Sio UDINI tu. Na Ukabila, ubaguzi wa rangi, hatukuwa na TAIFA. Tulikuwa na NCHI. Mwalimu alipambana navyo hivi tangu kabla ya uhuru. Unakumbuka ule mkutano wa TANU wa kura tatu mwaka 1958 kule Tabora? Unaijua AMNUT na ANC ya Mtemvu ilivyoanza?
Baada ya uhuru haya mambo yaliendelea kujitokeza kwa sura na mienendo tofauti. Mwalimu hakuwa na msamaha wala mswalie Mtume( S.A.W) kwa hilo. Jeshini tunaambiwa hakuangalia makunyanzi au hadhi ya mtu, taasisi au kikundi cha watu. Akafuta UCHIFU, akafuta EAMWS, akawatia ndani baadhi ya Masheikh na wazee wachochezi. Jitihada hizi za kuliweka TAIFA pamoja ndizo zimezaa kitabu cha Mzee Mohamed. Kaandika waliosahaulika, kaandika UISLAM ulivyopigania uhuru wa nchi hii ingawa hiyo sio kazi ya DINI yoyote!