Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Mohamed Said said:
Ama kuhusu DVD ya Ilunga kama mnataka uchambuzi wake hilo ni suala la maulamaa na mie ilm hiyo sina.
Mohamed Said,

..Shekhe Ilunga amevuka mpaka ktk mhadhara wake na kuhubiri umwagaji damu.

..hivi unafikiri ni Ulamaa gani atakayeunga mkono uchochezi wa namna ile??

..hata kama Ilunga ni ndugu yako, haupaswi kuwa "bubu" anapotoa kauli ambazo zinaweza kuiingiza nchi ktk machafuko.

cc: Ritz


 
Last edited by a moderator:

Mohamed Said,

..Shekhe Ilunga amevuka mpaka ktk mhadhara wake na kuhubiri umwagaji damu.

..hivi unafikiri ni Ulamaa gani atakayeunga mkono uchochezi wa namna ile??

..hata kama Ilunga ni ndugu yako, haupaswi kuwa "bubu" anapotoa kauli ambazo zinaweza kuiingiza nchi ktk machafuko.

cc: Ritz

Nimesema kuwa ilm ya kufutu mas'ala mie sina.
Itabidi watafutwe maulama ndiyo wahukumu.
 
Unamaanisha huna majibu ya hoja zangu?

Nishakwambia mara nyingi sana kuwa ujitulize.

Huko nyuma nishakueleza kuwa mimi huwa silazimishwi kufanya jambo.
Nishakueleza vilevile kuwa kuna post huwa sioni sababu ya kuchangia.

Nakuomba uridhike na jibu ninalokupa.
Usinilazimishe nikupe jibu ulitakalo.

Sina zaidi.
Nadhani umenielewa.
 
Pia nilikuliza hivi haya maswali


quote_icon.png
By adolay Mkuu Ritz

Neno padri ni cheo katika kanisa katoliki na kwa imani ya wakatoliki padri haruhusiwi kuoa nasikitika kwanini umwite Dr W.P slaa padri wakati anamke/mchumba vyovyote?

b) Wewe ni mwislam vipi kujishughurisha na kanisa katoliki umepewa huo usemaji lini mkuu na mamlaka ya kuteuwa mapadri?

c) Yeye amekujibu vibaya nani? unataka kutuambia Dr W. P slaa ndiye aliyekujibu vibaya kama siyo yeye vipi umshabulie yeye?

Tanzania itatawaliwa na mtanzania yoyote awe mpagani, mkritu au mwislam kama ilivo sasa kwa kuzingatia uwezo wake.

Fahamu hakuna Cheo cha rais kama padri au shekhe kwenye katiba na katiba hairuhusu upuu huo.


Naomaba ufafanuzi mkuu wangu.



majibu yako Ritz yalikuwa hivi
Mkuu adolay,

Na mimi naomba nikuulize kuna ubaya wowote kumuita mtu yoyote kwa Professional yake hata kama kastaafu. Upadri ni taaluma kama taalumu zingine mpaka uende shule.

Katiba haijakataza kugombea lakini ni busara kutokugombea sababu Watanzania tumechanganyikana dini mbalimbali.

Nadhani nimejibu vyema.

Mkuu wewe ni mkiristo vipi unajishughulisha na mambo ya waislam tena umekwenda mbali zaidi mpaka Somalia.​





Nikakuliza na kukujibu hivi

Mkuu

1.Hujajibu swali hata moja narudia alikujibu vibaya ni nani, Dr slaa?

2. Unafahamu katiba ya wakatoliki? kama unaifahau elezea upadri wa padri yoyete anaupataje?

3. Je kuna sifa zozote zinazoweza kumuondolea mtu upadri katika katiba ya kanisa na unaweza kuzitaja?

4. Je kunakustaafu upadri au kuacha katiba inasemaje ya wakatoriki na umri gani padri anapaswa kustaafu kama uliosema hapo juu.




Jibu Kuhusu waislam

Nani anakesha hapa kuleta hoja za mfumo kristo?, dhulma dhidi ya waislam?, Mou nk katika madai haya ungetaka nani akujibu?

a) mwislam na kama mwislam kwanini

b) mkristo na kwanini awe mkristo

tutaendelea mkuu Ritzs ukinijibu hapa, maana ndipo jibu lako lilipo.

Nifanyie uungwana kwa kujibu jibu sahihi kwa kila swali yaani mstari baada ya mstari.




Angalia majibu unayotoa hapo juu kwa kila ulichoulizwa, kisha tafakali kioja kipo wapi.

Ritz uwezo wako kusimamia hoja ni mdogo sana kama unavyojieleza hapo juu, haya ndiyo matokeo ya kuukumbatia uchochezi

kama ulivofuzu kozi za babu yako mohamed said za kichochezi mkiacha ukweli kule na kuamua kupotosha umma wa watanzania.

adolay,

Tumia lugha nzuri jifunze kwa wenzako unakuwa kama Nape anavyomkejeli Dr Slaa kumuita Babu...JF hakuna medali ya matusi wala kejeli, JF Home of Great Thinkers.
 
Last edited by a moderator:
Hamjanifahamu katika maandishi yangu. Sitafuti umaarufu wala sifa. Jukumu langu ni kusomesha basi. Kwa ajili hii "kubomolewa" au kinyume cha hivyo si jambo linalonishughulisha. Ama kuhusu DVD ya Ilunga kama mnataka uchambuzi wake hilo ni suala la maulamaa na mie ilm hiyo sina.
Hakuna ilm pale, upuuzi ni upuuzi! period. Mwislam mwenye kuijua dini yake kwa mafunzo, mwenye akili timamu na mwenye nia na dhamira safi ya daawa na ulinganifu wa dini ya mwenyezi mungu hawezi kusimama na kutetea uchafu kwa jina la ulmaa.

Acheni kutumia dini kukidhi kiu na matamanio yenu. Dini ya Uislam ni amani na salama. Rejeeni katika mafunzo ya Mtume Mohamad S.A.W, sunna na Korani na si kuudanganya umma. Too low! msiidhalilishe dini. Tool low, stupid and uncouth! simple

Mkuu Ritz, nakupongeza kwa kusimama na kusema hili si sahihi, huo ndio uungwana na ubinadamu.Umesimama na kusema hayo ni makosa ya kibinadamu, huo ndio uvumilivu na ukomavu,ya kwamba unafanya na kusema kilicho sahihi.
Hukutafuta perfume ya kuzuia uvundo. Thanks!
 
Tusipende kulalamika tu hapa!dini zote hizi zimeletwa na mataifa ya nje!sasa ebu tuangalie na kujikumbusha kidogo tu bila hata yakutumia nguvu nyingii!
wakati wakoloni wanaingia nchini moja ya malengo ya hao watawala ilikuwa ni kueneza dini zao !sasa ni ukanda upi ulitawaliwa na wakolono wakristu?na malengo yao yalikuwa ni yapi? kimsingi malengo yao ilikuwa ni kueneza dini dinihiyo wataenezaje?lazima waazishe shule watu wajue kusoma na kuandika na wawe na uelewa mpana kuhusiana na kile wanacho fundishwa!ukiangalia sasa maeneo mengi yalitawaliwa na wakoloni wa kikristo na ndiko shule nyingi zilijengwa na na haitabishaniwa kuwa wakristo wengi walisoma mapema!angalia shule za seminari za kiislam hazifanyi vizuri hadi leo ambapo mwalimu nyerere hayupo je kwa sasa mwalimu bado anawadumaza?jipangeni upya jifunzeni kwa wakristo wawape siri ya mafanikio yao!
 
Mkuu sijali labda wewe umeona hayo majibu.

Tafadhali tujuze walau kwa moja tu la MOU

- Nani amewazuia waislam wasiwe na mou yao? ukimaliza hilo tutakuuliza kwanini mohamed analalamikia Mou ya wakristu

Anaye / Aliye zuia M O U yetu ( waislam ) ni serekali inayoongozwa na mfumo kristo. Nimuda mrefu sasa tangu tulipo wasilisaha lakini mpaka sasa tunapigwa danadana. Ndio maana tunaona hii MOU iliopo sasa iondolewe, maana inawapa mslah nyinyi na inatukandamiza sisi
 
Hakuna ilm pale, upuuzi ni upuuzi! period. Mwislam mwenye kuijua dini yake kwa mafunzo, mwenye akili timamu na mwenye nia na dhamira safi ya daawa na ulinganifu wa dini ya mwenyezi mungu hawezi kusimama na kutetea uchafu kwa jina la ulmaa.

Acheni kutumia dini kukidhi kiu na matamanio yenu. Dini ya Uislam ni amani na salama. Rejeeni katika mafunzo ya Mtume Mohamad S.A.W, sunna na Korani na si kuudanganya umma. Too low! msiidhalilishe dini. Tool low, stupid and uncouth! simple

Mkuu Ritz, nakupongeza kwa kusimama na kusema hili si sahihi, huo ndio uungwana na ubinadamu.Umesimama na kusema hayo ni makosa ya kibinadamu, huo ndio uvumilivu na ukomavu,ya kwamba unafanya na kusema kilicho sahihi.
Hukutafuta perfume ya kuzuia uvundo. Thanks!

Ndugu yangu una ghadhibika haraka.

Nitachangia kwa kidogo sana.
Sheikh Ilunga amezungumzia ''kisasi.''

Imesomwa aya kuhusu kisasi kama Allah alivyosema katika Qur'an.
Kutokea hapo kinachofata ni ''interpretation'' ya hiyo aya.

Katika mazingira gani kisasi kitekelezwe na kadhalika.

Hapo ndipo mimi nikasema huo siyo uwanja wangu ilm hiyo ya kutafsiri
Qur'an sinayo kwa hiyo sitoweza kutoa fatwa.
 
Wala sina nongwa kwa hilo, nongwa yangu inasimama kwenye dhamira yako kuu ambayo ni UDINI wako ndani ya nchi isiyokuwa na udini.

Kichekesho zaidi ni kuwa maandishi yako huko nyuma ulisema wazi kuwa uliowatetea na unaowatete kwa kuwaandikia kitabu na leo kukigeuza kuwa ndio historia kuu ya Uhuru ni wazee wako, tena ukakazia kuw ni wazee wako wa damu!

Lakin tena hapa unazidi kukazia kuwa Ilunga ni mzee wako wa damu,

Sasa mantiki kuu ya kitabu chako inasimama rasmi kuwa simulizi ya wazee wako tu (baba yako) sio ya watanzania 44.5milioni.

Kibaya zaidi umepotosha kwakuiita eti historia ya uhuru wa Tanganyika upande wapili, hivyo unatueleza kuwa BABA yako angewekwa kwenye historia asili ya uhuru leo hii waislamu wasingekuwa na ajiitae mtetezi wao Mohamed Said?

Nimeeleza mara nyingi kabisa kuwa kitabu hicho sasa kina miaka 15 kinasomwa na tunakwenda toleo la tatu.

Nimesema mara nyingi pia kuwa si lazima mtu akakiamini kitabu changu.
Mimi sina ugomvi na mtu ambae atasema kuwa yale niliyoandika ni uzushi mtupu.

Sina uwezo wa kufanya mtu aniamini isipokuwa kuandika na kushawishi kuwa niandikayo ni kweli.
Sasa endapo kitabu kitaonekana cha maana hiyo ndiyo furaha yangu.

Halikadhalika ikiwa msomaji atakipuuza kitabu changu sina la kufanya.

Ila sasa kitabu hiki kimefaulu.
Ndicho kitabu kinachoaminika katika historia yake Nyerere mwenyewe ya kudai uhuru
na historia nzima ya TANU.
 
Nishakwambia mara nyingi sana kuwa ujitulize.

Huko nyuma nishakueleza kuwa mimi huwa silazimishwi kufanya jambo.
Nishakueleza vilevile kuwa kuna post huwa sioni sababu ya kuchangia.

Nakuomba uridhike na jibu ninalokupa.
Usinilazimishe nikupe jibu ulitakalo.

Sina zaidi.
Nadhani umenielewa.

Ndugu yangu naona unaishiwa majibu ama kweli hutaki kujibu kwa maksudi tu,

Mimi sikulazimishi ujibu, lakini kitabu chako kinaibua hoja ambazo zinakulazimisha ujibu!

Hebu kitendee haki kitabu chako kwakujibu hoja!

Mmoja wa walimu wangu aliwahi kuniambia kuwa, hakuna upuuzi ulio upuuzi mtupu!
 
Anaye / Aliye zuia M O U yetu ( waislam ) ni serekali inayoongozwa na mfumo kristo. Nimuda mrefu sasa tangu tulipo wasilisaha lakini mpaka sasa tunapigwa danadana. Ndio maana tunaona hii MOU iliopo sasa iondolewe, maana inawapa mslah nyinyi na inatukandamiza sisi

Lini mliwasilisha hiyo MoU? Lete hapa nakala yake!
 
Nimeeleza mara nyingi kabisa kuwa kitabu hicho sasa kina miaka 15 kinasomwa na tunakwenda toleo la tatu.

Nimesema mara nyingi pia kuwa si lazima mtu akakiamini kitabu changu.
Mimi sina ugomvi na mtu ambae atasema kuwa yale niliyoandika ni uzushi mtupu.

Sina uwezo wa kufanya mtu aniamini isipokuwa kuandika na kushawishi kuwa niandikayo ni kweli.
Sasa endapo kitabu kitaonekana cha maana hiyo ndiyo furaha yangu.

Halikadhalika ikiwa msomaji atakipuuza kitabu changu sina la kufanya.

Ila sasa kitabu hiki kimefaulu.
Ndicho kitabu kinachoaminika katika historia yake Nyerere mwenyewe ya kudai uhuru
na historia nzima ya TANU.

Ndugu yangu unaendelea kujichanganya tu, maelezo yako ya mwanzo ulisema wazi kuwa hujawahi kuhadhiri sehemu yoyote kwa hapa Tanzania, na zaidi ukadia wizara husika wamekiita ni "conspiracy" yaani ni cha kufikirika tu, kwa hilo tu nawasifu wizara!

Lakini hapa tena umebadili maneno na kusema ndicho kinachotambuliwa kwa historia halisi ya UHURU wa nchi hii?????

Nani wanakitambua?, watanzania au huko umangani ulikohadhiri?
 
"UDINI "Ningekuwa na uwezo wale wote wanoleta mada za kujenga chuki miongoni mwa wakristu na waislamu ningewapa bann ya mwaka mzima.Tuuweke UTANGANYIKA/UTANZANIA wetu kwanza mengine yanafuata.Hizi dini waliozileta wanapigana.Tuingelee namna gani tutasonga mbele na siyo KADHI,Mfumo kristu/Islamu blaahblah.Inachosha.:A S angry:
 
Inaudhi kusikia mtu kanyinwa haki kumbe hata "a" hajui, kusema amesahauliwa kumbe tukio lilikuwa kwa jirani yake. Tuwaache na maneno yenu ya kudai hata msichostahili. Hata mkipewa, dhambi hii hamuiachi itawala mpk mwisho mtabaguana koo na koo, mpk shehe na shehe mwenzake. Hata wenyewe kwa wenyewe jirani na jirani yake, mnafundisha vijana wenu kupigana kareti elimu inasinzia wanaferi, kesho muanze kudai mmesahauliwa. Masomo yalikuwa matatu mmepunguza napo mmefeli tu kama hujuihujui tu. Tutabadilisha mpk yale makosa ndy ziwe vema kwa wanenu. Mienendo ya hawa watu ni vurugu tu al qaeda element. Ukimpa ndoano anataka ukamvulie na huyo samaki historia ya kudai na kuhamasisha ndiyo iliyoharibu mataifa ya masahariki ya kati. Mungu nae anajua ukiwa na hiki anakupa changamoto. Siyo changamoto zetu hizi, bali sisi ni maisha yaliyokatika mazingira magumu. Endeleeni na ubazazi wenu tutaendelea hata kama hamtaki mtatoa na historia ya kwamba baba zenu walikuwa watawala sasa mpewe kutawala haaaaaaaya pu!!
 
Mmm, naanza kuhisi kwamba kumbe wote tunatakiwa tuwe Wakristo cause ndio dini yenye nguvu, kwanini kila sehemu Waislam ni watu duni hivi? Je? mungu wao hana nguvu kama Mungu wa Wakristo? rejea maswali yalioulizwa kwa bwana mohamed said hapo juu, kwani Somalia nchi yenye waislam wengi lakini ni nchi duni isio hata na amani, nenda Nigeria kaskazini kule kwenye waislamu wengi, kote huko ni sehemu masikini kweli na duni hasa, niliona siku moja kwenye Emmanuel TV, TB Joshua anawapelekea misaada ya chakula na mavazi, hali za watu wale kwakweli ni za kutia huruma sana, yaani masikini wa kutupwa, kitu cha ajabu sana ambacho hua siwaelewi nyie waislamu hua ni hiki, utakuta mtu hana hata pesa ya kununulia Kandambili au Viatu, lakini huyo huyo anazo pesa za kununulia silaha za kuwaulia Wakristo, hapo hua sielewi kabisa, back to the topic, tusipo angalia tutakuja potosha Historia hivihiv, naona humu kuna watu wanaanza kuaminishwa kuwa Hospitali za Makanisa zimejengwa kwa msaada wa MOU, hivi MOU imesainiwa lini na hizo Hospitali zimejengwa lini, kwa kumbukumbu zangu, Bugando kwamfano, ukienda pale kwenye jengo lao utakuta imejengwa 1971, sijui hasa ujenzi uliianza lini lakini mwaka huo ndio hospitali ilianza kufanya kazi, waislamu mlikuwa wapi? KCMC, nimekua naisikia, KOlandoto Hospital ipo tokea miaka ya 60 huko, Peramiho kule Songea, tokea nikiwa mtoto mdogo kabisa, Ilembula Hospital kule Iringa (Sasa Njombe) ipo tokea miaka ya 70s, miaka yote hiyo watu wenye uwezo walikua wanaenda kutibiwa hospitali zilizokua zikiitwa za misheni.

Ukweli kinachowasumbua ndugu zangu waislam sio hayo madai, ni wivu tu tena wa kijinga, hakuna watu creative huko kwenu, angalia misaada mnayo itaka hata sasa, sio shule au hospitali, nyie mnadai mahakama ya kaadhi, hivi nyie mnajiona kuwa ni wafanya makosa sana au tusemeje? Pesa za kuendesha chuo cha Morogoro toka serikali mnapata, mbona chuo hakiendelei?, haya shule za Kiisalamu kama Jamuhuri Dodoma au ile ya Kinondoni, mnadai eti NECTA inawafelisha watoto, ngoja tuone kama ni kweli, haya na mitihani ya Mock ambayo waalimu husika ndio wanatunga na kusahihisha, matokeo yake huwa yakoje? Uvivu wa kufikiri nao sometimes ni msiba mkubwa kwenye jamii, Tafakarini!
 
Ndugu yangu unaendelea kujichanganya tu, maelezo yako ya mwanzo ulisema wazi kuwa hujawahi kuhadhiri sehemu yoyote kwa hapa Tanzania, na zaidi ukadia wizara husika wamekiita ni "conspiracy" yaani ni cha kufikirika tu, kwa hilo tu nawasifu wizara!

Lakini hapa tena umebadili maneno na kusema ndicho kinachotambuliwa kwa historia halisi ya UHURU wa nchi hii?????

Nani wanakitambua?, watanzania au huko umangani ulikohadhiri?

Ungeweza kuniuliza vyuo nilivyoalikwa kuhadhiri bila hata ya kunitukana na kunikejeli.
Nami ningekujibu kiungwana na tungeendelea na mjadala. Kuanzia hapa usishangae ukioona nimekupuuza sikujibu kitu.

1. The Life and Times of Abdulwahid Sykes 1924 –1968 The Untold Story of the Muslim Struggle against British Colonialism in Tanganyika, Minerva Press London, 1998 translated into Kiswahili as Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes 1924-1968 Historia Iliyofichwa Kuhusu Harakati za Waislam Dhidi ya Ukoloni wa Waingereza, Phoenix Publishers, Nairobi, 2002.

2.
Torch on Kilimanjaro, Oxford University Press, Nairobi 2006

3. Contributing author African Anthology, The Mermaid of Msambweni, Oxford University Press, 2008 Nairobi

4.
Uamuzi wa Busara, Abantu Publications, Dar es Salaam, 2009

5. Broken Dreams: The Life of Ally Sykes, Phoenix Publishers, Nairobi forthcoming

PART OF RESEARCH PAPERS/ARTICLES

1. In Praise of Ancestors (1987) Africa Events (London)

2. Abdulwahid Sykes: Founder of Political Movement (1988) Africa Events (London)

3. Islam and Politics in Tanzania (1989) Al Haq International (Karachi)

4.
The Plight of Tanzanian Muslim (1993) Change (Dar es Salaam)

5. Tanzania - The "Secular" Unsecular State (1995) Change (Dar es Salaam)

6. The Question of Muslim Stagnation in Education in Tanzania - A Muslim Riddle (Paper presented at the Conference of the Global World of the Swahili Intercultural Dialogue on the Indian Ocean Zanzibar, February 20 - 23, 2000

7. Islamic Education and Intellectualism in Eastern Africa ‘Themes from the Pulpit in Tanganyika (Tanzania Mainland) 1800 – 2000 (Paper presented at International Symposium on Islamic Civilisation in Eastern Africa Kampala, Uganda organised by the Islamic Conference Research Centre for Islamic History, Art and Culture (IRCICA), Istanbul and the Islamic University in Uganda, Mbale December 15[SUP]th[/SUP] – 17[SUP]th[/SUP] 2003)

8. Sheikh Hassan bin Ameir - The Moving Spirit of Muslim Emancipation in Tanganyika (1950 – 1968) (Paper presented at Youth Camp Organised by Zanzibar University, World Assembly of Muslim Youth (WAMY) and Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) 27[SUP]th[/SUP] February – 4[SUP]th[/SUP] March 2004)

9. Islamic Movement and the Christian Lobby in Tanzania - the Experience of the late Prof. Kighoma Ali Malima (1938 – 1995) (Paper Presented to Tanzania Muslim Students Association (TAMSA) Sokoine University of Agriculture (SUA) Morogoro 11[SUP]th[/SUP] April 2004)

10.Terrorism in East Africa the Tanzanian Experience (Paper Presented at the Conference on Islam, Terrorism and African Development University of Ibadan, Nigeria 8[SUP]th[/SUP] - 10th February 2006)

11. The Legacy of Sheikh Ahmed Deedat (Paper Presented at International Symposium on Islamic Civilisation in Southern Africa, University of Johannesburg 1 - 3 September, 2006 (the paper was again presented to Islamic Propagation Centre International, Durban)

12.
Al Marhum Sheikh Kassim bin Juma (1940 – 1994) And the Dar es Salaam Pork Riots of 1993 Kenyatta University, Nairobi 2006

13. Visiting Scholar, University of Iowa, Iowa City and Northwestern University, Chicago, Illinois, USA, Presented paper on Islam and Politics in Tanzania, April 2011

14. Visiting Researcher Zentrum Moderner Orient, Berlin Germany, Presented Paper ''Christian Hegemony and the Rise of Muslim Militancy in Tanzania,'' July 2011.

Awarded Certificate of Appreciation by United States Information Services (USIS) for research into political history of Tanganyika and made Member Library of Congress, Washington, DC.
 
Mohamed Said,

Asante kwa majibu mazuri.
Kama una mda naomba uendelee kunielimisha machache kutokana na maswali ninayokuuliza. Naamini wapo na wengine watalaokuwa wanaelimika.
Inawezekana kweli hao wazee wetu (naamini ni wazee wa watanzania wote), walibaguliwa katika historia ya uhuru kwa sababu ya dini yao. Hata hivyo upo uwezekano sio kwa sababu ya dini pia, nikidhani kuwa pengine wapo hata wengine ambao hawakuwa waislamu ambao 'wamefunikwa'.
Naamini pia wewe kama muislamu una fahari kuwaenzi wazee wako waislamu. Swali langu dogo ni je, wewe kama mwanahistoria, huoni umuhimu wa kuandika pia historia ya hawa wazee, bila kuattach dini zao? Namaanisha kwamba ukatumia resources ulizojaaliwa kuwa nazo, na uwezo wako wa kuandika, na ukawaelimisha Watanzania historia ya uhuru, pengine bila ya kutaja sana dini? Nauliza hivi kwa sababu, kwa mtu ambaye ni radical kidogo, akisikiliza, au akisoma maandiko yako, anaona kama unaandika kwa ajili ya waislamu. Tutegemee kutoka kwako maandiko mengine ambayo yatataja wapigania uhuru bila kujali dini zao?
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom