Mkuu naomba unionyeshe majibu ya Mohamed Said hasa yaliyojibu hoja stahiki? Ukiweka iitikadi ya kidini hutauelewa mjadala huu utakuwa mpiga makofi tu hata pasipostahili ndugu yangu! Soma kwa makini uzi huu kisha fuatilia hatua kwa hatua majibu ya hoja!
nimefuatilia mjadala huu vizuri sana,hujapinga hoja za msomi Mohamed Said kwa ushahidi,bali umepinga kama ubishi wa mpira sokoni,umepwaya mno,kuendelea kubisha bila hoja ni kujionesha ulivyo dhaifu ktk mijadala.Unaweza kuacha kujadili ni bora ukajipange upya.Vijana wa kileo wanasema umeingia choo cha kike.Kukusaidia huyu Mohamed Said ni msomi wa historia na aliyeifanyia utafiti hiyo historia kwa kufanya mahojiano na watu mbalimbali wa zama hizo.Wewe huna chochote ulichofanya zaidi ya kupinga tu,umekaa na computer yako unaandika tu,toka chumbani nenda kafanye utafiti tafuta habari halafu njoo tena uanzishe mjadala.
Mimi sina tatizo kwa wewe kupinga kitabu changu. Mimi nimekipinga kitabu cha historia ya TANU kilichoandikwa na Kivukoni College sasa iweje mimi nikukataze wewe kukipinga kitabu changu? Tofauti yetu mimi na wewe ni moja tu. Mimi nimepinga kwa kuandika kitabu na kueleza historia ya TANU kwa kutumia nyaraka halisi za wenyewe waliounda African Association na TANU. Wewe mwenzangu unapinga mikono mitupu, maneno matupu na kwa bahati mbaya sana na huu ndiyo msiba niuonao kwako unaandika kwa kejeli na ujuba. Sasa wasomi wanapokhitilafiana katika jambo hupambanisha hoja kwa hoja basi. Hawabughudhiani wala hawatukanani. Iwe itakavyokuwa narudia kusema kuwa sina tatizo kwako au kwa yoyote yule kupinga kitabu changu. Sababu ni moja tu. Wanaoamua ukweli wa kitabu si mtu mmoja au wawili au kikundi cha watu. La hasha. Wanaotoa uamuzi ni wasomi na wanafunzi wa somo uloandikia pamoja wa wanajamii kwa ujumla. Kitabu changu kimefungua mlango mwingine si kwangu mie binafsi bali kwa watafiti katika vyuo vingi duniani vinavyosomesha African History kuitupia jicho upya historia ya Tanganyika. Hili mimi limenitosha. Kitabu sasa kina umri wa miaka 15. Kuwa juu ya kipindi hicho bado kitabu tunakijadili humu JF kama kimetoka jana kwangu mimi ni ushindi na faraja kubwa. Hivi tuandikavyo humu JF kitabu kinakwenda toleo la tatu. Kitabu cha Kivukoni College bado kipo kwenye toleo la kwanza na sidhani kama kuna mpango wa kukichapa tena kwa kuwa hakina wasomaji.
Mpaka sasa hakuna yeyote alioleta uthibitisho kuwa Mohamed Said, ni mchochezi.
Ngoja tuendelea kufuatilia huu mjadala tusubiri kuona huo uchochezi.
Nashukuru kwa maelezo yako mareeeeeeefu lakkini hayana mafaa. Rudia kusoma swali nililokuuliza, linahitaji majibu mawili tu sio ngono mpya.
ukiendelea hapa JF waweza jua kiswahili vizuri,lakini punguza ukereketwa utakuja tukana ktk maandishi yako,weka wazi huo mstari hapo chini
Ndugu yangu, sipo kwaajili ya kukufurahisha wewe, na kama ningelikuja hapa kwa hilo tu basi naamini mpaka dakika hii ungekuwa umelazwa mochwari kwa ajali ya kuvunjika mbavu.
Kimsingi mimi natetea hadhi ya historia ya uhuru wa Tanganyika iliyopotoshwa na mkufunzi wako mzee Mohamed Said, kimantiki mimi natakiwa na ndicho nilichofanya kuipua hoja toka ndani ya kitabu chake na kuzipinga, kisha Mohamed Said aje na ushahidi kwa kuzitetea!
Lakini kichekesho ni kuwa anakuja na vielelezo/ushahidi utetezi kwakutumia kitabu hichohicho alichokiandika yeye.
Hilo tu mkuu Ritz hujaling'amua ila unalishangilia kwa jicho moja, hii ni hatari sana kwa mstakabali wa nchi yetu!
Yericko Nyerere,
Mtu akivujika mbavu anapelekwa mochwari hii kali.
Kwa jinsi unavyojibu unaonekana ujakisoma kitabu cha Mohamed Said, usingemuuliza kama anamjua Adamu Sapi.
Ndugu yangu umeshindwa kuonyesha uchochezi wa Mohamed Said, unachotuonyesha ni kejeli zako, unamwambia Mohamed Said, ana upeo wa kimadrasa, na mimi nambebea viatu yake, hapo ndiyo unaonesha ni mwepesi sana kwa hoja.
Nakushauri punguza kejeli jenga hoja jifunze kupitia huu mjadala.
Yericko,Nyerere amefanya mengi mabaya na watu wameamua kumsamehe, kuendelea kuja na hoja zako za kidini utasababisha kumvunjia heshima babu yako.Mkuu naomba unionyeshe majibu ya Mohamed Said hasa yaliyojibu hoja stahiki?
Ukiweka iitikadi ya kidini hutauelewa mjadala huu utakuwa mpiga makofi tu hata pasipostahili ndugu yangu!
Soma kwa makini uzi huu kisha fuatilia hatua kwa hatua majibu ya hoja!
Nashukuru kwa maelezo yako ndugu yangu.
Unaposema mimi napinga kitabu chako mikono mitupu ni kweli, sijaandika kitabu chakupinga kitabu chako na hili naamini lingekuwa la furaha kwako.
Lakini si mwiko kupinga kitabu chako kwa majadiliano ya hoja hapa jamvini kabla ya kutunga kitabu hicho.
Nimetumia hoja nyingi zilizozaliwa kutokana na kitabu chako ambazo kimsingi wewe unadhamana ya kuzijibu,
Kwa mafaa ya wasomaji wetu hapa jamvini, ungewatendea uungwana kwa kujibu hoja kama zilivyosimama ndugu yangu.
:confused2:WELL THEN,BIG BROTHER STOP :blah:,,JIBU NA UTUELEZE BILA KUMEZA MEZA MANENO KAMA WEWE UNAKUBALIANA NA HOJA ZAKE,,
1.NINI SASA UNACHOKIPINGA??
2.NI HAKI YAKE KIKATIBA KUTOA ELIMU KWA JAMIIM NA KUELIMISHA PALE PALIPOTOSHWA,WEWE KINACHOKUWASHA WASHA NI NINI??
3.HAKUNA ALIEKULAZIMISHA KUSOMA WALA KUKIAMINI ALICHOKIANDIKA,NA KAMA UNA KIRI YA KWAMBA HAJAANDIKA UPOTOSHAJI,SASA POVU LA NINI??
4.KAMA TULIOSOMA TUMEEELEWA NA KUKIAMINI TUAMBIE WEWE SASA UKWELI UNAOUFAHAM WEWE NI UPI??
UMEUMBWA MWANADAMU KISHA UKAPEWA AKILI NA KIPAWA CHA KUAMUA,VIPI BINADAM TUNADHARAU KUTUMIA AKILI HIZO TULIZOPEWA??
Ndugu yangu Mohamed Said sijui kama unatambua mchango wa Adam Sapi?
Kwa taarifa yako mkoa wa Iringa umeweka rekodi kwa kutoa maspika wawili wa nchi hii, mwingine akiwa ni spika wa sasa, Anne Semamba Makinda ambaye ni wa kabila la Wabena kutoka mkoani humo.
Sapi alikuwa spika wa bunge la Tanganyika tangu Desemba 27, 1962, akashikilia nafasi hiyo kwa ufanisi mkubwa hadi Aprili 25, 1994.
Mwaka 1973 hadi 1975 aliuacha wadhifa huo kwa muda baada ya kuteuliwa na Rais Julius Nyerere kuwa Waziri wa Nchi wa Maendeleo ya Mji Mkuu (CDA).
Mtanzania huyo alivunja rekodi ya kushika wadhifa huo kwa muda mrefu zaidi na alifanikiwa kufanya kazi yake bila matatizo kwani alikuwa akisimamia bunge la chama kimoja ambalo lilikuwa la watu ¡®dugu moja¡¯.
Akijulikana kama Mtwa (Chifu), Sapi alikuwa Mwafrika wa kwanza nchini kupewa cheo cha heshima cha Kepteni wa jeshi la wakoloni wa Uingereza la King¡¯s African Rifles (KAR) ambalo ¡®Waswahili¡¯ walilitamka kama ¡®KEYA¡¯ wakimaanisha ¡®kei ei ara¡¯.
Ni chifu Adam Sapi Mkwawa, aliyekuwa Mhehe wa Kalenga, muumini wa dini ya Kiislam ambaye alifariki dunia Juni 25, 1999 kutokana na shinikizo la juu la damu.
Unataka wahehe nao waje na historia yao ya Uhuru wa Tanganyika?
Sijui unakasirishwa na nini mpaka unatoa lugha za kejeli.
ndugu yangu, sipo kwaajili ya kukufurahisha wewe, na kama ningelikuja hapa kwa hilo tu basi naamini mpaka dakika hii ungekuwa umelazwa mochwari kwa ajali ya kuvunjika mbavu.
Kimsingi mimi natetea hadhi ya historia ya uhuru wa tanganyika iliyopotoshwa na mkufunzi wako mzee mohamed said, kimantiki mimi natakiwa na ndicho nilichofanya kuipua hoja toka ndani ya kitabu chake na kuzipinga, kisha mohamed said aje na ushahidi kwa kuzitetea!
Lakini kichekesho ni kuwa anakuja na vielelezo/ushahidi utetezi kwakutumia kitabu hichohicho alichokiandika yeye.
Hilo tu mkuu ritz hujaling'amua ila unalishangilia kwa jicho moja, hii ni hatari sana kwa mstakabali wa nchi yetu!
Nashukuru kwa maelezo yako ndugu yangu.
Unaposema mimi napinga kitabu chako mikono mitupu ni kweli, sijaandika kitabu chakupinga kitabu chako na hili naamini lingekuwa la furaha kwako.
Lakini si mwiko kupinga kitabu chako kwa majadiliano ya hoja hapa jamvini kabla ya kutunga kitabu hicho.
Nimetumia hoja nyingi zilizozaliwa kutokana na kitabu chako ambazo kimsingi wewe unadhamana ya kuzijibu,
Kwa mafaa ya wasomaji wetu hapa jamvini, ungewatendea uungwana kwa kujibu hoja kama zilivyosimama ndugu yangu.
Mpaka sasa hakuna yeyote alioleta uthibitisho kuwa Mohamed Said, ni mchochezi.
Ngoja tuendelea kufuatilia huu mjadala tusubiri kuona huo uchochezi.
Yericko Nyerere,
Mtu akivujika mbavu anapelekwa mochwari hii kali.
Kwa jinsi unavyojibu unaonekana ujakisoma kitabu cha Mohamed Said, usingemuuliza kama anamjua Adamu Sapi.
Ndugu yangu umeshindwa kuonyesha uchochezi wa Mohamed Said, unachotuonyesha ni kejeli zako, unamwambia Mohamed Said, ana upeo wa kimadrasa, na mimi nambebea viatu yake, hapo ndiyo unaonesha ni mwepesi sana kwa hoja.
Nakushauri punguza kejeli jenga hoja jifunze kupitia huu mjadala.
Mkuu na usitegemee kutokea kwa jambo hilo, hawa wenzetu wana utamaduni wa kifaru ( kuzima moto kabla hauja changanya ) wanajaribu kumziba mdomo mzee wetu na huyo Yericko ndio chambo yao, maana wana hofu yakuja kuzaliwa watu wengi kama mzee huyu, lakini tuendelee na mnakasha typate alm, maana huu uzi kwamtu mwelevu nizaid ya darsa