Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

Kwanza nikusihi kuwa na adabu unapoongea/kujadiliana na mtu yeyote yule,

1) Ninapinga kupotoshwa kwa historia ya Uhuru wa Tanganyika.


2) Nikweli ni haki yake kuelimisha lakini si kuchochea maasi kwa kujenga tabaka la ubora mimi. (muislamu)


3) Ikiwa kitabu chake amekihalalisha kuwa ndio historia ya uhuru wa nchi hii, hapo ni 100% amemlazimisha kila binadamu duniani kusoma na kuamini alichokiandika. Hiyo ni shuruti.

4) Ukweli ninaoufahamu na uliondani ya mioyo ya wapenda amani waislamu kwa wakristu upo katika kitabu cha TANU kilichoandikwa na chuo cha kivukoni.
 

Mzee Mohamed labda tuangalie Scientific/mang'amuzi ya dhana ya UKWELI,

Ukweli huwa unasimama hata kama waamini na waumini wa UKWELI huo hawasujudu ukweli wenyewe.

Kitabu cha TANU kutotumika katika mafundisho ya historia kama unavyodai, sio kuwa sasa nchi haina historia na dhamana hiyo umeikwaa wewe na kitabu chako.

Ukweli unabaki pale pale kuwa historia ya Uhuru wa nchi hii imo katika kitabu cha TANU na si vinginevyo, kama kunamapungufu ni kuhuisha tu na sikuumba magomvi na machochezi yenye kuhatarisha umoja wetu uliojengwa kwa miongo mitano sasa!
 
I HOPE HAKUNA SEHEMU YOYOTE NILIYOKOSA ADABU KATIKA HOJA YANGU NA NASHUKURU KWA KUNIJIBU

1) Ninapinga kupotoshwa kwa historia ya Uhuru wa Tanganyika,,USAHIHI UPO WAPI?KAMA AMEPOTOSHWA KWA JAMBO KUBWA KAMA HILO MBONA JAMHURI HAIJAMSHITAKI??


2) Nikweli ni haki yake kuelimisha lakini si kuchochea maasi kwa kujenga tabaka la ubora mimi. (muislamu).>>KUELEZEA MCHANGO WA WATU FULANI AMBAO UMEFUTWA KWA MAKUSUDI KWA KULINDA INTEREST ZA WENGINE NI KUJENGA TABAKA NA KUJIKWEZA??,MBONA WAPO WAKRISTO NA WAISLAM WOTE KAWAAINISHA MCHANGO WAO,AU WEWE HUJASOMA KWA UMAKINI MAANDIKO NA HOJA ZAKE??


3) Ikiwa kitabu chake amekihalalisha kuwa ndio historia ya uhuru wa nchi hii, hapo ni 100% amemlazimisha kila binadamu duniani kusoma na kuamini alichokiandika. Hiyo ni shuruti.>> SIKU ZOTE UPUUZI,HUPUUZWA,KWANI WEWE HUWA UNAAMINI KILA UNACHOKISOMA NA KUKISKIA??KAMA KUANDIKA ALIKOANDIKA NA KUWAACHIA WATU WENYEWE WASOME NA WAPIME NI SHURUTI,MANENO HAYO UNAYOSEMA YANA UHALISIA??HAKUNA ALIEMLAZIMISHA KUKISOMA WALA KUKIAMINI,ILA KILA MWENYE AKILI TIMAMU ATAUONA UKWELI NA KUAMUA EITHER KUUFUATA AMA KUUKACHA,UPO??

4) Ukweli ninaoufahamu na uliondani ya mioyo ya wapenda amani waislamu kwa wakristu upo katika kitabu cha TANU kilichoandikwa na chuo cha kivukoni.,KAMA UKWELI UNAOUFAHAM WEWE NI HUO,BASI SAWA NA NAOMBA UUFUATE UKWELI HUO,WAISLAM NA WAKRISTO SIO WAJINGA,USIWASEMEE,WENYEWE KWA AKILI ZAO WANAWEZA PIMA NA KUONA IPI NI HAKI NA IPI NA BATILI,NA KWA HAKIKA PALIPOKUWA NA HAKI SIKU ZOTE BATILI HUWA NI YENYE KUJIETENGA,SEMA WENGI WETU HATUUPENDI UKWELI NA NDIO MAANA TUNAPOTOKA...!!UKWELI TUUPOKEE HATA KAMA UNACHOMA YERICKO.
 

Mkuu majibu niliyokupa bado yana nguvu ya ushawishi wa hoja mujarabu!

Lakini naona umeibua maswali mepesi sana ambayo majibu yake bado yamo kwenye majibu yangu hapo juu!
 
Yericko Nyerere,

Ukimsoma vizuri Mohamed Said, kataja kwingi kuwa kitabu chake alichokiandika amlazimishi mtu yeyote kukiamini wala kukikubali.

Kitabu kina miaka 15 na kinakwenda toleo la tatu mpaka sasa serikali imeshindwa kuuona uchochezi wa Mohamed Said, wewe ambaye unaosema ni uchochozi umeshindwa kuthibitisha.

Hiyo historia iliyoandikwa kwenye hicho kitabu wanayoipima ni watanzania wao ndiyo wana maamuzi ya kukipuuza au kukikubali wewe usitake kuwasemea watanzania.
 
Last edited by a moderator:

Kuna mengi ya kujifunza katika hii mada, hasante wachangijai na muanzishaji. Hapo juu umesema kuna waongo ni kina nani na uwongo wao ni upi? Dhumuni la swali langu ni mambo mawili nahisi labda maswali yako kwa Mohamedi Said tayari yalikuwa yamejengwa katika dhana kwamba ni muongo au kwamba katika hii mada tayari kuna wao waongo na sisi wa kweli ambayo nafikiri ni mwanzo mbaya kama tunataka kupata faida kwa wote. Otheriwse nimependa maswali yako uliyomuuliza Mohamedi Said.
Na itakuwa vyema kama unaweza kuturudisha katika mada na kama vipi weka update ya yale muhimu kwenye post yako "mama" ili iwe rahisi kujua tuko wapi. Kwa sasa ishaanza kuwa shaghalabagala.

Angalizo: sina baya moyoni au juu yako.
 
Mkuu majibu niliyokupa bado yana nguvu ya ushawishi wa hoja mujarabu!

Lakini naona umeibua maswali mepesi sana ambayo majibu yake bado yamo kwenye majibu yangu hapo juu!

THE BIG SHOW,

Amekujibu majibu muruwa na kaweka hoja hadwarani.

Ni hiari yako kukubali au kukataa.

Nakumbushia mkuu tuonyeshe huo uchochezi wa Mohamed Said.
 
Last edited by a moderator:
mkuu majibu niliyokupa bado yana nguvu ya ushawishi wa hoja mujarabu!

Lakini naona umeibua maswali mepesi sana ambayo majibu yake bado yamo kwenye majibu yangu hapo juu!


munakasha huuwezi..!

Lakini furaha yangu ni kwamba ukweli moyoni mwako unaujua,,

"bal akhtharu hum,laa yaagh'lamunal haqq' fahum' muugh'ridhwu
un"

"bali wengi wao sio wenye kuitambua haki,na ndio kwa maana wanaidharau"
uzuri wewe haki ushaifaham,thanks a lot.,wasaidie kuwaamsha na wengine.
 
big sHOW,

Amekujibu majibu muruwa na kaweka hoja hadwarani.

Ni hiari yako kukubali au kukataa.

Nakumbushia mkuu tuonyeshe huo uchochezi wa Mohamed Said.

Umechanganya mkuu maswali ya mdau Big Show na majibu yangu.

UTHIBITISHO wa Uchochezi wa Mohamed Said upo kwenye kitabu chake hasa anaposema waliodai uhuru wa nchi hii ni waislamu, na anakazia zaidi kwakusema kama ni sifa basi walistahili wao tu, lakini zaidi anasema Mwalimu Nyerere aliwadhulumu haki yao yakuwa kwenye historia ya Uhuru wa nchi hii.

Hilo ni sehemu kuu ya UCHOCHEZI na UHAINI.
 
Last edited by a moderator:

Mnakasha nauweza na niseme wazi nimeulinda kwa nguvu zote na nitaendelea kulinda hadhi ya uhuru wetu na wanaukombozi wetu mzee Karume na Nyerere.

Najivunia kuujua ukweli na ninaulinda dhidi ya maharamia wa historia ya uhuru, weruvu na wajuvi wamesimama imara kulinda hadhi ya uhuru wetu, silindi hadhi ya dini yangu kwakuwa naamini sisi sote ni ndugu moja na Tanzania HAINA dini.

Ukiweka udini kwene masuala yanayowahusu watanzania wote maana ya lengo lako inatoweka na kuwa mpigania DINI tu kama alivyo Mohamed Said!

Mimi tangu sasa namuona na namtambua kuwa ni MWANAHARAKATI wa KIISLAMU anaetaka kuliangamiza taifa hili kwamgongo wa historia ya Uhuru na Nyerere.
 

Ni wazo zuri mdau, japokuwa ukisoma maelezo ya awali ya uzi huu na majibu ya Mohamed yametoa picha + kubariki kile nilichosimamia, nitakaa nitulie na kujaribu kuhuisha upya.
 
Tobaaa!!! naona Big Show umeamua kuvunja kabati la hekima leo.
 
Yericko Nyerere,

Ndiyo maana nakuambia ujakisoma hicho kitabu "Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes"

Mohamed Said ajasema kuwa uhuru wa Tanganyika umeletwa na Waislam alichofanya kuwaleta wale waliotoshwa na historia.

Mohamed Said, yupo atakueleza Wakiristo ambao walipingania uhuru kawataja kwenye kitabu chake.
 
Last edited by a moderator:
Weka bayana kipengele hadi kipengele kama kweli umesoma kitabu chake kuthibitisha unataja kama uchochezi.
 

Lugha yako kaka, lugha yako kaka, lugha yako.
Jifunze adabu ya majadiliano.

Nani haramia humu ndani?
Hapa tunajadili mada.

Haijazidi wala haijapungua.

Hakuna asemaye Nyerere si kiongozi wa harakati.
Wala mimi hakuna nimesema kuwa hakupata kuwa kiongozi wa TANU.

Nisemalo mimi ni kuwa historia imewatupa nje wengi walikuwa kabla
ya Nyerere na waliokuwa pamoja na Nyerere.

Upungufu huo ndiyo niliouonesha katika kitabu changu.

Kama wewe unaona kuwa mimi kuonyesha mchango wa Waislan ni
kupigania dini yangu sawa huo ni msimamo wako na ni lazima niuheshimu.

Kukubaliana kutokubaliana ndiyo moja ya nguzo za mjadala.

Nimekupa changamoto na habari kuhusu KUDHARAULIWA kwa kitabu cha
TANU kilichoandikwa na Kivukoni College.

Je una la kusema katika hayo?

Hadhi ya Nyerere na Karume wewe huna uwezo wa kulinda.
Hadhi zao zitalindwa na historia zao walizoacha nyuma.
 
Katika gazeti la tazama la leo tarehe 15/1/13 kuna mwandishi wa makala bwana Kusupa ameeleza kwa kina nani aliyeanzisha taasisi ya EMWS na chanzo cha mgogoro wa EMWS, ushiriki wa AGA Khan na Aga Khan anawasilisha maslahi ya nani.Nimeshindwa kuiweka hiyo nakala hapa lakini nadhani ingeweza kupitiwa na wasomaji na kupitia changamoto zake, pamoja na kwanba gazeti lenyewe sio linakubalika sana lakini unaweza kupata makala ambayo ikakufungua kwa hoja yake.
 
Swadaka Allahu L'azwim. Umetoa kitu mujarab kwa wakti muafak. Mola akuzidishie zaidi na zaidi kwani wao wanajifanya vipofu hawaoni, viziwi hawasikii na mabubu hawa semi na adhabu yao ipo mahsusi kabisa.
 


ukiachilia mbali tofauti zetu zote za dini,sisi sote hapa tumezaliwa na kuikuta tanzania ipo huru na amani lazima tuendeleze utamaduni huu,na hatupo hapa kudiscuss udini au kutamba ya kwamba dini ya fulani iko bora zaid ya mwingne,kila mtu anajua thamani ya dini yake,na moyoni mwake anajua fika kama yupo njia ya haki ama amepotoka,,

binafsi sion wapi ndugu mohammed alipopotosha,kama kuusema ukweli na kuisema haki iliyofinywa ni uchochezi basi jamhuri inamfaham huyu mtu,na yupo wala hajifichi,yumkini wangemtafuta na kumfungulia mashtaka,lakini wamemwacha kwa kuwa wanajua uhalisia wa hoja zake,wewe kama unaona ni mchochezi na una vithibitisho,huoni kama haulifanyii haki taifa lako??kwanini sasa usiende kwenye vyombo vya sheria kumshitaki??kwanini unakuja kujenga tension hapa jukwaaani na kwa jamii kwa ujumla??nani sasa mchochezi na mhaini wewe au yeye??
Thats why nashikilia msimamo wangu wa kwamba mchochezi na mhaini ni wewe yericko.
Tushakugundua sasa,na tunashukuru kujua rangi zako sasa.
 

Wazungu wanasema ''off the cuff.''
Jibu lako ni la kukutoka tu.

Nimekushauri uende Idara ya Historia ukaulize hadhi
ya kitabu cha Kivukoni.

Kwa hakika ikiwa unataka faida ya elimu fanya hivyo.

Nakupa ushauri ambao utakusaidia maishani kama unataka
kuja kuwa msomi makini wa kuheshimika.

Ushauri wangu ni huu.
Siku zote kiwache kichwa chako wazi.

Usikifunike kichwa chako.

Kiruhusu kila siku kiwe wazi kupokea elimu
mpya hata kwa wale unaowaona hawajui kitu.

Ungelikwenda Idara ya Historia pale Mlimani ungepata
mengi tena bila ya gharama yoyote.
 

Mkuu katika kukujibu na kuutawala mjadala huu nimesimamia uthabiti na utajiri wa misamiati ya lugha ya kiswahili.

Kwa hilo tu sina kosa kukwambia wewe ni muharamia wa historia ya uhuru wa tanganyika.

Juu ya hoja yako kuhusu kitabu cha TANU nimeijibu tena kwa mang'amuzi ya nera!

Rudia kulisoma upya na kwaumakini jibu lile mzee wangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…