Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Yericko Nyerere,

Unataka kutuambia kabla ya Nyerere kuwa rais Tanganyika kulikuwa na udini.
Sio UDINI tu. Na Ukabila, ubaguzi wa rangi, hatukuwa na TAIFA. Tulikuwa na NCHI. Mwalimu alipambana navyo hivi tangu kabla ya uhuru. Unakumbuka ule mkutano wa TANU wa kura tatu mwaka 1958 kule Tabora? Unaijua AMNUT na ANC ya Mtemvu ilivyoanza?

Baada ya uhuru haya mambo yaliendelea kujitokeza kwa sura na mienendo tofauti. Mwalimu hakuwa na msamaha wala mswalie Mtume( S.A.W) kwa hilo. Jeshini tunaambiwa hakuangalia makunyanzi au hadhi ya mtu, taasisi au kikundi cha watu. Akafuta UCHIFU, akafuta EAMWS, akawatia ndani baadhi ya Masheikh na wazee wachochezi. Jitihada hizi za kuliweka TAIFA pamoja ndizo zimezaa kitabu cha Mzee Mohamed. Kaandika waliosahaulika, kaandika UISLAM ulivyopigania uhuru wa nchi hii ingawa hiyo sio kazi ya DINI yoyote!
 
Majibu ya Mohamed Said sio mwarobaini wa historia yetu,Maono na mchango ya wadau hapa inamafaa zaidi kuliko kusubiri ngano za Mohamed Said,Watanzania wengi sasa wamefunguka na kuelewa kuwa kumbe walirubuniwa na Mohamed Said hivyo sasa wanahitaji fikra mpya ambazo ndizo tunazowalisha hapa mimi, wewe na wale,Hawahitaji sana majibu ya Shehe Mohamed Said bali yeye kama sehemu ya kutetea ngano zake na aje na hayo majibu hapa hapa!
Siyo na kivukoni? historia ilianzia kwa nyerere ikaishia kwa nyerere, wewe ndiyo hiyo unaiona ya maana? Hapa imesambaratishwa vibaya sana. Inawauma lakini ndio yakini, kuna yakini ikafutwa na uongo? Haiyumkini kabisa.
 
mbona jibu ni ndiop; au hujamsoma mzee Said akikusimulia jinsi baadhi ya wazee wake walivyokuwa wadini? Au unafikiri mgogoro wa uchaguzi wa 1958 hadi ukaigawa TANU ulitokana na nini?

MM,

Ukweli udini ulianza 1953 Nyerere alipochukua uongozi wa TAA.
Nimeeleza vizuri katika kitabu.

Ilipofika 1955 tatizo likawa kubwa ndani ya TANU hapo
ndipo Sheikh Hassan bin Amir alipoitisha mkutano na kupiga
marufuku udini katika TANU.

Tatizo hili halikuibuka tena hadi 1958 katika Uchaguzi wa Kura
Tatu.

Waislam wakalipiga tena vita na hata AMNUT ilipoasisiwa haikuweza
kupata uungwaji mkono na Waislam.

Matokeo yake ikawa haina nguvu hadi ikapigwa marufuku 1965 baada
ya kupitishwa sheria ya chama kimoja.
 
Nlisema uko kama kipepeo.. unaruka ruka kila ukikamatwa unakimbilia kwingine. Kama hakuna ushahidi wowote wa Nyerere kuagiza lolote au kusema lolote dhidi ya Uislamu na Waislamu wewe unapata wapi ujasiri wa kusema alikuwa anapiga vita Uislamu?

Hitler alipoamua kuwaua Wayahudi na kutafuta ile "final solution" hakujificha. Lakini angeonekana kama kituko kweli kama wakati huo huo anasema wayahudi ni kansa ya dunia halafu anawapa madaraka, anawaachia uongozi na kula na kunywa nao. Ahmedinajad naye anapowapiga vita Wayahudi hawapigi kwa kificho. Verwoerd na sera yake ya Ubaguzi wa rangi hakufanya hivyo kwa kificho. Angekuwa mnafiki wakati huo huo akitukuza watu weupe halafu awape nafasi na madaraka kwenye serikali yake watu duni - weusi.

