Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

swadaka allahu l'azwim. Umetoa kitu mujarab kwa wakti muafak. Mola akuzidishie zaidi na zaidi kwani wao wanajifanya vipofu hawaoni, viziwi hawasikii na mabubu hawa semi na adhabu yao ipo mahsusi kabisa.


naam,kheri insha allah,,
"maa' aamanat kablahum min kariyatin akh'lak'nahaa,afahum yuu'minuun"??

Hawakuamini wengi waliopita miongoni mwa ummah nyingi kabla yao,je itakuwa hawa??bila shaka hawataweza kuamini,lakini ukweli lazima usemwe..
 
Mkuu majibu niliyokupa bado yana nguvu ya ushawishi wa hoja mujarabu! Lakini naona umeibua maswali mepesi sana ambayo majibu yake bado yamo kwenye majibu yangu hapo juu!
Y Nyerere, Kitaalamu siku zote kwa wasomi huwezi kujadili utafiti kwa kuweka maneno mawili matatu. Ni vizuri na wewe ukafanya utafiti na kuandika kitabu cha kupingana na hicho cha Mohammed said. Kwani utafiti siku zote unapingwa na utafiti na si vinginevyo. Chukulia jambo hili kisomi zaidi.
 
Mohamed Said twashukuru umetoa faida nyingi sana na umeeleweka vyema,waweza pumzika huyu Yeriko nyerere tuachie sisi hana hoja hana uthibitisho,hicho kitabu anachong'ang'ania pengine hata jalada lake halijui.Uwezo wake ni mdogo sana.Imamu shafii anasema kila alipofanya mjadala na mtu mjinga alishindwa,lakini kila alipofanya mjadala na mtu mwenye elimu alishinda.huyu maarifa yake ni yale ya unalishwa biskuti unaambiwa mwili! ujinga mtupu
 
Last edited by a moderator:

Unasema ukweli kuwa historia ya TANU imekamilika katika kitabu cha Kivukoni.
Swali langu ni hili.

Nakupa swali moja tu unipe jibu.

African Association iliasisiwa na Kleist Sykes kama katibu.
Huu ulikuwa mwaka wa 1929.

Ofisi ya TANU hapo ilipoasisiwa TANU 7 Julai 1954 hiyo nyumba
kajenga Kleist katika ya 1929 - 1933.

Nyaraka alizotumia John Illife katika kuandika historia ya African
Association alitumia nyaraka za Kleist.

Hiyo TAA ikaja kuongozwa na Abdulwahid mtoto mkubwa wa Kleist
kuanzia 1950 - 1954.

Abdu ndiye aliyempokea na kumtia Nyerere kwenye uongozi wa TAA
mwaka 1953.

Katika kitabu cha Kivukoni yote haya huyakuti.
Sasa ndiyo linakuja swali.

Swali lenyewe ni hili.
Historia hii unaweza kuiita imekamilka?

Historia ambayo hata chanzo cha siasa imeamua kupuuza?
Unaweza kweli kuichukua hii kama historia ya TANU?
 



swadakta kabisa.,
mimi namsihi ni bora kwake kama hafam basi na awaulize wenye kujua haya mambo,kujifanya waweza kuleta hoja kisha ukashindwa kuitetea ni kujidhalilisha na kuwadhalilisha wale watakuwa upande wako kishabiki pasi na kujua uhalisia wa hoja wenyewe,
kila ukweli unaposemwa kukimbilia kuuficha hailet tija,uache ukweli uvunje bufuru la kichwa cha uongo,uzandiki na unafiki,.
 

Nirudie tena kauli yangu iliyo kwenye uzi huu kuwa, Ni kweli Historia ya Uhuru Wetu inamapungu na inahitaji kuhuishwa. Lakini kutunga simulizi ya wazazi wako na dini yako na kuifuta rasmi ile ya TANU iliyopo hata kama inampungufu, huku ukihalalisha kiimla kitabu chako kuwa ndio historia ya Uhuru wa Nchi hii ni jambo la kufedhehesha sana.

Imani yangu na uelewa wangu utasimama mithiri ya mlima sayuni kuamini kuwa Mohamed Said ni Mchochezi na Muhaini, walau nimejenge hoja toka kwenye kitabu chako lakini umeruka kimanga, yatosha kuamini niaminicho, na ninashukuru werevu na wajuvi wake kwa waume, waislamu kwa wakristu wamegoma kuburuzwa na Mohamed Said.
 
kijana huna hoja,hata ukitumia maneno ya kashfa kiasi gani kwa Mohamed Said hata kujibu upuuzi wako na wala hata kugusa kwa maneno unayojaribu kuyatumia.Kinachofurahisha umeshindwa hoja unaanza kumshambulia binafsi,kasome upya muda bado unao hujachelewa.Porojo zako tushazichoka huna jipya.Rudi kwa waliokutuma waambie wakupe matusi mapya.
 
Last edited by a moderator:

Uungwana ni jambo jema sana ndugu yangu.

Ikiwa unataka tujadiliane jibu hoja zangu zilizoelekezwa kwa mzee Said.

Jitahidi usishikiwe akili ndugu yangu.
 
Last edited by a moderator:
Uungwana ni jambo jema sana ndugu yangu.

Ikiwa unataka tujadiliane jibu hoja zangu zilizoelekezwa kwa mzee Said.

Jitahidi usishikiwe akili ndugu yangu.

Naona ndugu zangu mechi yetu imevurugika.
Chandimu kimetawaliwa na rafu nyingi.

Kama ujuavyo chandimu hakina mwamuzi
wachezaji wanajiamulia sheria za mchezo wenyewe.

Matusi yanatawala mjadala wetu.
Hili si jambo la kiungwana.

Rai yangu mimi ni hii.

Sina mamlaka ya kuufunga mjadala ila nashauri kitu kimoja.
Na hapa najipa madaraka.

Wanaukumbi waniulize lolote katika kuanzishwa kwa African
Association hadi kufikia TANU na jinsi uhuru ulivyotafutwa, nani
kafanya nini, kwa nini yule alitoka TANU nk. nk.

Nimeona tutumie njia hii kwa sababu kwingi nilikohadhiri kipindi
cha maswali na majibu hung'ara sana hata kushinda mhadhara
wenyewe.

Huenda njia hii ikapunguza na kushusha joto la ghadhabu kati yetu.

Nawasilisha.
 
uungwana wako uko wapi ili nawe uwahusie watu kufanya uungwana? kumwita Mohamed Said mchochezi na mhaini bila ushahidi ndio uungwana? Tatizo lenu wagala mshazoea kulishwa maneno bila ya kuyatafakari.Mwalimu Mohamed Said ameshafungua milango ya maswali uliza uelimike
Uungwana ni jambo jema sana ndugu yangu. Ikiwa unataka tujadiliane jibu hoja zangu zilizoelekezwa kwa mzee Said. Jitahidi usishikiwe akili ndugu yangu.
 
Last edited by a moderator:

Haahaa umenivunja mbavu mkuu, kweli chandimu kimevurugika!

Mkuu ondoa shaka, mjadala bado upo hai na ninashukuru kuona umeweka wigo mpana wa mjadala huu,

Tunayo fursa nzuri ya kukosoana kwa hoja na kushindwa kwa hoja bila jazba wala kejeli.

Tujadiliane kwamafaa ya taifa letu.
 
Ndugu yangu Mohamed Said,

Unautambua mchango wa Chifu Maleale kwenye harakati za ukombozi wa nchi hii?

Je yumo kwenye historia ya uhuru wa Tanganyika na mashujaa wetu?
 
Ndugu yangu Mohamed Said,

Unautambua mchango wa Chifu Maleale kwenye harakati za ukombozi wa nchi hii?

Je yumo kwenye historia ya uhuru wa Tanganyika na mashujaa wetu?

Cheif Thomas Marealle Paramount Chief.
Anatokea Marangu.

Rafiki wa Abdulwahid Sykes.
Rafiki yake Ally Sykes.

Abdu Sykes akimtania Chief Thomas Marealle.
Akimwambia,'' Unajua Tom kwa nini wewe Waingereza
wanakuita ''Chief'' hawakuiti ''King?''

Abdu alikuwa anaendelea na kumwambia, ''Waingereza
wanaona wakikuita wewe ''King'' utafanana na Mfalme
George.''

Wote wataangua kicheko.
Hata hivyo siku zote Abdu alikuwa akimuita Chief Marealle ''King
Thomas Marealle.''

Siku moja nimekutana na David Marealle.
Tukiishi jirani lakini hatukuwa na mazoea.

Siku tulipopata wasaa wa kuzungumza akanambia.
Alipokuja Dar es Salaam kwa mara ya kwanza alipokewa
na Abdulwahid Sykes.

Alitoa sifa nyingi sana za shukurani nami nikamfahamisha kuwa
huyo mie ni mzee wangu.

Sasa kabla hatujakwenda mbali sana nakuwekea hapa kitu ustaladhi nacho
Insha Allah:

Shukurani

''...kazi hii isingewezekana kama isingekuwa kwa msaada wa hali na mali nilioupata toka kwa Ally Sykes.

Ally Sykes alinipa wasaa wa kuzungumzanae kila nilipotaka, akanieleza madhila ya ukoloni pamoja na kuwa ni mtu wa shughuli nyingi.

Yeye hivi sasa anaendesha biashara yake toka ofisi yake iliyoko katikakati ya mji wa Dar es Salaam.

Aliniruhusu nisome majalada yake binafsi, barua zake, shajara na kumbukumbu nyinginezo za ukoo wa Sykes.

