Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

kwani amekulazimisha ukisome??toa hoja wapi kuna upotoshaji kwenye maandiko yake??
Hapa mchochezi na mwenye choko choko unaonekana ni wewe,,hueleweki hasa unataka nini,au unaenjoy kuona huu mjadala upo unaendelea,unachangiwa na wengi,muanzilishaji ni wewe n,k.,hueleweki ni hasa unataka,unatuchosha yericko,,

what the hell are you talking about??actions are by their intentions,so whats your intention mr??

Mantiki ya mjadala huu ni kuchambue kwa hoja za kubeza kile kilichopotoshwa na mzee Mohamed
 
Porojo za wazee wa Gerezani bado zinaendelea, duh...! Hakuna adui wa maendeleo kama porojo...kama kawaida kuna watu porojo ni jadi yao! Wanakula porojo, wanavaa porojo na wanalala porojo, kwao porojo na ukweli ni kitu kimoja.

Inaelekea hizi ''porojo'' ni darsa tosha maana napokea simu nyingi za kunipongeza. Nakuwekea hapa ''porojo'' kutoka mdomoni kwake Abdulwahid alipozungumza na Historical Association of Tanzania:

Abdulwahid alipobaini kuwa historia ya Tanganyika inaweza kuwa chanzo cha husda na hasama kati yake na Nyerere na viongozi wengine wa TANU, akaamua kutosema chochote kuhusu hilo (mchango wake katika kuasisi TANU) ingawa kabla hajafa alikubali mwaliko wa Chama Cha Historia Cha Tanzania (Historical Association of Tanzania) (HAT).

Imeshindikana kujua Abdulwahid alizungumza kuhusu nini katika mwaliko ule, lakini inasemekana moja ya maswali aliyoulizwa ilikuwa kuwa kama si kweli Nyerere ndiye aliyekipa chama uhai kuanzia mwaka wa 1954.

Katika kujibu swali hili Abdulwahid alilirudisha swali lile kwa wasikilizaji wake kwa kutoa mfano wa John Glenn, Mmarekani wa kwanza kwenda angani kuzunguka dunia.

Abdulwahid aliwauliza wasikilizaji wake, ''Nani apewe sifa, wanasayansi wa Kimarekani waliotengeneza roketi ile au John Glenn aliyekuwa rubani wa chombo?''

(Kutoka ''Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes...''
 
Baada ya kueleza hayo yote ni muhimu sasa kuangalia jinsi ukereketwa wa Kikristo unavyofanya kazi katika serikali na jinsi kazi hiyo inavyoathiri Uislam. Wizara ya Elimu inachukuliwa kama mfano kwa sababu ya umuhimu wake katika jamii. Katika wizara hii, inaweza kuonekana kwa uwazi kabisa jinsi Ukristo unavyofanya kazi na jinsi udini ulivyoshamiri katika kugawa nafasi muhimu kati ya Waislam na Wakristo.

Ilikuwa katika wizara hii katika historia ya Tanzania ndipo kwa mara ya kwanza waziri Muislam alipochaguliwa kuongoza wizara, Kanisa likaingilia kati waziwazi kumpiga waziri vita na kuhoji nafasi nyingine za juu ambazo zilipewa Waislam. Serikali haikuweza kupingana na Kanisa na waziri huyo, marehemu Profesa Kighoma Ali Malima aliondoshwa katika wizara hiyo.

Mwaka 1987 Profesa Malima aliteuliwa kuwa Waziri wa Elimu akiwa Muislam wa kwanza kushika nafasi hiyo. Mawaziri wanane waliopita walikuwa Wakristo. Kulikuwa na malalamiko kutoka kwa Waislam kuwa wizara hiyo imegeuzwa jimbo la Wakristo, hasa pale padri alipoteuliwa na Julius Nyerere kuongoza wizara hiyo.

Profesa Malima aliposhika wizara hiyo aliona upo umuhimu wa kufanya marekebisho kadhaa ili kurejesha imani ya Waislam katika wizara hiyo. Kulikuwa na tuhuma kuwa Wizara ya Elimu ilikuwa ikiwabagua vijana wa Kiislam kupata nafasi katika vyuo vya elimu ya juu na ilikuwa ikizuia kupanda vyeo kwa Waislam.