Nyerere hajawahi kuwa na njama dhidi ya Uislamu au Waislamu. Asingeweza kuwa hivyo na wakati huo huo kuamini maisha yake mikononi mwao. Ushahidi wa hili ni kitabu chako cha Abdulwahid Sykes. Ni katika kitabu hiki umeweza kwa umahiri mkubwa kumuonesha kuwa Nyerere tangu kabla ya Uhuru na baada ya Uhuru amekuwa ni rafiki wa Waislamu. Hajawahi kusema neno baya kuhusu Uislamu (angalau hakuna ushahidi wowote juu ya hilo) wala dhidi ya Waislamu.

NONE.

Na hata kwa wale unaowaita wazee wako hutampata hata mmoja ambaye anaweza kukuambia aliwahi kumsikia Nyerere akiulalamikia Uislamu au akisema maneno ya kejeli dhidi ya Waislamu waliokuwa wanamzunguka. NONE.

Utarukaruka tu kama kipepeo lakini mwisho utatua tu na itabidi ukubali ukweli wa historia tu.
Yeyote anayesoma Biblia na kuamini yaliyomo kuwa yote ni kweli hashangazi kutamka maneno kama yako.Yaani maandiko yote yanaonesha kuwa Yesu hakuwa Mungu na bado wao wanasema alikuwa.
Matendo ya Nyerere yanaonesha alikuwa akipiga vita uislamu na hata wakristo wenye hekima wameliona hilo lakini bado wako wengi wanasubiri mpaka itokee pahala Nyerere aseme Leo naupiga vita uislamu ndipo watu hao waone ni ushahidi kuwa Nyerere kweli alikuwa adui wa uislamu.Ile kuifunga EAMWS na kuwatimua masheikh kwenye TANU haitoshi kwao.
Asingeweza kusema hivyo wakati akijua watu wenye akili kuliko zake akina Abdulwahid Sykes wapo.
 
Hivi ndugu yangu unamatatizo ya AKILI?

Mada nzima nimeieleza kwa kirefu nikihusisha ukoloni wa Kijerumani na ukoloni msonge wa Kiingereza lakini kumbe wewe upo ahera kabisa?

Unakosa kusoma mada nzima kwakuwa unatawaliwa kwa hisia na ushabiki katika mada hii,

Tuliza moyo,akili na mwili wako anza upya kuisoma makala hapo juu utaona tunachokijadili tangu 12/01/2013 mpaka leo hii!

Bahati nzuri tumeisha kuzoea kwa kaul zako wala utupi shida tena.

Wewe upande wa histori ya Tanganyika ni mtupu sana, unasema Oscar Kambona alikuwa ni mwanachama wa kawaida tu wakati yupo TANU.

Hujui alikuwa na cheo gani ndani ya chama halafu unasema unajua historia ya Tanganyika.
 
WC,

Sidhani kama tunachogombania ni uaisi wa TANU na Nyerere.

Mimi ninachosema ni kuwa historia ya TANU na kuasisiwa kwake
ikiwa utaanza na kuishia hapo utakuwa umepunjika pakubwa.

Historia ya TANU haikuanza pale New Street tarehe 7 Julai 1954.

Historia ya TANU imeanza 1929 kwa kuanzishwa kwa African
Association.

Hili tumejadili kwa kirefu sana.
Lakini sidhani kama hili ni jambo kubwsa sana kwa sasa.

Historia rasmi ya Kivukoni imechukuliwa kama ndiyo ukweli wa historia
ya TANU.

Hapana ugomvi.

Ila ipo historia hii ambayo mimi nimeandika na kwa sasa ni mashuhuri sana.
Watu wana haki ya kuamua ipi wanaiamini.
TANU haikuwepo mwaka 1929 kama ambavyo TANGANYIKA haikuwepo kabla ya vita kuu ya kwanza ya dunia kumalizika mwaka 1918. Wewe unalazimisha iwe hivo ili kuwa-accomodate wazee wako hawa! Hiyo ndio Mzee Mwanakijiji anaita HISTOHISIA!

Sasa hivi TANU haipo na CCM hii ya akina Jakaya sio TANU kabisaa.
 
Last edited by a moderator:
Mbona hawakufikishwa mahakamani hata wale wengine waliofikishwa mahakamani kwa kutaka kuipindua serikali ya Nyerere walishinda kesi lakini Nyerere alitoa amri wakamatwe tena. Mwenye heri anakuwa na shari.

Hizi ndizo porojo za mitaani..alitoa amri hiyo lini na wapi?
 
