
Waislam wakikubali hilo basi wakubali na la Ilunga kuwa msemaji wao kama ilivyo katika DVD.
Wamkubali Ponda n.k. Hawa tunajua ni wachumia tumbo kwanini wao wawe ndio Uislam?
Mohamed, waacheni waislam na waumini wafanye yenye neema kwao kwa kutumia mafunzo, hadithi na suna ikiwa ni pamoja na matumizi bora ya akili zao bila ghilba, kurubuniwa au kupotoshwa. Waacheni waislam waisome na kuitumikia dini yao kwa mujibu wa maamrisho ya Allah na si kwa mujibu wa maoni, fikra, hekaya, ngano na riwaya za binadamu.
Na hakika watakusikiliza sana kwasababu maneno yako ni matamu! Utawaambia kuhusu mfumo kristo na utafiti wa Warsha uliobaini madudu wizara ya elimu na kisa cha wanafunzi kutochaguliwa vyuo vya elimu ya juu.
Hutawaeleza kuwa utafiti wa warsha ulilenga vyuo vikuu huku kukiwa na tatizo kubwa chini.
Hutawaeleza kuwa shule zikifungwa Kilwa kwa kukosa wanafunzi huo ndio mwanzo wa kukosa wanafunzi.
Hutawaeleza kuwa tafiti za Warsha hazikulenga na kufuata kanuni za utafiti zimeeleza hali iliyopo.
Utafiti wa warsha haukutafuta chanzo na suluhu umeegemea kutafuta sababu.
Ndio maana nimekuuliza, hivi kuna utafiti gani uliowahi kufanywa na kubaini kuwa katika elimu ya awali, msingi na sekondari mambo ni mazuri isipokuwa elimu ya juu! Hilo umeshindwa kulijibu, that's ok, na ndicho ambacho hutaulizwa huko uendako bali utasikilizwa.
Kuna kitu kinaitwa escapism, yaani kutafuta sababu za faraja katika dhiki na mahangaiko.
Kwa mfano, mtu wa mtaani hana pesa kwa kipato kidogo, basi anaamua kujiliwaza kwa kunywa pombe sana na kutafuta kibinti cha kupooza machungu. Mtu huyo wa mtaani hajui kuwa hapo ndipo anapokwepa tatizo na akirudi nyumbani lipo pale pale tena limeongezeka.
Leo mkuu wa NECTA akiwa mwislam kama ilivyowahi kutokea kwa Rais, makamu na mawaziri tena wa elimu hali itabaki kuwa ilivyo kwasababu tatizo si viongozi tatizo lipo katika grassroot level.
Haiwezekani shule iwe na wanafunzi 250 na walimu wawili halafu wafeli useme ni Necta! Haiwezekani hujuma ifanyike kwa Hussein Bin Kherefu imwache Gugurito kibindinginya!
Hivi mfumokristo unahujumu vipi wananfunzi wa darasa moja ambao Johm William anapata division na Mariam Muhsin division 2 shule na darsa hilo?
Hivi uonevu upo wapi FEZA sekondari wafaulishe zaidi ya Morogor, Ikizu au Makoko seminary?
Hivi kwanini Mwantumu Ramadhan Husein Mohamed aongoze kutoka Marian Seminary(katoliki) tena kitaifa mfumo huo umwache.
Hivi ilikuwaje kati ya 1993-1995(kama nipo sawa) Alharamani sekondari itoe wanafunzi 3/4 ya darasa la Chuo kikuu?
Tena kati ya hao robo wamefanya masters na wengine PhD! Huu mfumo uliwaacha vipi yarabi wakavuka viunzi hivyo?
Nini kilitokea kwa mwalim Mzige? Je, kuna utafiti wa kwanini Alharamaini waliweza na sasa wameshindwa?
Kwanini watoto w vigogo wa kiislam wanasoma kule kwa masista Morogoro!
Kwanini Kilwa iliyokuwa iwe ''Capital'' ya nchi hii ipo katika hali iliyokuwepo, wakati huo huo Iramba na Kondoa wanapiga hatua?
Kwanini mfumo haukuathiri Machame, Mwanga na Same, Bukoba na Muleba!
Je, waislam walitumia fursa zilizokuwepo kwa namna njema au ndio walitumbukia katika ''ukafir''
Na mwisho mfumokristo unawaathiri vipi wenyeji wangu wa Kivinje na Masoko hadi kufikia mahali wameacha watoto wakimbie shule na zifungwe!
Kwanini shule za Mashia na Ismaili zifanye vema huku za waswahili wengine zihujumiwe! huu mfumo unatumia software gani na ya mwaka gani katika kutekeleza majukumu ya dhulma na Inda, husda na fitna dhidi ya waislam.
Kuna lot of basic things huwaelezi watu wako kwasababu wanataka kusikia wanachokipenda na si kile unachotaka kuwaambia. Nawe unatumia udhaifu huo huo wa kuwaaambia wanachotaka kusikia na si kile wanachopaswa kufanywa.
Narudia ESCAPISM kwa kutumia ukristo, mfumo ukristo, serikali, sisi dhidi yao, tumeleta uhuru n.k. havitatoa jibu la tatizo.
Jibu la tatizo litapatikana pale tu hii tabia ya ''cheating and deceiving' itakapokoma.
Pale state of denial itakapopata matibabu na pale upendo utakapotangulia chuki, husda, fitna na uzushi.