Profesa Malima alipoona dhulma ile iliyokuwapo katika wizara ile dhidi ya Waislam, Profesa Malima aliwateua Waislam wanne kushika nafasi katika kurugenzi mbalimbali na akaandika taarifa ya siri kwa Rais Ali Hassan Mwinyi [1]kumtaarifu udini [1] alioukuta katika wizara ile. Katika taarifa ile kwa rais,[1]

Profesa Malima alieleza kuhusu kudumazwa kwa Waislam katika mgao wa elimu. Taarifa hii ilivuja kwa vyombo vya habari[1] na kwa Wakristo wengine. Katika watu walioipata taarifa hii ni Rais Mstaafu Julius Nyerere wakati ule akiwa Mwenyekiti wa chama tawala CCM.
Kuwekwa kando kwa Waislam kupo wazi kiasi ya kuwa mtafiti haihitaji hata kufanya utafiti wa kina unaopewa nguvu na takwimu.

Mtafiti yeyote wa sayansi ya jamii hatoweza kushindwa kuona ukweli huu kwa macho tu. Hali hii inaonekana katika kila nyanja ya maisha. Utafiti wa kwanza katika tatizo hili la Waislam kudhulumiwa katika ugawaji wa madaraka ulifanywa na vijana wa Kiislam katika jumuiya yao iliyokuwa ikijulikana kama Warsha ya Waandishi wa Kiislam, kwa ufupi ikijulikana kama Warsha.

Kanisa kwa mara ya pili tokea mwaka 1963 ilipata wasiwasi kuhusu mabadiliko ambayo yalikuwa yanafanyika katika Wizara ya Elimu. Lakini katika miaka ya 1980, hali ya mambo yalikuwa yamebadilika sana. Waislam walikuwa wamejizatiti nje ya mfumo wa siasa kiasi ya kuwa hapakuweza kupatika kibaraka katika Waislam ambae angekuwa tayari kutumika kulihami Kanisa. Hali ya uhasama wa wazi kati ya Waislam na serikali ilikuwa imejitokeza wazi kabisa.

Hata hivyo mawakala wa kanisa katika serikali walimshutumu Profesa Malima kwa kuwa Muislam mwenye ësiasa kalií. Profesa Malima akatakiwa ahojiwe mbele ya Kamati Kuu ya CCM kwa kuingiza hisia za kidini ambazo zimesababisha uadui baina ya waumini wa dini hizi mbili. Suala hili likajadiliwa Dodoma chini ya uenyekiti wa Julius Nyerere.

Lakini badala ya kujadili suala la dhulma kwa Waislam na kulitafutia ufumbuzi, yule anaedhulumiwa ndiye aliyewekwa kizimbani badala ya dhalim anaedhulumu; msukumo wa mjadala ukawa katika uteuzi wa wakurugenzi wanne Waislam aliofanya Profesa Malima katika Wizara ya Elimu. Profesa Malima alionekana amekiuka mwenendo na taratibu zulizodumu katika wizara ile kwa kipindi kirefu ya kuwa ni Wakristo pekee wenye haki ya kushika nafasi za juu katika wizara za serikali.

Kwa ajili hii profesa Malima akavuliwa madaraka kama Waziri wa Elimu. Rais Mwinyi alikuwa hana uwezo wa kuhimili nguvu ya Kanisa. Nchi inayodai kuwa ni ya kisekula ilikuwa imeshindwa kwa mara nyingine kuwapa Waislam haki yao waliyohakikishiwa na katiba ya Tanzania.

(Kutoka ''Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes...'')
Kumekuwa na waislam watatu waliongoza wizara hii. Juma Kapuya, Jumanne Maghembe na sasa Shukuru Kawambwa. Taarifa zako zinasemaje, na hawa wanapingwa na kanisa? Ni kwanini hawajagundua uoza aliogundua malima wakati zama hizi transparency ni kubwa na ni rahisi kuibua uoza kwenye wizara yeyote?
 
Porojo za wazee wa Gerezani bado zinaendelea, duh...! Hakuna adui wa maendeleo kama porojo...kama kawaida kuna watu porojo ni jadi yao! Wanakula porojo, wanavaa porojo na wanalala porojo, kwao porojo na ukweli ni kitu kimoja.
Mkuu, jamaa wako addicted na hizi porojo zinazowafanya wawe kama mazezeta yanayoambukizana uzezeta...sijaona hata sehemu moja mohamed said akiwahimiza waislam kusoma kwa bidii zaidi ya kulalamika...huyu ndiyo role model wao...full kulalamika/uzezeta...
 
Ukiondoa udini ambao in my view,Mohamed Said kautumia visivyo ku prop up sales za kitabu-ukweli usiopingika jamaa kashusha nondo nzito sana katika hiki kitabu
P1080317.JPG
 
Unaandika umekasirika.

Mimi ni mashuhuri na naalikwa katika mahafali ya shule nyingi za Kiislam.
Huwezi kualikwa kama hupendi elimu.

Katika kitabu changu kuna habari muhimu kuhusu elimu na matatizo yaliyowakuta
Waislam katika EAMWS waliotaka kujenga chuo kikuu mwaka 1968.