Pitia pitia kwenye nyuzi tumeshaomba huo mdahalo lakini mpaka sasa watu kimya. Umechelewa jamvini Karatu imeshaliwa.

Ule Matola aloingia mitini mara ooh mama mgonjwa. Mara ooh nna simu mtandao mbaya. Kwi kwi kwi teh teh teh.

Mohamed Said kisha sema hayupo hapa kujibu maswali tena hususan yale yasio na tija.

Jee, ulikuwa unamjuwa Mshume kabla ya kumsoma Mohamed Said?
Zomba bana sasa majibu ya Copy & paste uliyokuwa unayaleta wewe ndio mdahalo? tulipewa maswali ili tujiandae sasa yale yaliobaki nikaona huna uwezo wa kujibu hata moja, ndio maana nikaona niendelee na ratiba zangu zingine kuliko kupoteza muda.
 
MM,

Ukweli udini ulianza 1953 Nyerere alipochukua uongozi wa TAA.
Nimeeleza vizuri katika kitabu.

Ilipofika 1955 tatizo likawa kubwa ndani ya TANU hapo
ndipo Sheikh Hassan bin Amir alipoitisha mkutano na kupiga
marufuku udini katika TANU.

Tatizo hili halikuibuka tena hadi 1958 katika Uchaguzi wa Kura
Tatu.

Waislam wakalipiga tena vita na hata AMNUT ilipoasisiwa haikuweza
kupata uungwaji mkono na Waislam.

Matokeo yake ikawa haina nguvu hadi ikapigwa marufuku 1965 baada
ya kupitishwa sheria ya chama kimoja.


Una maana kuliuwa na Waislamu wenye udini dhidi ya Wakristu tangu 1953 na wakarudi tena 1955 na tena hawahawa na udini wao wakarudi tena 1958 ?
 
Yericko,

Wewe baba yako ndiye Baba wa Taifa na ndiye muasisi wa TANU.
Tuandikie kitabu vipi aliasisi TANU.

Hii itafuta ''ngano'' za Mohamed Said.

Utakuwa umetufanyia ihsani kubwa sana.

Kitabu tayari kipo cha Kivukoni hata kabla ya hicho cha ngano zako mkuu,

Kinatakiwa kuhuishwa kidoggo tu kwa yale yaliyosahaulika tu
 
Mkuu zomba ule mdahalo wenu na mkuu Matola ulishindwa vibaya sana kibaya zaidi ulikuwa ukifanya kazi ya kucopy na kupaste kama ni mark wewe ulipata 25% na Matola 87%.Mwenzako ana A wewe D Haha ha ha ha ha.

Pitia pitia kwenye nyuzi tumeshaomba huo mdahalo lakini mpaka sasa watu kimya. Umechelewa jamvini Karatu imeshaliwa.

Ule Matola aloingia mitini mara ooh mama mgonjwa. Mara ooh nna simu mtandao mbaya. Kwi kwi kwi teh teh teh.

Mohamed Said kisha sema hayupo hapa kujibu maswali tena hususan yale yasio na tija.

Jee, ulikuwa unamjuwa Mshume kabla ya kumsoma Mohamed Said?
 
Last edited by a moderator:
Wakuu pg # 258 Mohamed Said kashindwa kutoa majibu kila tukimuuliza maswali rahisi kabisa anayakwepa sasa sijui tuwaombe Mods waandae mdahalo kama ule wa Matola na zomba labda tunaweza kupata majibu tunayotarajia vinginevyo sioni sababu ya kuendelea na huu mnakasha.

Mods mnaweza pia kuandaa utaratibu kama mlivyofanya kwa mheshimiwa Zitto Kabwe .

Nakala Invisible Paw ....

Mkuu Ngongo,

Tatizo siyo Mohamed Said hebu soma kichwa cha habari cha huu uzi watu ndiyo watatakiwa wathibitishe uchochezi wa Mohamed Said.
 
Last edited by a moderator:
Bahati nzuri tumeisha kuzoea kwa kaul zako wala utupi shida tena.

Wewe upande wa histori ya Tanganyika ni mtupu sana, unasema Oscar Kambona alikuwa ni mwanachama wa kawaida tu wakati yupo TANU.

Hujui alikuwa na cheo gani ndani ya chama halafu unasema unajua historia ya Tanganyika.

