Uchochezi wa Mohamed Said na dhihaka kwa Wapigania Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar

weka hapa jamvini acha porojo kaka,kama nidhamu ya majadiliano uliivunja mapema sana kwa Mohamed Said kwa maneno yako ya kejeli na dharau.Kulitaja kanisa ktk kuleta uhuru wa tanganyika ni kiroja.ushiriki wake ulikuwa wa kinafiki na kiini macho.Historia itabaki na haitabadilishwa kama mnavyotaka kufanya.
 
Last edited by a moderator:

Duuuh umeathirika ndugu!

Amini kama unavyoamini kuwa uislamu pekee ndio ulioendesha harakati za ukombozi wa Tanganyika.
 
Last edited by a moderator:
Fanya munakasha kwa lugha za kiungwana tu utaeleweka dharau na kejeli wala hazikupi ushindi wowote, Mohamed Said kajishusha mpaka level yako ili muelewane ni hiari yako kufuata huu ushahuri au kuuacha.
 
Fanya munakasha kwa lugha za kiungwana tu utaeleweka dharua na kejeli wala hazikupi ushindi wowote, Mohamed Said kajishusha mpaka level yako ili muelewane ni hiari yako kufuata huu ushahuri au kuuacha.
Sasa kejeli imetoka wapi? Kwani wewe unajua level yangu? Watu wengine bhana...
 
Wakati TANU inazaliwa ahali yako Mzee Mohamed Said alikuwa na miezi kadhaa tangu azaliwe. Aliona nini sasa wakati huo? Hakuna aliyepigania uhuru wa Tanganyika. Waingereza walitutawala hapa kama waangalizi waliokuwa wameteuliwa na UN. Hawakuwa wabishi kuondoka walipotakiwa kufanya hivo. Wala hakukuwa na mikutano ya Lancaster kama wenzetu. Hii historia ya kupeana nauli, kupikiana chai, kupeana lifti kwenye gari,..., kama ndio upiganaji wenyewe, basi hata tuliowachangia ili wafanye harusi mke/mme yule si wao peke yao.

Ni vizuri kukumbuka pia Mwalimu aliacha kazi ya mshahara mzuri kwa ajili shughuli hii ya kurudisha uhuru wetu. Pengine umasikini huu wa kupewa nauli, chakula na chai ulichangiwa na hilo pia kwa kuwa tayari alishakuwa na familia.
 
Last edited by a moderator:

Sa...ndo unaona wivu?!
 
Sa...ndo unaona wivu?!

Hapana sioni wivu.
Wivu kama choyo ni kitu cha watu dhalili.

Si sifa ya mtu kujinasibishanacho.

Nimeandika kipande hicho kwa mshangao kuwa inawezekanaje
kile kilicho dhahir na hadhir hakijulikani kinaulizwa kitu kisichofahamika.
 

Ukiandika kwa kejeli mjadala utavurugika ile nafasi ya mazungumzo ya kiungwana utatoweka.

Hivyo hivyo ulivyoandika hebu andika kwa adabu.
Nitakueleza hayo uliyosema kwa kejeli na dharau.

Nitakudokeza.

Nyerere akipokea hela nyingi kupita alizokuwa akipata akiwa mwalimu ukiacha kipindi kifupi
mwaka 1954/55.
 

Ikiwa kweli una haja ya kufanya mnakasha na mimi basi staha itangulie.

Niulize swali au maswali kama watu wawili wanaoheshimiana wako katika
mjadala wa uso kwa macho.

Uliza tena hili swali laikini ondoa hizo kejeli.
Insha Allah nitakujibu.
 

Tutulie tuendelee na mnakasha.

Inawezekana kuwa huyu sheikh alikuwapo na kisa cha yeye kutofahamika yawezekana hakuwa maarufu.

Hapana haja ya kusuguana na ndugu yetu kisa tu ati kaleta jina la sheikh ambae sisi hatukupata kumfahamu.

Leo hii kuna masheikh wengi Kibada, Nyamisati, Kilwa na kwengineko.
Wangapi wanawajua masheikh hawa?

Tumuache Yericko aendelee na darsa yake ili tupate faida.
 
Kejeli yangu kwenye post hiyo ni ipi? Tarehe 7.7.1954 ulikuwa na umri gani mzee. Mwalimu aliacha ajira nzuri tena ya kudumu akaingia kwenye siasa ambako kulikuwa hakutabiriki. Wewe umemsimanga kwa kila namna kwa misaada hii midogo toka kwa wazee wako hawa. Unajua vizuri kwamba Mwalimu ameacha madaraka ya nchi hii akiwa masikini pengine kuliko alivyoingia madarakani. Sifa kama hii wanayo viongozi wachache sana barani humu.

Hebu fikiria kama familia ya Sykes ingeupata urais wa nchi wangekuwaje na nchi hii haikuwa yao ya asili.
 
Ikiwa kweli una haja ya kufanya mnakasha na mimi basi staha itangulie.

Niulize swali au maswali kama watu wawili wanaoheshimiana wako katika
mjadala wa uso kwa macho.

Uliza tena hili swali laikini ondoa hizo kejeli.
Insha Allah nitakujibu.

Hapa ulikuwa unamkosoa mwanakijiji kwa kuandika kiswahili fasaha kabisa..darasa
By Mzee Mwanakijiji


Yericko asante kwa darasa; keep it up.
Mkuu labda unaweza kunionyesha nilipokukejeli? Ni hapo nilipotaka kujua papers zinaitwaje kiarabu?
Naona inabidi tuwe wanyoofu sana tunapotoa hoja maana naona kama vile umepata ka loophole fulani ka kukwepa hoja.
Na mimi nilikuwa nataka kujua kutamka papers kwa "sekne"...kuna ubaya hapo?
 
Mohamed Said ,nilikuwa naomba ufafanuzi kidogo kwenye kipande nilichoweka hapo chini. Umeelezea kifo cha Kighoma Malima halafu baada ya kifo tu ukaweka hiyo sentensi ya Cardinal Polycarp Pengo kutoa tamko kuhusu kumdhibiti Kighoma Malima kwa sababu uamuzi wake wa kugombea nje ya CCM.
Hii ni style ya uandishi wako tu au ulikuwa unalenga kulihusisha Kanisa na kifo cha Malima kwa kuchomeka hiyo sentensi ya mwisho?
Kwa sababu hilo tamko ni shutuma nzito kwa cardinal , unaweza ukatuonyesha ni wapi iwe kwenye gazeti au record yeyote aliposema hayo?
 
umekurupuka kujibu,sikatai kwamba hakuna wakristo walioshiriki harakati za uhuru,la hasha.Ninachopinga ni kanisa kulihusisha na harakati za uhuru
Duuuh umeathirika ndugu!

Amini kama unavyoamini kuwa uislamu pekee ndio ulioendesha harakati za ukombozi wa Tanganyika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…