Kisa hiki ni maarufu sana.

Hatulalamiki tunawatayarisha na kuwajulisha Waislam wajue historia yao na dhulma
wanayofanyiwa.

Matokeo ya juhudi hizi ndiyo haya unayoona leo.
Waislam wanadai haki zao.
 
Ukiondoa udini ambao in my view,Mohamed Said kautumia visivyo ku prop up sales za kitabu-ukweli usiopingika jamaa kashusha nondo nzito sana katika hiki kitabu
View attachment 79422
Nakushukuru kwa kuweka hapa kitabu.

Nakulaumu kwa kusema natafuta mauzo ya kitabu changu.
Hapana.

Kilichonisukuma ilikuwa kutoa jibu tu kwa kile kitabu kilichoandikwa
na Chuo Cha Kivukoni.
 
Kumekuwa na waislam watatu waliongoza wizara hii. Juma Kapuya, Jumanne Maghembe na sasa Shukuru Kawambwa. Taarifa zako zinasemaje, na hawa wanapingwa na kanisa? Ni kwanini hawajagundua uoza aliogundua malima wakati zama hizi transparency ni kubwa na ni rahisi kuibua uoza kwenye wizara yeyote?

Itabidi ufungue uzi mpya tuzungumze kila kitu katika hiyo Wizara na mambo yake.
Ila kwa sasa ikutoshe tu kuwa Insha Allah hivi karibuni zitasikika taarifa za NECTA.

Usidhani ni maskhara.
Mengine hata mimi sijaweza kuamini.

Hawa jamaa wataalamu kwelikweli.
Wanajua kuwazunguka Waislam.

Sasa hivi wanashughulika na shule za kata.
Maana zimejaza Waislam.

Kuwa na subra.
 
Andrew,where arth thou,our hero father of the nation is being hanged out to dry-give us the other side of the coin-give us the real Nyerere
 
Last edited by a moderator:
Itabidi ufungue uzi mpya tuzungumze kila kitu katika hiyo Wizara na mambo yake.
Ila kwa sasa ikutoshe tu kuwa Insha Allah hivi karibuni zitasikika taarifa za NECTA.

Usidhani ni maskhara.
Mengine hata mimi sijaweza kuamini.

Hawa jamaa wataalamu kwelikweli.
Wanajua kuwazunguka Waislam.

Sasa hivi wanashughulika na shule za kata.
Maana zimejaza Waislam.

Kuwa na subra.
Shule za kata hizi zenye walimu wawili wanafeli waislam tu? Dah...
 
Unaandika umekasirika.

Mimi ni mashuhuri na naalikwa katika mahafali ya shule nyingi za Kiislam.
Huwezi kualikwa kama hupendi elimu.

Katika kitabu changu kuna habari muhimu kuhusu elimu na matatizo yaliyowakuta
Waislam katika EAMWS waliotaka kujenga chuo kikuu mwaka 1968.

Kisa hiki ni maarufu sana.

Hatulalamiki tunawatayarisha na kuwajulisha Waislam wajue historia yao na dhulma
wanayofanyiwa.

Matokeo ya juhudi hizi ndiyo haya unayoona leo.
Waislam wanadai haki zao.

you have worn the hearts of muslims especially those who cannot think out of the religious box,so brother u have the right to get a multitude of invitations to inspire the muslim congregations. But one thing i can't hestate to air it to the great thinkers' theatre is that mohamed said umetulia mzee hauna papara hilo silifichi
 
Mkuu, jamaa wako addicted na hizi porojo zinazowafanya wawe kama mazezeta yanayoambukizana uzezeta...sijaona hata sehemu moja mohamed said akiwahimiza waislam kusoma kwa bidii zaidi ya kulalamika...huyu ndiyo role model wao...full kulalamika/uzezeta...

Naona umeishiwa hoja sasa umejikita kwenye viroja.

Leo siku ya tatu nakuona upo kwenye huu uzi ambayo unasema porojo na mazezeta.

Namshukuru sana Mohamed Said, kwa kutoa darsa muruwa. Kuna watu wanamkejeli huku wanajifunza kwake.

Ukiona mtu anaponda kitu halafu bado anakifuatilia kwa umakini wa hali ya juu hujue kavutiwa na nondo.
 
huyu naye ni mchochezi mkubwa wa chuki za kidini

watu hawa ni hatari sana kwa taifa letu ... warudishwe kwao
 
Last edited by a moderator:
Hakika Mohamed Said, umetushibisha elimu umeweka mambo hadhwarani.

Nimejifunza mengi sana kutoka kwako jinsi ya kufanya munakasha kiungwana.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom