Ndio historia ya TAA maana kabla ya mapinduzi ya Abdul Wahid kumpindua baba yake na kuongoza, chama cha TAA kilikuwa kijiwe tu cha wazee wa Kariakoo tena niseme gerezani.. Hivyo enzi hizo wakristu wengi walikuwa wakiishi kuanzia Ilala kota Msimbazi na kuelekea Magomeni na hawakuwa sehemu ya kijiwe hicho.KUMBE TAA,hapo mwanzo ilikuwa kijiwe cha wazee wa kariakoo,kama ilivyokuwa SAIGON,asanteni sana kwa darasa
Hivyo waliposhika kina Abdul uongozi ndio wakaanza kuchukua wanachama kutoka sehemu mbali mbali nchini pasipo kujali dini wala makabila na kukifanya chama hicho cha kisiasa. Walimhitaji Nyerere sana tu kutokana na elimu, kipaji na uwezo wake ktk kuwaunganisha Watanzania wote, jambo ambalo baadhi ya wanachama kina Takadir hawakupenda kuona TAA inachukua hata watu kutoka bara. Sasa tujiulize kama hawa watu kina Takadir hawakutaka watu kutoka bara, hicho chama cha TAA kingekuwa kinapigania Uhuru wa kina nani?