Nisome kwaumakini katika maandiko yangu mkuu,

Nimesema alikuwa mwanachama wakawaida nikipinga dhana ya nyinyi utaka awe sehemu ya waasisi wa TANU.

Ikiwa mnataka mchango wake uthaminiwe siwaelewi mnataka uthaminiweje?

Je kila mwanatanu aandikwe kwenye historia ya UHURU?
 
Yericko,

Wewe baba yako ndiye Baba wa Taifa na ndiye muasisi wa TANU.
Tuandikie kitabu vipi aliasisi TANU.

Hii itafuta ''ngano'' za Mohamed Said.

Utakuwa umetufanyia ihsani kubwa sana.

Anapo pakuanzia?
 
Sana sana huku unasaidiwa ili usiendelee kupumbaza wenye elimu finyu ila hakuna anayeruka ruka na uzushi uliouandika. Kama lengo lako lilikuwa ni hilo, tunakupuuza tu wewe na maandishi yako then tunasonga mbele.

Mkirua,

Si kama nasema kwa kujisifu ila naeleza mambo ambayo nina hakika
huyajui.

Si rahisi kukipuuza kitabu changu wala maneno yangu ninapoandika
au kuhadhir.

Ingekuwa upo uwezekano wa kunipuuza views hapa JF zisingefika
51,000 +.

Zimegonga kiasi hicho kwa kuwa nisemayo ni mambo mazito ambayo
si wengi walikuwa wanayajua.

Siku moja niko Msikiti wa Manyema baada ya sala ya Ijumaa.

Mara kanijia mheshimwa mmoja Muislam akanisalimu na akaniuliza,
''Wewe ndiye Mohamed Said unaeandika katika Africa Events?''

Akanambia, ''Tumekuzungumza katika Halmashauri Kuu ya CCM
kuna mjumbe kamlalamikia Mwenyekiti kuwa kuna watu wanajaribu kupotosha
historia ya TANU. Hamu yangu ilikuwa kukufahamu nimekuulizia hadi
nimekupata.''

Miaka mingi imepita.
Kitabu nimeandika huu mwaka wa 15 na tunakwenda toleo la tatu.

Haijawezekana mimi ''kupuuzwa na maandishi yangu na kusonga mbele.''
Ingekuwa inawezekana wewe ndiyo ungetoa mfano.

Wewe ungekuwa wa kwanza kunipuuza.
Ungesoma ukanipuuza kwa kukaa kimya.

Ibra kubwa ya kitabu hiki ni kuwa ukikisoma lazima maswali mengi yatakuja
kichwani kwako.
 
Mkuu zomba ule mdahalo wenu na mkuu Matola ulishindwa vibaya sana kibaya zaidi ulikuwa ukifanya kazi ya kucopy na kupaste kama ni mark wewe ulipata 25% na Matola 87%.Mwenzako ana A wewe D Haha ha ha ha ha.

Ahsante Mwalim , aliyekimbia kashinda. NECTA ni hivyohivyo kama wewe.

Ulitaka niwape takwimu za uhakika bila ku copy na ku paste au sio?
 
Anapo pakuanzia?

Zomba,

Pako pa kuanzia.

Anaweza kuanza Nyerere alipokikuta chama cha TAA kiko hoi hakina
mwelekeo wa siasa...

Hii ni ''cue'' maarufu akina Mzee Ngombale wako atawahoji wao wana
mengi.

Ataingia katika nyaraka za mzee wake na atazungumza na mama.
Sifanyi maskhara kweli Yericko anawezakuja na kitu cha maana sana.
 
Zomba bana sasa majibu ya Copy & paste uliyokuwa unayaleta wewe ndio mdahalo? tulipewa maswali ili tujiandae sasa yale yaliobaki nikaona huna uwezo wa kujibu hata moja, ndio maana nikaona niendelee na ratiba zangu zingine kuliko kupoteza muda.

Na ndio ukasingizia mama mgonjwa kalazwa, simu mbovu haina chaji. Umesahau?
 
Patamu hapo. Yepi yaliosahaulika? tukumbushe.

Zomba,

Wewe ulitaka kumkatisha tamaa si unaona tayari keshaanza ''literature review.''
Tayari atakipitia kitabu cha Kivukoni na kuangalia yalosahaulika.

Huu ni mwanzo mzuri sana.
 
Back
Top Bottom