Ally Sykes alinifahamisha kuwa kumbukumbu hizi zilikuwa ndani ya sefu ambayo haikupatwa kufunguliwa kwa zaidi ya miaka therathini.

Nikiyapitia majalada yake nilishangazwa na utaratibu wa Ally Sykes wa kupanga kila kitu na kila kipande cha habari mahali pake hata kingekuwa kidogo namna gani wakati ule wa harakati.

Ally Sykes ana barua ya mwaka 1954 iliyoandikwa kwa penseli toka kwa Zuberi Mtemvu kwenda kwake akimtaarifu juu ya mazungumzo aliyokuwanayo (Mtemvu) na Nyerere kuhusu yeye na TANU; stakabadhi ya hundi ya posta toka kwa Ally Sykes kwenda kwa Japhet Kirilo wakati wa Mgogoro wa Ardhi ya Wameru.

Nakala ya barua isiyokuwa na tarehe kutoka TAA kwenda kwa Malkia Elizabeth iliyotiwa saini na viongozi wote wa TAA:

Rais Julius Nyerere, Makamu wa Rais Abdulwahid Sykes, Katibu Mkuu Dome Okochi, Naibu Katibu Dossa Aziz, Mweka Hazina John Rupia, Naibu Mweka Hazina Ally Sykes ikimpongeza Malkia kwa kutawazwa.

Barua ya mwaka 1952 toka kwa Rashid Mfaume Kawawa kutoka Bukoba kwenda kwa Ally Sykes ikimfahamisha juu ya hali ya siasa katika Kanda ya Ziwa.

Nyaraka kutoka kwa Lady Judith Listowel, Kenneth Kaunda, Julius Nyerere, Kasela Bantu, Chifu Thomas Marealle ...orodha haina mwisho.
..''

Kutoka (''Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes...'')

Nyingi katika hizi ni barua ambazo Ally Sykes alikuwa akipokea kutoka kwa wazalendo hawa waliokuwa wanapambana na wakoloni.
 
yericko nyerere rudi uje uchukue darasa huku.
Ndugu yetu mohamed ni mkwasi wa historia kwa kweli.
 

Nashukuru kujibu kuwa unamfahamu na historia kwaufupi umeitoa,

Lakini tatozo letu katika mjadala huu ni lilelile, mkuu hujajbu swali la msingi kuwa kwanini Chifu huyu hayumo katika kitabu cha historia ya uhuru wa Tanganyika kilichoandika na chuo cha Kivukoni ilihali yeye ni mkristu?
 
Nimesoma thread hii na lazima niseme kuwa Y Nyerere hutendei haki mjadala huu.

Kama kweli umekisoma kitabu na kukielewa kiasi ya kwamba kumwita ni mchochezi, tuletee wapi kwenye kitabu, iwe ni chapter, page paragraph yoyote ile ili na sisi twende huko tukasome. Accusations zako ni hewa kwa ufupi
 

Unajua Bwana Nyerere ungejituliza tungekuwa na mjadala mzuri sana.
Hivi unajua kuwa sijamaliza habari za Chief Marealle?

Nilitegemea utakuja na maswali kuhusu mchango wake katika TANU kama
upo na mambo mengine.

Sasa unaniuliza habari za kwa nini hakuandikwa na Kivukoni katika kitabu chao
cha historia ya TANU.

Swali hilo si ungekwenda kuwauliza CCM?
Maana wao ndiyo warithi wa TANU na hicho kitabu kimeandikwa na wataalamu wao.

Lililonishtua zaidi unasema habari za Ukristo.
Mbona ndugu yangu unapenda chokochoko?

Kwenye kitabu changu Chief Marealle nimemtaja.
Hivi umeshindwa kuona ule udugu baina ya Abdu na Chief Marealle?

Hilo si kielelezo tosha cha hali ya mambo yalivyokuwa huko tulikotoka?

Jitulize na jishughulishe kufikiri.
Usiwe na papara ya kuandika, kuandika, kuandika bila ya tafakuri.
 

Mkuu umetoa historia kwa ufupi na kwamtu yeyote msomi anapata picha bila hata kuambiwa kuwa Chifu huyu alihudumu vipi katika harakati za ukombozi, ndiomaana katika shukrani zangu nimesema wazi kuwa nashukuru kuona unamfahamu na umetoa historia yake kwa UFUPI.

Mpaka hapo natambua unafahamu zaidi wasifu wa chifu huyu, ama kwakuongeza maneno mawili ni kuwa alikuwa mfadhiri wa siasa za Mzee Nyerere (kiuchiumi).

Kuhusu swali la kwanini hayumo kwenye historia ya uhuru, nimelielekeza kwako likijenga nadharia ya kitabu chako kuwa wazee wako waliachwa kwa hila/ghiriba za Mwalimu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…