Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
huyu naye ni mchochezi mkubwa wa chuki za kidini
watu hawa ni hatari sana kwa taifa letu ... warudishwe kwao
Kuandika historia ya kweli hakuna hatari yoyote.
Ondoa hofu yako.
Hebu soma hapa chini na nionyeshe hatari iko wapi:
Mwaka wa 1974 Rais Julius Nyerere aliwatwisha Chuo Cha Kivukoni jukumu la kuandika historia ya TANU. Chuo hiki kilianzishwa kama shule ya kuwasomesha makada wa TANU katika mambo ya itikadi, propaganda na uhamasishaji umma wakiiga mfano wa Ruskin College ya Uingereza. Chuo Cha Kivukoni kwa ajili hii kisingeweza kufanya utafiti huru wala kuandika historia sahihi ya TANU.
Mwaka 1976, katika mkutano wa kumi na sita wa TANU Nyerere alisisitiza tena kuandikwa kwa historia rasmi ya TANU. Lakini historia rasmi ziku zote zimekuwa za kupotosha kama anavyoeleza Maslov:
''Kuwafuta watu waliopita ni kasoro nyingine katika maandishi yanayohusu historia ya Chama Cha Kikomunisti cha Urusi. Katika vitabu na makala za utafiti, kama vile ni sheria, watu walio muhimu katika historia huwa wanaorodheshwa katika katika ''orodhaí na baadhi yao hawatajwi kabisa.''
Historia ya Chama Cha Kikomunisti cha Urusi haina tofauti na historia ya TANU.
Mwaka 1985, Rais Nyerere alipokuwa anamtunukia digrii ya heshima Basil Davidson, alitoa changamoto kwa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kuandika historia ya kweli ya Tanzania.
Mwaka 1988, katika sherehe ya kuadhimisha miaka thelathini ya Azimio la Tabora, Nyerere aliwasifu wanachama wa mwanzo wa TANU ambao walijiunga na chama kati ya mwaka 1954 na mwaka 1958.
Nyerere alisema: ''Hicho kilikuwa kipindi kigumu sana katika historia ya Chama chetu na ni watu wachache sana walikuwa na ujasiri wa kujiunga na chama na kukifanyika kazi.''
Jambo la kustaajabisha katika kauli ya Nyerere ni kuwa wakati yeye anawasifu watu waliojiunga na TANU katika ya mwaka wa 1954 na 1958 yeye binafsi hajawaenzi wale ambao siyo tu walijiunga na TANU bali ndiyo waasisi wa TANU yenyewe.
Kwa hali hii inakuwa vigumu kuamini kama kauli yake ilikuwa inatoka kwenye dhati ya nafsi yake.
