Mkuu iko hivi,
Waarabu walifika pwani ya Afrika mashariki kwa karne nyingi sana, kabla ya wageni wowote kuja na kilichowaleta ni biashara, japo kuna baadhi ya watu wanaamini kuwa Waafrica ndio walikuwa wa kwanza kwenda bara Arabia kufanya biashara za kupeleka Madini (Vito) na pembe za ndovu na Vifaru na baada ya biashara kukolea ndio na waarabu wakaanza kuja Afrika mashariki
Wareno walifika pwani ya Africa mashariki kwenye miaka ya 1400, na walikuwa wanakuja wakitafuta njia ya kwenda India kufata viungo (spices), hivyo safari yao walikuwa wakisafiri kwa kuambaa pwani kwa pwani wakipita nchi zote za pwani ya Afica Magharibi na walipofika Angola wakaplan kuweka base pale, kisha wakaenda mpaka south africa pale walipokuta bahari mbili zinaungana na ndipo wakapaita Cape of good hope, kisha wakaanza kupanda kuja juu ya africa na walipofika Mozambique wakaona iko kwa kiasi fulani inacorrespond na Angola (location, latitude, Eastings) hivyo wakaweza point yao (BAse),
wakati wanakaribia pwani ya Tanganyika (Kilwa)walikutana na mashua nyingi sana za wachuuzi wa kiarabu ambao walishakuwa kwenye pwani ya Tanganyika kwa muda mrefu. Na ndipo wareno walipouliza njia ya kwenda india na waarabu ndio waliowaonyesha njia ya kwenda huko na msimu wa kwenda huko(Upepo), na ndipo wale Wareno walipoiita hi bahari ya East Africa kuwa Indian Ocean(Way to India)
Wareno hawakuwa na nia ya kuifanya East Afrika kuwa Koloni lao, kwani Mwarabu alishakuwepo, wao walibase na Mozambique na ile forty Jesus ilikuwa ni Transit point ya kusubiri Upepo wa kupeleka Meli zao India
Sio Rahisi kusema moja kwa moja Mwarabu hakushiriki biashara ya Utumwa, tukizungumzia miaka ya 1800 ni kweli biashara ya utumwa ilikuwa inapigwa vita duniani, lakini kabla ya hapo ilikuwa ni biashara ya Dunia nzima Wazungu, Waarabu, Wayahudi wote walishiriki hiyo biashara
Kuna kizazi cha Waafrika kiko kule India na kilipelekwa na Wareno kule kwa kazi za mashamba na kama Askari