Shekh Mohamed Said, napata matumaini unapoelezea fitna na chuki za Mfumo Kristo Alla akupe kila la kheri! pia naomba unimalizie yale ya Wapigania uhuru wa huku Moshi ambao wengi ni Waislamu kama wameingia ktk historia ya nchi hii! Kwa sababu mwaka 1991 ulimuhoji kaka angu Al marhum Mfoi na rafiki yake Mackenga ktk nyumba ya Shekh Salim hapo Lumumba Dar juu ya kadhia ya kuuzwa jumba la Wakfu na Bakwata!
Marehemu na mwenzake walikuja ktk Mkutano mkubwa wa Waislamu chuo kikuu Dar mwaka 1991 kujadili hatima ya Bakwata na wewe uliwahoji pia kuhusu Wazee wapigania uhuru wa Moshi akina Yusuf A. Olotu, Mariamu Baiskeli, Halima Selengia, Mfaume Kimario, Lucy Lameck nk!
Sasa kwa kuwa sina kitabu chako ulichoandika, naomba unijuze kama na wao umewataja ktk kitabu chako na kama bado basi nakuomba na hao na wengine wa mikoa yote nao tuwakumbuke ktk dua zetu!
Na kuhusu Jina la Amri Abeid ulilolitaja ktk makala yako, huyu alikuwa nani? Kumbuka uwanja wa Mpira wa Arusha una jina lake yaani Shekh Amri Abeid!
Na jee, kuna ukweli wowote kuwa Nyerere alitaifisha nyumba za Watu 1967 kupitia azimio la Arusha kwa sababu za udini? inasemwa kuwa nyumba nyingi zilizotaifishwa zilikuwa za Waislamu wenye asili za Asia ni kweli?